7. Mwanzo wa Maisha na Wewe (17-18)
Kiini Cha Maisha: Gundua Siri ya Mafundisho Makuu
Hatua ya Kukomaa #3 · Mzunguuko wa Maisha
Somo la Kiswahili kuhusu hatua ya ukomavu na mzunguko wa maisha ya kiroho.
Sauti na Video
Kitini cha Somo
(17) Hatua ya Kukomaa #3
- Kijana anaweza kuchanganyikiwa wakati inapoanza na inapoishia lakini si kwa baba.
- Baba huanza wakati anapokuwa na mtoto.
- Tendo la uumbaji na kulea mtoto.
Malengo 3 ya Mungu Kwetu
“Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimili wa Kristo”(Ef 4:13).
(1) Mungu anahitaji sote twende mbele katika hatua hii ya tau na hatua ya mwisho ya maendeleo ya kiroho.
(2) Mungu anahitaji kila mmoja wetu aongoze wengine katika maisha mapya ya kiroho.
(3) Bwana anatamani kwamba tuwajibike katika kujali wote wanaopata maisha ya kiroho wanotunzunguuka.

- Alama ya Yesu Kristo inapaswa kuonekana katika maisha yetu. Kufikiria Kuhusu Wengine.
- Kamwe usisahau kushirikisha maisha yaletayo Injili na wengine.
- Wajibu wetu kujali wote tunao waleta katika familia ya Mungu.
- Uongozi una zaidi katika kuwasaidia wengine kukua zaidi ya nafasi ya uongozi unayoshika.
- Hakikisha kila mmoja analelewa katika mtazamo wa kiroho.
Tunachojifunza
- “Mababa” ni waamini waliokomaa ambao wamepiga hatua zaidi ya kupambana kwa waamini vijana na wapo tayari kuwatunza wengine bila kuteteleka.
- Watu wa Mungu wanaweza na watakua na kufikia ukomavu halisi ndani ya Kristo.
- Tunawajibika Kurithisha ukweli wa maisha kwenda kwa wengine na kutunza maendeleo yao ya kiroho.
Tunavyoweza Kutumia
- Je, Umewatunza waamini vijana katika Kristo?
Liliendaje? Namna gani lingefana?
- Je, kuna yeyote ambaye unamtunza?
(18) Mzunguuko wa Maisha
- Mzunguuko halisia wa maisha tangu kuzaliwa-kukua-kukomaa-kuzalisha-kujali-kuzeeka- kutokuwepo ni ukiroho wa kweli pia.
- Kazi yetu nikuwafanya wengine wafanikiwe zaidi katika ukuaji zaidi yetu wenyewe.
Kushikilia Kizima
- Tatizo Kubwa: Waamini mara chache wana malengo ya kiroho.
- Maamuzi-Sisi huamshwa kirahisi kwa umuhimu wa hali yetu ya uwepo wa maisha.
- Usahihi- Tunapata usahihi wa picha ambayo tayari tunayo au tusiyonayo tumeiona katika maisha yetu.
- Shabaha- Tunachangamsha msimamo katika kufikia ukomavu na kukamilisha mpango fulani kwa maisha yetu.
Mioyo Miwili Inalia
(1) Kitabu cha Joshua kinaita moyo wangu kutumaini kwa Mungu mkuu kupitia maisha yetu.
Yote yanawezekana.
(2) Kitabu cha Waamuzi hunyenyekeza moyo wangu. Ninaumia kwa namna nilivyopuuzia
majukumu ya maisha yangu.
- Uwezo kamili wa ushindi hukaa karibu kuelekea ubaya wa aibu ya kushindwa.
Baadhi ya fursa za maisha. Zako ni zipi?
- Je, unaishi na mwenza wa kutisha?
- Je, kiongozi wako hafahamu uwezo wako?
- Je, kuna mtu yeyote ‘aliyekuibia’ msichana wako?
- Je, unapata hofu ya kuzeeka?
Ramani Yako ya Ukuaji wa Kiroho

- Inafafanua ulipo katika ramini yako ya kiroho
- Weka kumbukumbu mahali unapotakiwa kuwa.
- Mtafute Bwana ili akufikishe mahali unapaswa kuwa.
- Tafuta kuzaa maongezeko ya matunda
Tunachojifunza
- Ukomo wetu wa muda unatufanya tuwe na uhitaji wa kupambanua mahali tulipo katika ramani ya ukuaji wa kiroho na hii inatusukuma tusonge mbele.
- Mungu kimkakati anahitaji kutenda kupitia maisha yetu lakini kuongezeka katika ukuaji na ukomavu wa kiroho ni mambo ya muhimu yanayohitajika.
- Tunapokusudia kukua, mara ukuaji huwa rahisi na unanavutia.
Tunavyoweza Kutumia
- Onyesha wapi umefikia katika ramani ya ukuaji wa maisha ya kiroho. Kwa nini umejikadiria hapo?
- Je, unahisi uhitaji wa ukuaji wa kiroho? Mwambie Bwana kuhusiana na jambo hili kisha muombe akuonyeshe vipau mbele vyako katika maisha katika eneo hili.
Rasilimali
PDF ya Somo la 7 | Kitabu cha Kiini Cha Maisha | Orodha ya masomo