10. Kukua kwa Ndoa Zinazokua (Efe 5:31-33)

Kiini Cha Maisha: Gundua Siri ya Mafundisho Makuu

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Ndoa na Ukuaji wa Kiroho · Picha ya Ndoa ya Kibiblia · Umoja Katika Ndoa

Somo la Kiswahili kuhusu ukuaji wa ndoa kwa mwanga wa Waefeso 5:31-33 na maendeleo ya kiroho.

Sauti na Video

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 10  |  Kitini kamili cha Kiini Cha Maisha

(Efe 5:31-33)

  • Ndoa zinazokua huonyesha namna gani ndoa zikue katika utimilifu wa Kristo na kanisa tunapolichunguza katika ukuaji tofauti hiyo inawezekana katika kila hatua kati ya hatua zote tatu za ukuaji wa ukristo. Ndoa ya kuogofya inatukumbusha kwamba tuna safari ndefu kuyafikia maisha yetu ya kiroho.
Mchoro wa somo la Kukua kwa Ndoa Zinazokua (Efe 5:31-33)
  • Ndoa hutufunga kiagano hadi pale kifo kinapotutenganisha na hivyo basi hii inatuwezesha kujiweka vizuri sisi pamoja mahusiano yetu na wenzi wetu. Tunapokuwa katika ufahamu wetu wa Mungu katika kujitoa kubariki ndoa yetu, na tuzama kwa wenzi wetu na kumpenda yeye kama Mungu anavyotupenda.

Picha Ndoa ya Kibiblia (Efe 5:31-33)

“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.” (Waefeso 5:31-33).
Mchoro wa somo la Kukua kwa Ndoa Zinazokua (Efe 5:31-33)
  • 31: Ndoa ni mwongozo: Maelezo ya Mungu katika maana ya ndoa.
  • 32: Ndoa ni muundo: Kama muundo unaoakisi baada ya mtiririko kati ya Mungu na watu wake.
  • 33: Marriage inawezekana
  • Muundo wa Mungu na muonekano wa ndoa huongoza katika kuelekea uzuri wa ukaribu. Wawili huwa mwili mmoja, kimwili, ndiyo, lakini katika nafsi moja na kusudi. ‘Umoja’ huu huwa kishitaki kinachowezesha kufanya kazi kupitia mchakato wa ndoa. Uzuri na furaha ya ndoa hupendeza kama huu ‘mwili mmoja unatendewa kazi nje ya wawili.

Masusmbufu ya Ndoa- Mchoro

  • Mchakato wa kupika
  • Ulazima wa joto
  • Ukaribu hutengeneza msuguano huo/joto/ masumbufu
  • Muunganiko ni mwema; wawili kuwa mmoja

Mchakato wa ukuaji huu wa ndoa umefungwa katika maendeleo yetu binafsi ya kiroho. Tunaweza iangalia vibaya (kupoteza) au kiuchanya (kuongeza na kurekebisha). Ndoa, baadaye, ni kurekebisha uzoefu hutoa thawabu kubwa. Tunapokuwa na ufahamu wa kupoteza, kama vile katika mahusiano ya ufuasi halisi( mfano, kufa wenyewe), na baadye tunaweza kufanya kazi pamoja pasipo kulalamikia wenzi wetu au Mungu au wengine kwa usumbufu. Badala yake, huangalia mbele kwa ujasiri katika muundo wa ‘umoja’ kwa mahusiano yetu. Hebu tufuate ndoa katika madaraja matatu.

Ngazi 1-Kujitoa na Uwazi

Maono: Nataka kuwa naye!

  • Fikiri kuhusiana na gharama za kifedha, migandamizo, mabadiliko ya majukumu, umbali wa makazi unaotokea pale wapenzi wameoana, na bado wanahitaji kuoana!

Wapendanao Hubadili Maono

  • Kujitoa
  • Watakao
  • Kujitoa mara nyingi kwa kiasi kikubwa hujengwa kutokana na matarajio ya mtu

Changamoto za Wapendanao

  • Kutokuwa imara na upendo huwa usio imara
  • Matumaini hupotea
  • Matumaini kurejeshwa (kujengwa)

Majibu ya Wapendanao

  • Kukata tamaa( mara nyingi huwa kwa muda tu) kwa mpendwa mmoja wapo- kimuhemuko na kimwili.
  • Kukubali matarajio ya chini kwa muda( kuishi kwa hisia badala ya ukweli- na umoja)
  • Kuacha baadhi ya tabia na kukubali kiasi cha chini kuliko maneno na vitendo vinavyo kubalika.

Hitimisho Hatua ya mwanzo ya ndoa mara nyingi huwaonyesha upendo wa ‘kimakosa’. Japokuwa upendo huu usio wa haki ni wa kujitoa kiasili, kujitoa hutumika kwa matarajio ya mtu na kutimiza ndoto. Wakati yanapoacha kufikiwa, mambo makubwa ya kupanda na kushuka hutokea.

