1. Chanzo cha Maisha (1-3)

Kiini Cha Maisha: Gundua Siri ya Mafundisho Makuu

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Simulizi ya Mafanikio · Mtazamo Una Maana · Badiliko Lazima Lije

Somo la Kiswahili kuhusu tumaini, mtazamo wa kibiblia, toba na mabadiliko yanayohitajika katika maisha na kanisa.

Sauti na Video

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 1  |  Kitini kamili cha Kiini Cha Maisha

(1) Simulizi ya Mafanikio

  • Fikiria kuhusu puto lisilo na hewa au Mwewe bila upepo
Mchoro wa somo la Chanzo cha Maisha (1-3)
  • Lakini Kanisa linashindwa
  • Wachungaji ni Waovu

Roho ya kushinda ipo hewani. Tunawezaje kuwa kama Mungu alivyotuita?

Kitu gani kifanyike?

  • Rejea Katika Maandiko “Basi tuseme nini juu ya hayo?Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?”(Warumi 8:31).
  • Je, si katika nyakati za giza, tuonapo Mungu akiingilia kati kiajabu? Kwa Abram, Daudi, n.k.
  • Simulizi za Mungu pamoja na miujiza hurejesha tumaini.
“Mkiisha kuyatimiza yote, kusimama imara” (Efe 6:13)

Ni neno la Mungu lenye nguvu pekee kupitia Roho Wake ambaye husogelea utu wetu na kuzalisha maisha mapya na kutupatia sura ya kiroho, nguvu na kusudi (1 Peter 1:24-25).

Hatari Yetu Kuu

  • Mungu hutuvuta sisi katika mto kwake
  • Hakuna chenye nguvu kama yake Mungu
  • Usivute mashua pembeni na kutoka!
  • Hakuna cha kutubadilisha!
  • Simama imara na uuone wokovu wa Bwana!
  • Kiini cha Maisha kinabainisha kisababishi cha msingi juu ya mgogoro huu katika Kanisa la Kikristo na kupendekeza suluhisho la kivitendo kwa kulenga ushirikiano wa maisha ya Kimungu kuelekea ndani ya moyo wa kanisa kupitia mafunzo sahihi ya uongozi.

Tunachojifunza

  • Vita imeshindwa. Mungu ameshinda. Tunahitaji kuendelea kukumbuka nguvu ya Mungu na kumwamini yeye.
  • Bwana anatamani kutuwezesha kama alivyomuwezesha Yusufu, Danieli, Yesu ili tuweze kama wao, tunatakiwa kuwa karibu na Mungu ili aweze kutimiza mapenzi yake kupitia maisha yetu.

Tunavyoweza Kutumia

  • Je, umejeruhiwa kiroho? Maeneo gani unahisi kushindwa?
  • Yaorodheshe maeneo hayo ukianzia na lile linaloanza katika akili yako.
  • Ikiwa uliteremka katika mashua, tubu na urudi ndani ya mashua sasa.
  • Omba unakwenda kukaa naye haijalishi hali ni mbaya kiasi gani.

(2) Mtazamo Una Maana

  • Mtazamo hubadili namna tunavyofikiri, tunavyopambana na ugumu na tunavyojaribu kutatua matatizo.
  • Unaweza kuumiza au kusaidia
  • Kutazama duniani kutoka katika nafasi ni tofauti sana.

Kanisa linavyozidi kung’ang’ania mitazamo ya uongo, maumivu zaidi huingia.

Kufanya Uchaguzi Muhimu

  • Kanisa dhaifu na tabia zisizo za kimungu huonyesha kuanguka kwa imani yetu katika Kristo.
  • Dunia inavamia moyo na makazi kupitia teknolojia ya kisasa.
  • Je, tumealika uovu katika kanisa letu na makazi yetu?
  • Je, hauwezi kuona ushahidi wa kanisa dhaifu?
  • Kanisa ni zaidi ya taifa lililopo katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.
  • Mapinduzi ya uasherati yanatokea duniani.
  • Waamini ni kama askari ambao hawajathibitishwa, wasiotambua namna ya kutumia neno la Mungu.

Badiliko Linakuja

  • Badiliko lazima lije. Litakuja, lakini ni hakika pasipo utumwa duniani.
  • Ni lazima tuutambua ukweli na utupeleke katika ushindi!
  • Neno la Mungu linatosha kushinda.
  • Tunahitaji mtazamo wa kibiblia kuliko mtazamo wa kidini.
  • “Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio” (Mithali 30:5).

