4. Mwanzo wa Maisha na Wewe (9-11)

Kiini Cha Maisha: Gundua Siri ya Mafundisho Makuu

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Kuwa Macho · Kukaribisha · Imani Ikuayo

Somo la Kiswahili kuhusu kuwa macho kiroho, kukaribisha kazi ya Mungu, na imani inayokua.

Sauti na Video

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 4  |  Kitini kamili cha Kiini Cha Maisha

(9) Kuwa Macho

  • Mtazamo wa muelimishaji
  • Kuendeshwa na maisha bila kuwa macho
  • Mabadiliko ya balehe na uelewa wa utambulisho
  • Ujinga husababisha kutokuwa na shukrani
  • Moyo wa kupenda vitu na umri wa kidunia

Tatizo la Kiroho Lililofichika

  • Ujinga wa maisha ya kiroho
  • Maisha ya mwili, Na Ray Stedman yaliwafanya watu wa Mungu kutambua vipawa vya kiroho na Roho wa Mungu
  • Harakati za kikarizimatiki pia zimesaidia kuweka muunganiko lakini pia zimetengeneza upotoshaji
  • Tunavyozidi kujitenga na umakini wa Roho wa Mungu atendaye kazi ndani yetu katika maisha ya Kikristo, ndivyo tunavyozidi kufa kiroho. “Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kufuata mfano tuliowapa ninyi. Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani” (Wafilipi 3:17-19).

Uamsho wa Zamani

  • Uamsho wa zamani ulirejesha umakini mkubwa wa uwepo wa Mungu.
  • Hawakuhukumiwa kwa kazi zao bali kwa Roho wa Mungu aliye ndani yao.
  • Ujinga hutengeneza dini za kibinadamu/dunia ya ubunadamu.

Kutotangulia Kuwafikia Kwa Sasa

  • Wanaume, wanawake na watoto 65,000,000 husikia Injili kwa mara ya kwanza kila mwaka.
  • Watu 178,000 watasikia Habari Njema kwa sasa kwa mara ya kwanza.

  • Miezi 12 iliyopita makanisa 50,000 yalianzishwa.

Kutoamini Mungu Kimatendo

  • Waamini wanaendelea na maisha yao ya Kikristo bila kuwa na ufahamu wa uwepo wa Mungu.
“Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, ni kama wanyama wapoteao”(Zaburi 49:20)
  • Endelea kwenda kanisani, mshukuru, au toa zaka pasipo kumuwazia Mungu.
  • Tunaweza kuwa na matendo yote lakini tusiwe na ufahamu wa ndani wa Mungu unaotembea na kutuhamasisha.

Mpumbavu amesema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, wamefanya machukizo; Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, aone kama yuko mtu mwenye akili, amtafutaye Mungu.Wote wamepotoka; wameoza; wote pamoja, Hakuna atendaye mema. Je, wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, wala hawamwiti Bwana.(Zab 14:1-4).

Kuutafuta Uwepo Wake

  • Uamsho huja wakati tupo tayari kurejesha nafasi sawia ya Mungu katika maisha yetu.
  • Je, ni lengo letu kumjua Mungu au kumjua yeye zaidi?

Tunachojifunza

  • Binadamu, ikihusisha na wanaojiita Wakristo, wanaishi pasipo kujua nguvu ya Mungu aitoayo inayoonekana na isiyoonekana katika maisha
  • Pasipo ufahamu wa kazi ya Mungu katika maisha yetu, mioyo yetu huwa migumu na kiburi hukua.
  • Tunapo manisha katika uwepo wa Mungu katika maisha yetu, tunajinyenyekeza, tukishukuru, tukimuangalia Mungu na kumtegemea yeye tu.

Tunavyoweza Kutumia

  • Chunguza maisha yako kwa ishara ya kumilikiwa kunakotoka kwa Mungu. Je, unaishi maisha yako ya Kikristo au una endesha huduma yako pasipo msaada wa Mungu?
  • Tathmini ufahamu wa wale wakuzunguukao (walio kanisa na wasio kanisa) kwa uwepo wa nguvu wa Mungu.

