5. Mwanzo wa Maisha na Wewe (12-14)

Kiini Cha Maisha: Gundua Siri ya Mafundisho Makuu

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Malengo ya Maisha · Kuutafuta Mwongozo · Udadisi

Somo la Kiswahili kuhusu malengo ya maisha ya kiroho, kutafuta mwongozo wa Roho, na udadisi unaosaidia ukuaji.

Rasilimali za Somo

Somo hili lina kitini cha Kiswahili. Hakuna sauti au video iliyoorodheshwa katika maktaba ya sasa.

Kitini cha Somo

Pakua PDF ya Somo la 5  |  Kitini kamili cha Kiini Cha Maisha

(12) Malengo ya Maisha

  • Kila nguvu ina mwelekeo na jitihada.
  • Japo maisha yetu ya kiroho kwa kiasi kikubwa hufanya kazi kupitia utendaji wetu ukihusisha akili, jambo hilo lina nguvu yake pamoja ikiambatana na kusudi lake.
  • Kama tunaweza kupambanua kusudi la Mungu ndani yetu na kushirikiana na Roho Mtakatifu, hivyo basi tutasonga mbele katika nguvu.
  • Je, ulishawahi kuhisi ushindi wa nguvu kipindi cha nyuma?

Kutanua Maarifa Yetu

  • Mahangaiko mengi ya kiroho yatapotea kama tutakuwa na maarifa sahihi.
  • Waamini wengi ni wajinga kwa malengo ambayo Mungu anayo kwa ajili yao.
  • Kama upepo, Roho wa Mungu hatuwezi kumuona kwa macho yetu ya mwilini. Roho Mtakatifu bado ananipeleka katika Maendeleo kamili ya Kiroho.
  • Lakini tunapotambua kazi ya Roho, mtazamo wetu hubadilika!
“Elisha akaomba akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”( 2 Fal 6:17).

Upepo Unavuma

  • Hatuwezi kumuona Roho lakini tunaweza kutambua makusudi Niko wapi? yake. Ni hatua zipi zinanifanya nikue? Naweza kukuwaje Zaidi?
“Ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo” (Wakolosai 1:28)
  • ‘Mtimilifu katika Kristo’ na ‘mtakatifu’ hayo ni malengo makubwa kwa ajili yetu.
“Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala hautambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu( Yoh 14: 16-17)”.
  • Mungu yu hai ndani yetu kutuwezesha katika umakini wetu wa kiroho.

  • Kuwa na ushirika nasi
  • Kukamilisha kusudi la utukufu wake kupitia sisi

Tunachojifunza

‘Nguvu ya maisha ya kiroho’ ni kiwakilishi cha ‘nguvu ya kimwili’ inayotembea katika mwili wa binadamu.

  • Nguvu ya maisha ya kiroho inapokuwa kazini katika maisha yetu ni sawa na Kristo kufanya kazi ndani yetu kupitia Roho Mtakatifu.
  • Kiakili unapojiunga katika mapenzi yetu na Mungu hufanya maisha ya kiroho kuwa mepesi zaidi na yenye msimamo.

Tunavyoweza Kutumia

  • Uliwahi kufikiri kuhusu Mungu ukitumia Roho wake Mtakatifu ndani yako ili kutimiza kusudi lake?
  • Ni kutoka katika Wakolosai 1:28 na 1 Petro 1:15-16, utasemaje Mungu anajaribu kufanya kupitia msukumo wa maisha ya kiroho ndani yako? Umeenda nayo kwa muda gani?

(13) Kuutafuta Mwongozo

  • Mungu kwa bidii anaishi ndani yetu kutusaidia kuwa kama Kristi.
  • ( (Muovu anafanya kazi maradufu kutuchanganya.)
  • Lakini waamini wanaishia kuchanganyikiwa kwa namna iliyo nzuri ya kusimamia mahusiano.
  • Tumwonapo mtoto mdogo, huwa hatuweki kwao matarajio yafananayo na mtu mzima.

