9. Mwanzo wa Maisha na Mafundisho (33-40)

Kiini Cha Maisha: Gundua Siri ya Mafundisho Makuu

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Lengo Kuu · Utendaji wa Ndani · Maendeleo ya Uongozi · Mafunzo Katika Makanisa

Somo la Kiswahili kuhusu lengo kuu la mafunzo, utendaji wa ndani, maendeleo ya uongozi, na mafunzo kanisani.

Rasilimali za Somo

Somo hili lina kitini cha Kiswahili. Hakuna sauti au video iliyoorodheshwa katika maktaba ya sasa.

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 9  |  Kitini kamili cha Kiini Cha Maisha

Mafundisho (33-40)

(33) Lengo Kuu

  • Kusudi la TLC: huimarisha mtiririko wa nguvu za Mungu, ikilinda mabadiliko ya maisha ya watu wa Mungu.
  • Kila shule, kanisa, familia na mahitaji ya mtu kuchunguza hali yake katika mlengo wa malengo ya Mungu na kufanya mabadiliko yanayohitajika.
  • Tusisitize kwa makusudi ya Mungu katika maisha yetu na mafunzo —siyo sheria lakini kusudi la Kristo.
“Wewe, Bwana, nguvu zangu nakupenda sana; Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.” (Zaburi 18:1-2).
  • Tabia za Kiini cha Maisha
Mchoro wa somo la Mwanzo wa Maisha na Mafundisho (33-40)
  • Kusisimuka kwa akili
  • Tathmini ya Urahisi
  • Kuzawadia Kibinafsi
  • Kuwezesha na kuimarisha
  • Mtazamo wa Kimungu na Mwongozo wa kiroho
  • Matunda ambayo yanadumu

(34) Utendaji wa Ndani Kushika haraka neno la uzima: “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitabisha bure. (Fil 2:14-16).

  • Mimea na watu: huachia nafasi ili kwamba mmea uweze kupata mwanga wa kutosha na hewa.

  • Njia mbili za kuunganisha shuleni

(1) Weka mafunzo ya msingi wa maisha kama programu tofauti-ambayo huendelea zaidi ya

agenda ya jumla.

(2) Kuunganisha programu ya mabadiliko ya kiroho katika mpango uliopo.

Changamoto yetu kubwa ni kutathmini wapi mtu anapatikana; kinachofuatia kutafakari wapi aende, na msaada wetu wa tatu kumsaidia kufika kule.

  • Vipi kuhusu wale wapo katika mifumo yetu ambao hawamfahamu Bwana?
  • Ukuaji wa kiroho katika hatua:

(1) Waamini wapya hujifunza kusikiliza sauti za Baba zao na kuwa makini na utendaji wa Roho Mtakatifu kupitia utambuzi na mengineyo.

(2) Waamini vijana hujifunza kupambanua maneno na Roho Mtakatifu sambamba katika kupambanua vilevile maneno ya muovu ambayo husababisha udanganyifu nyuma ya majaribu. Watajifunza namna ya kutii maneno ya Mungu na kuyatumia ili kujilinda wenyewe na kupambana na majaribu.

(3) Waamini wakomavu hutazamia katika nyakati za utajiri wa kuabudu, kufundishwa, kuongozwa, kugawiwa na kulindwa na Mungu, yote ni katika kutumika kuonyesha njia anazotaka Mungu zimzalie matunda kupitia maisha yao.

  • Washauri wazuri hutaka, kutoa maono makubwa ya Mungu.
  • Muundo wa Mungu ni kutengeneza watu ambao hupenda kumsikiliza kwa Mungu, na kujifunza kufanya haya katika kila eneo.
  • Mungu amedhamiria kutengeneza ndoa nzuri ili tuweze kuonyesha namna nidhamu ya kiroho na ukaribu wao na Mungu ili uweze kuwa na ndoa zenye matokeo makubwa kabisa.
  • Tunafundisha, tunashauri, na kuhubiri kutenda sambamba na Mungu na kuwafundisha wengine kufanya hivyo.

(35) Maendeleo Ya uongozi

  • Kufundisha shule ziku zote hukosesha lengo! Kwa nini?
  • Pasipo kujizoweza maisha ya kiroho, mtu hawezi kuwa kiongozi mzuri. “ Pasipo mimi hamwezi kufanya kitu”(Yohana 15:5).
  • Mfalme Daudi alikuwa na wazo kama hilo: “Abarikiwe Bwana Mungu, Mungu wa Israel, atendaye maajabu” (Zaburi 72:18).
  • Viongozi huwa wapo hatarini; kwa kujifanya ibada na nguvu sababu ya kiburi #9 Mwanzo wa Maisha na Mafundisho (33-40) 21

  • Hatua#1: Lengo ni kuendeleza imani katika Mungu ambayo huja kupitia ulinzi uliomo ndani ya upendo wake.
  • Hatua#2: Lengo ni kujifunza kulitumia Neno la Mungu kuyashinda majaribu.
  • Lengo letu: “Na walio na hekima wang’aa kama mwangaza wa anga; na hao wawaongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele(Danilei 12:3).
  • Si viwango tu: Uadilifu tunao uishi, utu wetu katika nuru ya kusudi la Mungu Mtakatifu moja kwa moja huwavutia namna tunavyowavuta na kufundisha watu. (Tito 1:6-9)
  • Na BWANA akamwambia Samweli, “Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

(36) Mafunzo Katika Makanisa

  • Ni muhimu kuwafundisha viongozi katika makanisa yetu
  • Hakuna mafunzo yanayo ongoza uongozi wa uasi
  • Watu hufuata viongozi kwa wema au ubaya
  • Jipatie ramani ya kiroho. Kwanza kutana na makundi baadaye wafuate watu binafsi yaani mmojammoja. (Efe 2:20-22)
  • Simamia muda katika ufuatiliaji
  • Mfano wa wanandoa wanaopelekana mahakani na kuwafuatilia katika hatua mbalimbali
  • Kitu gani hutokea wakati hakuna ukuaji? Namna gani mtu hukabiliana?
  • Inakuwaje kama watu hawahitaji kukua? Hakuna maono? Hakuna uchungaji mpya?

(37) Ushirikiano Katika Shule za Mafunzo

  • Mchungaji mpya na familia, lakini….
  • Ukomavu si kupata shahada!
  • Kuepuka Ukatili
  • Mpango wa umoja unahusisha Kiini cha Maisha
  • Majukumu ya mwalimu
  • Majukumu ya mwanafunzi

Rasilimali

PDF ya Somo la 9  |  Kitabu cha Kiini Cha Maisha  |  Orodha ya masomo