2. Gundua Chaguzi Zako

Discover Your Choices

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Deusdedit C. Kanunu

Gundua jinsi uchaguzi wa mawazo na imani unavyohusiana na tumaini, ujasiri na ukuaji wa kiroho.

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 2  |  Kitini kamili cha D2

Onesha ni kwa jinsi gani chaguzi zetu zinahusiana na Matumaini na Kujiamini kwetu!

Mchoro wa uchaguzi unaoonyesha kujiamini katika Mungu.

Njia ya Maisha ya kiroho

  • Inaanza na Maisha Mapya katika Kristo
  • Hatua Tatu
  • Hatua ya 2 - Pata Ujasiri katika Neno la Mungu lenye Nguvu

Ukweli kutoka katika Uongo - Msingi wa 2

“Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu” (1 Yoh 2:14).
  • Mhimu. “Una nguvu!”
  • Lengo. Jenga Ujasiri.
  • Tatizo. Hatujiamini kama tulivyo ________.
  • Matokea. Tunajisikia dhaifu na Tumeshindwa.

Uwanja wa Vita

  • Asili ya Mioyo yetu ni _______, “Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati...” (Marko 7:21).
  • Moyo mpya ni mzuri wote, “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho” (Rum 8:5).
  • Akili zetu ni Uwanja wa Vita. Jambo la Maana hapa ni juu ya nini tunakiamini na kipi tunakitegemea katika kuamini kwetu.“na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu” (Rum 12:1-2; Efe 4:23).
  • Nani anaendesha kufanikiwa kwa akili zetu - Eva
  • “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani” (Efe 6:11).

Kivuli cha Mtu

  • Je, Una nguvu? Kitu gani kinakufanya uwe dhaifu?
  • Je, wakati mwingine hujishutumu na madai haya ya ushindi na uko tayari kuishi kama umepoteza? k.m. "Hivi ndivyo nilivyo, nadhani."
  • Yohana alisemaje ukilinganisha na tunavyoamini ndani? Unaeza kuona namna gani tumaini lako wakati mwingine linavuja kutoka katika roho yako?

Kujitambua sisi wenyewe

Maeneo mawili hasa yanayohitaji kuimarishwa

Maamuzi ya fikra zetu (___akili____)

Kuamini kwamba Njia za mungu siku zote ni nzuri (___Imani____)

1. Maamuzi ya Fikra na Chaguzi zetu

  • Wakati unaposhindwa au kupigwa, kumbuka msemo fupi katika akili yako (majaribu).
  • Angalia jinsi chaguzi zetu (yaani, akili) huathiri sana hisia zetu.
  • Kuunganisha kile tunachoamini kwa uchaguzi wetu. ____________ njia:
  • Akili zilizoshindwa. “siwezi kufanya hiki, sawa .” “Nafikiri siwezi.” “Hakuna mtu anataka niwe rafiki yake.”
  • Mwamini Mungu. “Bwana ni Mzuri!” “Asante kwa kunisamehe!”
  • Kujiamini. “Mimi ni mjanja!”“Hili naliweza.”
  • Ukiwa pale tu tunapoamua kufuata fikra zetu, Je, tunaweza kuzifuta na kuchukua fikra mpya

2. Njia za Mungu siku zote ni Nzuri - Imani!

  • Kukua Kiroho ni jambo la maana na linapimwa kwa kukua kwetu kwa Imani katika Njia za Mungu (Ayubu 17:9; Zaburi 1:6).
  • Utii hutenda maaajabu - hata kama hujisikii kupenda au kama inaonekana haiwezekani
  • “Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu” (Efe 6:17).

Chujuio la Kujiamini - Chaguzi 3

Chaguzi tatu za kujiamini.
  • Chaguzi nzuri ni zile zilizo na maana kwa Mungu
  • Maamuzi yote ya mhimu yanaweza kuwekwa katika moja ya aina 3
  • 1. Kujiamini katika Mungu (Mara nyingi ni nzuri). Ibrahim alimuokoa Lutu (Mwanzo 12:1-4; 14:1-24).
  • 2. Ujasiri uliopotea (Mabaya). Unakuwa na ujasiri lakini katika vitu ambavyo siyo vya Ki Mungu. (Mfano Utajiri; Ibrahimu alidanganya Mwanzo 12:10-20; Yoshua alipigana na mji wa Ai Yosh 7).
  • 3. Ukosefu wa Ujasiri (mabaya). Kutokuamini katika Mungu (“Ina nguvu” Nahumu 13:31; Sauli 1 Samweli 15:24).
  • Kumbuka. Kujiaminisha wewe mwenyewe aidha kwa hali ya chini au ya juu ni mbaya kwa sababu hakuna uhusiano na Mungu

Tafsiri za Imani zinazosaidia

  • Kila Tafsiri inahitaji kubeba "Imani" ( mfano, Imani, Ujasiri, kuamini).
  • Mfano 1. Kutokuwa na Usalama:
  • Mfanoe 2. Uaminifu.
  • Mfano 3. Upendeleo binafsi.

Utendaji kazi katika Maisha. Njia ya Urejesho

  • Akili. Kumbuka neno au mstari unaokuja katika akili yako
  • Ujasiri mzuri. Amini katika Njia za Mungu na buni mara kwa mara __________________.
  • Ujasiri uliopotea (sanamu) na ukosefu wa ujasiri husababisha uchaguzi mbaya unaosababishwa na mihemko, mwili, mahusiano, na matatizo ya kiroho kwa sababu ya ____ _____________ katika Mungu.
  • Kukuwa hutokea tunapotubu kutoka katika matendo ambayo siyo sahihi ya siyo mwamini Bwana na kisha tunaanza kumwamini Bwna
  • Kuitambua dhambi kunapelekea kutubu, kurejeshwa, kuamini katika Bwana na kufanya uchaguzi sahihi.
  • Muhimu. Una nguvu. Rudisha umiliki wa akiki yako. Amini na mtii yeye!

Kushuhudia Maisha yako

  • Ni neno gani analolitumi shetani kukutesa nalo? ( majaribu)
  • Wakati gani unajikuta wewe mwenyewe unapata mashaka na njia za Mungu kama vile ni vizuri kila wakati?

Kazi za Kufanya

  • Kamilisha zoezi namba 1. Oanisha vizuri.
  • kamilisha zoezi namba 21:Tafsiri za Imani.

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 2  |  Kitini kamili cha D2