2. Chanzo cha Maisha (4-6)

Kiini Cha Maisha: Gundua Siri ya Mafundisho Makuu

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Maisha ni Udhihirisho wa Utukufu · Msukumo wa Maisha · Ishara za Maisha Mapya

Somo la Kiswahili kuhusu maisha kama udhihirisho wa utukufu, msukumo wa maisha, na ishara za maisha mapya katika Kristo.

Sauti na Video

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 2  |  Kitini kamili cha Kiini Cha Maisha

(4) Maisha ni Udhihirisho wa Utukufu

  • Maisha ni siri ya ajabu inayoshikilia siri kuu za dunia.
  • Sote tunafahamu uhalisi wa maisha ulivyo, japo tunaweza kuelezea maisha haya kwa kuchunguza.
  • Maisha yanatembea, yanapumua, yanajizalisha, yanakua, hulika,

Wakristo huongelea sana kuhusiana na maisha ya kiroho lakini bado hawawezi kuyaelezea maisha hayo kiuhalisia.

Mfanano wa Maisha

  • Wandishi wa maandiko pamoja na John kwa namna fulani walishangazwa kwa alama kama nuru, upendo, na maisha.
  • “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu” (Yoh 1:4)
  • Maoni ya maisha ya msingi ni muhimu katika kuelewa ufuasi mzuri.
  • Maisha mapya huelezea mwanzo wa maisha ya kiroho.

Maisha ni sura ambayo ukweli mwingine unaweza kuning’inia humo.

Kufichika Katika Nuru

  • Ukweli mwingi umefichwa katika maisha yetu katika vitabu vya teolojia.
  • Lakini alitumia mifano
  • Ukweli wenye thamani umefichwa, mbali kuufikia.
  • Harakati za Keswick
  • Miujiza huleta imani lakini si kwa ukuaji makubwa

Nidhamu ya Kiroho

  • Ni rahisi kupima nidhamu inayofanyika lakini hii si sawa na kuhuishwa.
  • Ulisha wahi kuomba au kusoma Biblia bila kukuhuishwa?
  • Kwa wengi ni kama kuendesha bila kuwa na mahali pa kufika
  • “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” (Yoh 10:10)

“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu msalabani, ili tusife dhambini bali tuishi katika haki; kwa maana kwa kupigwa kwake tulipona” (1 Petro 2:24).

Tunachojifunza

  • Mungu anahitaji tufahamu kweli hizi na kuzijenga katika uumbaji wake.
  • Yesu na wandishi wa maandiko walitumia maneno ya mfanano ikihusisha neno ‘maisha’ kutusaidia kuyakamata na kuelewa kweli za muhimu.
  • Kanisa kwa ujumla halijachukulia wazo la maisha na kusudi lake.
  • Taasisi za elimu za Kikiristo zimeficha kweli za muhimu kwa wanafunzi wao, zikipoozesha si maisha yao tu bali na kanisa kwa ujumla.

Tunavyoweza Kutumia

  • Fanya kwa uzuri kuelezea maisha ya kiroho na namna mtu akuavyo kiroho.
  • Lengo kuu la Ukristo ni nini? Uwe kimahususi iwezekanavyo.

(5) Msukumo wa Maisha

  • Rahisi ni njema zaidi!
  • Kweli za muhimu za maisha kupitia kanuni ambazo zinaonekana kirahisi katika uumbaji.
  • Uumbaji, kwa mfano, hutoa picha inayoonekana ya ukuaji wa kiroho.
  • Kua, kua, kua!

Ukuaji wa kawaida huja katika asili, hii ni kwamba, hutokea pasipo kupangilia kwetu.