Ngazi 2-Ndoa Iliyo Na Changamoto

  • Maono: Fuata malengo ya Mungu ya ndoa bila kujali vikwazo.

  • Matumaini ya ndoa hutolewa na kujitoa kwa kumanisha katika matumaini ya Mungu ambaye hutoa mmoja katika Neno.
  • Kukata tamaa kunatoka kwa kurekebisha kutoka kwa umoja uliopatikana na kurudi nyuma katika kuzingatia matakwa na matamanio ya mtu mwenyewe.

Vijana Waliooana Hubadili Maono

  • Upendo: Napenda kuoa/kuolewa, lakini……
  • Hasira Iliyopotea: Mimi hukasirika sana sababu ya mke wangu.
  • Maono Yaliyopotea: Je, ni hii yote kuna ndoa?

Tabia za Wanandoa Wachanga

  • Kuchanganyikiwa: Nina nia ya kuweka matarajio yangu mbele ya uhusiano wetu.
  • Ujanja: Sipendi upendo wa kweli kupata nianachohitaji
  • Uovu: Burudisha mawazo ya mahusiano kuwa bora.

Changamoto za Wanandoa Wachanga

  • Mahitaji kuruhusu Neno la Mungu kumleta mmoja kwake Mungu ili kutunza maono hayo na kujitoa.
  • Maombi mengi hufanya kazi kupitia magumu na yasiyopitika katika mahusiano ya ndoa.
  • Kwa muendelezo sameheaneni na mtumainieni Mungu kuwapatia mahitaji yenu ya muhimu zaidi.

Hitimisho

Neno la Mungu hutoa tumaini na mwelekeo kwa wanandoa waliochanganyikiwa kwa siku za hatima yao ya pamoja. Ndoa hufanya kazi pale Mungu anaporuhusiwa kutenda kazi na kuijenga katika nyakati za kutokuelewana. Ndoa changa mara nyingi huishi maisha ya kidunia kwa upendo wa ‘phileo’ , “ Jinsi unavyonitendea ndivyo nami ntakutendea” Hizi ni nyakati mbaya za maeneo zinazo zingatiwa na upendo wa 'agape' huanza kuangaza.

Ngazi 3- Majibu Mazuri Kutoka Kwa Upendo wa Mungu

  • Maono: Kujitolea kwa bidii kwa mke wa mtu
  • Upendo wa Kristo ni upendo uliokomaa, zaidi husafisha mienendo yetu, maneno, na mguso hutuwezesha kuwapenda wale walio tofauti nasi au vinginevyo tungesababisha kutokuwa na ulinzi katika ndoa zetu.

Muendelezo wa Ndoa Ya Watu Waliokomaa

  • Nimejidhabihu kwa ajili yake.
  • Wakati mwingine, nakuwa nimesongwa nikimsaidia mpenzi wangu, najisahau mwenyewe.
  • Wakati nimekosewa, kwa haraka husamehe
  • Jawabu si kupata nivyotaka, lakini ni kuona ambacho Mungu ananifundisha kupitia mpenzi wangu
  • Ninajaribu kugundua mahitaji ya mwenzi wangu ili niweze kumpendeza.

Tabia za Ndoa Ya Watu Waliokomaa

  • Mahusiano na Mungu huwa imara ili kwamba mahusiano ya mwenzi fulani yawe imara hata wakati kuna kutoelewana, kuvunjika moyo au kuwa na matarajio tofauti.
  • Kuongezeka kwa nyakati za ukaribu kwa mwenzi huwa hakuko katika uzuri bali katika kujitoa, si kujitoa kwa ukaribu wa mwili pekee lakini katika moyo mmoja.
  • Mmoja wao huzama katika mahusiano na Mungu kuuelekea ufahamu wa upendo wa Mungu, kumwezesha mmoja kusafisha upendo wake kwa mpenzi wake kama anavyoongozwa na Roho.
  • Kujitolea kuwa na maudhui thabiti na mwenzi wako mwenyewe.

Hitimisho

Kutajirisha upendo wa ‘agape’ humwezesha mwamini mkomavu kuepuka ulevi wa uchoyo na kuhitaji, na badala yake inalenga kumjenga mwenzi wa mtu kwa njia ya matendo na maneno thabiti na ya fadhili, kufurahia umoja wa moyo na akili ili kuleta amani, furaha na upendo.

Tunavyoweza Kutumia

  • Fikiri ndoa iliyo na usumbufu na uonyeshe namna matatizo binafsi/ kiroho yanavyoweza kuathiri ndoa yao.
  • Umewahi kuona ndoa nzuri? Je, umeshuhudia tabia zipi kwa ndoa hizi nzuri?
  • Ainisha sifa binafsi moja au zaidi katika maisha yako ambayo inahitaji kushughulikiwa ili kuwa na ndoa yenye ukaribu.

Rasilimali

PDF ya Somo la 10  |  Kitabu cha Kiini Cha Maisha  |  Orodha ya masomo