Picha Ya Kimwili

  • Yohana alitumia maisha ya kimwili kama picha kutusaidia kuelewa uwepo na maana ya maisha ya kiroho.
  • Picha hii inayotusaidia inafafanua maendeleo yetu ya maisha ya kiroho.
  • Inasaidia sana kufikiria umwili kuelewa ukiroho.
  • Maeneo matatu ya maisha ya kiroho, kilichofichika kinakuwa bayana.

Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangua mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu.


Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, mmemshinda yule mwovu( 1 Yoh 2:12-14).

  • Una uhakika hawaelezei makundi yalipo kimwili?

Hatua Tatu

  • Lengo la mchakato mzima ni kuwa kama Yesu- mkristo
Mchoro wa somo la Mwanzo wa Maisha na Wewe (12-14)

aliye komaa.

  • Kila hatua inafafanua kinachotokea kwa kila hatua ya maendeleo.
  • Kama waamini wa muda tunaweza kuhamasisha mwendelezo unaoendelea(mfano wazazi)
  • Tatizo la kanisa dhaifu ni kutowafundisha watoto wetu wa kiroho!

Tunachojifunza

  • Maendeleo ya kiroho ya waamini yana mfanano katika maendeleo ya binadamu.
  • Udhaifu ndani ya kanisa hauna uhusiano katika kukosekana kwa nguvu ya injili au Neno la Mungu, lakini ni kushindwa kwa watumishi wa Mungu kiuwajibikaji kufundisha wale wananowazunguka.
  • Kuna hatua tatu za maendeleo ya kiroho: waamini wapya (watoto), vijana waamini (wakiume) na waamini waliokomaa (mababa).

Tunavyoweza Kutumia

  • Jisomee 1 Yoh 2:12-14. Umeyaonaje makundi haya matatu? Onyesha tofauti moja kwa kila hatua, ya kimwili na ya kiroho.
  • Je unamfahamu mtu yeyote aliye mfuasi? Kama haumfahamu, kwa nini unafikiri imekuwa hivi?

(14) Udadisi

Mchoro wa somo la Mwanzo wa Maisha na Wewe (12-14)
  • Mara tu waamini wasikiapo hatua hizi tatu, na kutambua hakuna hatua ya nne, huanza kushangaa kundi linalowahusu.
  • Ni kama picha ya kikundi! Je, nami nimo humo? Je, ninafanana na nani?
  • Picha ya familia kwa utayari huwasilisha kwa waamini kila mahali!

  • Makundi yapo kwa ajili ya kututia changamoto kuliko kuwa na ukamilifu!

Maono Safi ya Ukuaji

  • Badala ya kuona ukuaji wa afya, waamini wengi wameangukia katika udumavu wa kiroho
  • Wana ugomvi katika eneo moja au zaidi katika maisha yao na wamepoteza tumaini
  • “Ukuaji wa haraka” wa Kimwili na kiroho.

Tumaini Linalokua

  • “Unamanisha uanhitaji niwe kama Yesu?” (‘Baba’)
  • “Ni hatua ipi niifuate?”
  • Maisha hukua kiupekee.
  • Lakini tunaweza kuijenga.
“Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze, Zinifanikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako. Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yanguna shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.” (Zaburi 43:3-4).

Tunachojifunza

  • Udumavu wa ukuaji hutokea kwa upungufu matamanio ya kukua, au kuamini kwamba ukuaji si wa lazima au si wa muhimu.
  • Kama waamini wakiona ukuaji wa kiroho kama uhalisi unaowezekana, kupenda kwao kukua kutawaka.

Tunavyoweza Kutumia

  • Jinsi gani watu wanaokuzunguka wapo tayari kujifunza neno la Mungu? Tathmini tabia za wale wanaohudhuria mikutano ya kujifunza, kuomba na kuabudu.
  • Namna gani upo tayari katika kujifunza na kukua? Katika maeneo gani utajengeka na kuwa hodari?

Rasilimali

PDF ya Somo la 5  |  Kitabu cha Kiini Cha Maisha  |  Orodha ya masomo