Uwepo wa Maisha

  • Roho wa Mungu ameunganishwa na sura hizi za maisha kwa sababu Roho ni Uhai.
  • “Roho hutoa uhai”
  • Mara tu Roho Mtakatifu anapokuja kuishi ndani ya mwamini, huelekezwa katika njia ya maendeleo na muonekano.
  • Kusudi la Mungu kutukuza kwa hiyo tunaweza kutafuta namna tofauti itakayokamilisha lengo lake ndani yetu. Imani huondoa wasiwasi.
“Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu”(Wafilipi 1:6). • Uwezo wa mbegu

Zoezi

  • Chora nukta kisha andika tarehe na muda, kwa mkusanyiko mzuri, wakati ulipo aminiwakati maisha yako ya kiroho yalipoanza ndani yako. Tengeneza kiduara cha kuchorea mstari wa mshare kuelekea kulia.
  • Mshare huu unamwakilisha kimahususi ukuaji wa Kimungu ambao anaopanga kuingiza katika maisha yako.

Tunachojifunza

  • Waamini hawahitaji ‘kujitengeneza’ wenyewe katika ukuaji kana kwamba ukuaji si asilia au si kawaida.
  • Hakuna kiwango tofauti au ubora tofauti wa maisha ya Kimungu; Mungu anaishi kwa usawa kwa kila mwamini.
  • Kuhuishwa huanza pale mioyo yetu inapoonyesha kukubali wa tamanio la Mungu kuishi, kukua na kufanya kazi ndani yetu na katika maisha yetu pia kimwili na kiroho.

Tunavyoweza Kutumia

  • Una uhakika umezaliwa mara ya pili?
  • Soma Waefeso 1:13-14. Tazama jinsi Roho Mtakatifu anakaa ndani ya mwamini wa kweli. Kisha mshukuru Bwana kwa kazi yake ndani yako.

(6) Ishara za Maisha Mapya

  • Maisha ya kiroho, baadaye, zaidi kama maisha ya kimwili yenye udogo lakini yenye nguvu yenye uweza iliyomo ndani ya kila mwamini wa Kikristo.
Mchoro wa somo la Chanzo cha Maisha (4-6)
  • Hakikisha una uzima wa kiroho.
  • Mapema, chunguza rangi ya utoto, upumuaji, mapigo ya moyo, muitiko wa mwili na mlio wa mishipa.
  • Mabadiliko ya kiroho vilevile hutokea.
  • Bayogenesisi( kanuni ya kisayansi inayosema: uzima hutoka katika uzima)

Upepo & Uzima

“Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” (Yoh 3:8)

Maji & Uzima

“Walakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemichemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.” (Yoh 4:14).
  • Nguvu ya uhai ina mwelekeo mmoja kuliko kutawanyika, na kwa hiyo imeambatana na uhai wa kiroho–umezunguuka and huru, bado ni ya kusudi.

Udhihirisho wa Kazi za Roho Mtakatifu

“Aliyezaliwa kwa Roho”(Yohana 3:8)

  • “Shauku ya Neno la Mungu”
  • Shauku ya kujumuika pamoja na Waamini wa Kikristo.
  • Shauku ya kuongea na Mungu(Maombi)
  • Kuwa makini na wenye dhambi
  • Hitaji la msamaha kupitia Kristo Yesu.
  • Upendo unaokua wa kumpenda Mungu na njia zake.
  • Kuwajali wenginne na kujali mahitaji yao.

Tunachojifunza

  • Upepo na mito inatufundisha kuhusiana na uwepo, kusudi na uweza wa Roho Mtakatifu.
Mchoro wa somo la Chanzo cha Maisha (4-6)
  • Maisha mapya huja kutoka katika uwepo wa Roho katika nafsi zetu.
  • Maisha ya kiroho, kama maisha ya kimwili, hufunua uhalisi wake kupitia ishara zinazotarajiwa.
  • Ishara hizi za maisha ya kiroho zitakuwepo tu ndani ya mwamini halisia, japokuwa ishara hizo zinaweza kuhifadhiwa au kuharibiwa kwa kuendelea katika dhambi.

Tunavyoweza Kutumia

  • Hebu fikiri ulipomfahamu Yesu kwa mara ya kwanza. Pitia ishara za maisha zilizoanishwa juu. Je, unaweza kuziona katika maisha yako mwenyewe?

Rasilimali

PDF ya Somo la 2  |  Kitabu cha Kiini Cha Maisha  |  Orodha ya masomo