Hitimisho

  • Tunahitaji mtazamo wa Kimungu
  • Tunaona kitu gani?
  • Mungu anaona nini?
  • Mungu amesema kwamba tuna kila tunachohitaji.

And Nao walipomwona, walimsujudia lakini baadhi yao waliona shaka. Na Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mat 28:17-18).

Tunachojifunza

  • Kanisa duniani kote lipo katika hali ya hatari kwa sababu dunia inaongeza ushawishi katika akili zetu na maisha yetu.
  • Kanisa linasimama katika ardhi yenye fursa ya kuachana na ngozi za zamani na kuiga utukufu uliojaa ukweli wa Mungu kwa ajili yao wenyewe na wale wanaoizunguuka dunia.

Tunavyoweza Kutumia

  • Je, unafikiri kanisa lenye ukweli wa Mungu likiambatana na ahadi zake na uwepo wake, linaweza kushinda kile kinacholitisha kanisa? Au nawewe, kama mfuasi wa zamani, una mashakamashaka?
  • Fikiri kimahususi kuhusiana na mazingira yako; weka alama katika maeneo unayoona ushindi na kushindwa pia.

(3) Badiliko Lazima Lije

  • We Tunapenda kuzuia mabadiliko.
  • Lakini changamoto katika kanisa hutulazimu kubadilika.
  • Kua au Kufa!

Kuwa mshindi au utabike kushindwa. Haya ndiyo machaguo yetu.

Ushiriki wa Mungu Uliofichika

  • Kanisa la kwanza lilitawanyika, lilikimbia kila mahali, zaidi kama chungu (ants).
  • “Basi wale walitawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano…” (Mdo 11:19). “ Na sasa walikuwa Antiokia , kanisani………Walipokuwa wakihudumu…” (Mdo 13:1-3)

Tambua Msingi wa Matatizo

  • Kuongezeka kwa taarifa kumetupiga
  • Hata hivyo hakuna kiuhalisia kilichobadilika.
  • Je, kuna ndoa ngapi za furaha unazozifahamu?
  • Tunaweza kuomba kwa ajili ya mtembeo wa uweza wa Roho wa Mungu, lakini kwa nini vizazi vifuatavyo ni vigumu?
  • Tatizo linaendelezwa kwa sababu kulikuwa hakuna namna ya kuunganisha injili kuwafikia watu wa Mungu.

Njia ya Kuelekea Nyumbani

  • Toba ni njia yetu ya kurejea kwa Mungu.
  • “Tubuni basi, mrejee,ili dhambi zenu zifutwe,zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana”(Mdo 3:19)
  • Uamsho huja kwa sababu ya toba ya kweli inapotokea katika mioyo mingi.
“Ikiwa watu wangu,walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya, basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao” (2 Nya 7:14)

Ufumbuzi wa Mungu

  • Kama tukimwijia, naye atatuijia na kutuonyesha namna kanisa linavyoweza kupambana na giza lililomo duniani kupitia nuru.

  • Ikiwa Israeli itarudi na kuilekea madhabahu, Mungu atasikia na kuiponya.
  • Mungu aketiye mbinguni na kuwacheka adui zake(Zab2:4)

Tunachojifunza

  • Mungu hutumia mashambulizi yanayolijia kanisa ili kwamba tuache mitazamo yetu ya zamani na kugundua uweza utukufu wa ukweli wake.
  • Tatizo halisi ambalo linapambana na kanisa ni kutoamini.
  • Badiliko huanza kwa kumrudia Mungu, kunyenyekesha mioyo na kutubu dhambi zetu.
  • Watau wa Mungu ni lazima tuchukue hatua au tupoteze ardhi kinyume na adui zetu.

Tunavyoweza Kutumia

  • Je, umekatishwa tamaa na dhambi ndani na kukuzunguuka, au unaikubali kama vile mambo yatokeavyo?
  • Kama Nehemia, alikuja katika madhabahu ya Mungu siyo tu kwa ajili ya dhambi zenu za moyo na jicho uliopotoka/lililopotoka, lakini vilevile kwa namna ya watu wa Mungu.

Rasilimali

PDF ya Somo la 1  |  Kitabu cha Kiini Cha Maisha  |  Orodha ya masomo