(10) Kukaribisha

  • Maisha haya(1:4) yamekuja duniani na yametanabaisha Maisha haya na Nuru kama Yesu Kristo katika Yohana 1:14.

“Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa , si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu bali kwa Mungu”( Yohana 1:12-13).
  • Mungu alizalisha Roho Wake ndani yao na akawapatia maisha hayo mapya kuwepo.

Kuwa Mwenyeji mwema

  • Kuna tofauti gani kati ya mwenyeji mwema na mwenyeji mbaya?
  • Mtazamo wa mgeni
Mchoro wa somo la Mwanzo wa Maisha na Wewe (9-11)
  • Katika mahitaji binafsi
  • Katika mipango ya mgeni
  • Katika imani, kuna kuishi.
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao” (Ebr 11:6).

Kutafuta Kwa ajili ya Mungu

  • Pasipo imani, hakuna hakuna maisha ya kiroho. Mungu alisema kwa Mfalme Rehoboamu, “Naye akatenda yaliyo maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake kwa amtafute BWANA”( 2 Nyakati 12:14).

Tunachojifunza

  • Mwamini si kwamba mwanzoni humkaribisha Yesu katika maisha yake katika kuanza( mfano wokovu) lakini maisha yake huendelea kuhitaji kuzamisha umakini wa Yesu Kristo ambaye kwa sasa anaishi ndani yake.
  • Imani huja kutoka katika hali hiyo mpya ambayo Mungu ametupatia. Imani inayokuwa huwakirisha ufahamu wetu wa utambuzi na ukaribisho wa uwepo wa Mungu na kazi yake katika maisha yetu.

Tunavyoweza Kutumia

  • Rejesha mawazo yako pale Mungu alipo fungua moyo wako kwanza ili umfuate. Tazama Yohana 1:12-13 na namna ulivyofungua moyo wako kwake.
  • Fikiria kuhusu wiki iliyo pita. Kwa namna gani, umemtafuta Bwana?

(11) Imani Ikuayo

  • Wakristo wana changamoto kuu mbili kila moja inahitaji kutumia imani:

(1) Kujifunza namna ya kumrudia Bwana wakati ameanguka.

(2) Mwendelezo wa kumtafuta Bwana hata wakati mambo yote yapo safi.

Kumrudia Bwana

  • Kusahaulika
“Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliacha torati ya Bwana na Israeli wote pamoja naye” (2 Nyak 12:1).
  • Rehoboamu alipata matatizo katika mwaka wake wa tano wa kutawala kwa sababu ya kutokuwa mwaminifu kwa Bwana. “Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi Bwana”( (2 Nyak 12:2).
  • Mambo yalikuja kuwa mazuri pale yeye na Israeli walipo jinyenyekesha na kurejea.
“Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya BWANA ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekana katika Yuda mambo mema”(2 Nyak 12:12).

Imani na Mambo Yake

  • Hii inaelezea kwa nini tunaweza kuanguka wakati kila jambo linaonekana kwenda vizuri au wakati tulipokuwa chini, tukiwa katika kukata tamaa tunaweza kumwita Mungu kwa ajili ya msaada maalumu na kuutafuta msaada huo. Nguvu yetu inategemea imani tuliyonayo.
  • Mabadiliko haya na fursa hutokea kwa siri katika mioyo yetu na akili yetu.

Tunachojifunza

  • Ukuaji wa kiroho huchipua kutokea katika kutendea kazi imani yetu au kumtegemea Mungu.
  • Kushindwa kiroho hutokana na kutoamini njia za Mungu kuwa ni bora na muhimu.

Tunavyoweza Kutumia

  • Elezea imani yako kwa Mungu. Unapofanya, weka kiwango namna unavyofikiri Mungu ni muhimu katika maisha yako kuanzia 0 hadi 10.
  • Fikiri wakati unaporudi nyuma. Elezea wasiwasi wako kwa huo. Je, ulikuwa na wasiwasi katika mambo baadhi ya Mungu au njia zake?

Rasilimali

PDF ya Somo la 4  |  Kitabu cha Kiini Cha Maisha  |  Orodha ya masomo