
#1 Hadithi Iliyofaulu
Mwanzo wa Maisha
Muhtasari: Kifungu #1, Hadithi Iliyofaulu, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Wingu jeusi la kutofaulu limefunika kanisa la Kikristo. Ni baya kiasi kuwa na tamaduni zinazodunisha uhuru wa mkristo katika kujieleza katika maisha haya na kuabudu, lakini kujitolea kuishi kwa maadili yanayozidi kupotea. Wachungaji na wakristo wote wafalakiana, haya yakichangiwa na picha za ngono kamari na anasa za dunia.
Ubaya zaidi, msingi ya familia inapasuka. Upendo wa watoto wetu kwa Bwana unadidimia. Kuna kitu kibaya mno katika kanisa wakati takwimu inaonyesha ya kwamba wengi wa vijana wetu ambao walilelewa makanisani wanamwacha Bwana na kanisa.
Hatari inatuotea sisi sote. Ninashuku kwamba mengi yanastahili kusemwa kwani uovu kanisani ni dhahiri mno. Roho ya kushindwa inaenea katika nchi nzima. Inapotujia, tunahisi kukata tamaa. Wakati mwingine tunaanza hata kushuku iwapo maadili tuliyoyashikilia ni ya kweli na mema.
Tunapaswa Kufanya Nini?
Njia mmojawapo bora ya kupigana na jaribio hili ovu la kushindwa ni kurejelea misingi ya neno. “Basi tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” (Warumi 8:31). Mungu kwa kweli yuko upande wetu.
Agano la kale mna hadithi nyingi zilizofaulu. Sio kama hadithi za kawaida za kufaulu zinaonyesha uerevu wa mwanadamu. Badala yake zinaonyesha taswira ya mtu katika wakati wa kulemewa na kukumbwa akikabiliana na kushindwa kukuu. Ni hadi wakati huu ambapo Biblia huonyesha jinsi Mungu huingilia kati na kwa njia ya ajabu huwaokoa wale waliitao jina lake. kuuona wokovu wake. Twaweza kuwa hatujui yote Mungu ayafanyayo, lakini twajua vile ataka kutenda nasi kwa wakati huu. Bwana anataka kututia nguvu tukamilishe ile kazi ametupa.
Mara tukumbapo uweza wa uhai wetu, zaidi twazihisi nguvu za Mungu ndani yetu. Hatuhitaji kwenda kutafuta rasilimali zingine huko nje ili kufaulu. Anataka awe ndiye tunayemtegemea. Neno la Mungu linatukumbusha kwamba yeye yuko upande wetu. Itakuwa ni msukumo mwema kwa maisha yetu ya kiroho kama tungejua na kuamini kwamba hilo pekee ndilo linalohitajika. Mungu alituumba ili tupate kufaulu, “na mkisha kuyatimiza yote kusimama” Waefeso 6:13. Watu wa Mungu wanaweza kusimama imara kwa sababu Mungu hatishwi ni adui. Nasi pia hatuhitaji kuwa na wasiwasi.
Hatari Yetu Kuu
Mungu, kama mto mkuu, kila wakati hutuvuta kutelemkia ukuaji mkubwa.
Shida yetu kuu ni kwamba tunaruhusu chelezo yetu kushika ukingo mwa mto na kutoka nje. Wakristo lazima wasimame wima na kujishughulisha. Twapigana kwa kila wakati kufahamu ukweli wa Mungu ili akaweze kutuongoza vyema katika machafuko ya maisha hata wakati majaribu yanapotujia na mawazo ya kishetani.
Hamna nguvu au uweza ulio na nguvu kuliko Mungu ambazo zaweza kushinda kusudi lake nzuri. Iwapo tuko naye – au tuseme vyema – iwapo yeye yuko pamoja nasi, basi tunaweza yatimiza yote yale Bwana amekusudia katika kupitia maisha yetu. Tunaweza fanya maamuzi ya kumtumainia hata katika mapambano mabaya kwa kutuhakikishia kwamba yale asemayo ni ya kweli na kisha kumwamini.
Na jinsi tuendeleavyo kufahamu matendo ya Mungu yaliyo na nguvu, yafaayo kila mara katika maisha yetu, tutakuwa katika kumtumaini yeye na tutatambua jinsi amani yake ya ajabu huiweka mioyo yetu nyakati
Somo
- Vita vimeshindwa. Mungu alishinda. Twahitaji kila mara kukumbuka
kwamba nguvu za Mungu na kuiweka tumaini letu kwake.
- Mungu anapendezwa kututia nguvu – kama Yusufu, Daudi, Danieli,
Yesu – ili tuweze, kama hao, kuwa karibu na Mungu ili kwamba aweze kutimiza mapenzi yake kupitia kwa maisha yetu.
Kariri Na Tafakari
- Warumi 8:31
- Waefeso 6:13
Zoezi
- Je, umejeruhiwa kiroho? Ni katika nyanja zipi unahisi kushindwa? Nukulu ambazo zaja katika mawazo yako.
- Iwapo umetoka nje ya chelezo cha imani yako ya Kikristo, mwambie Bwana kwa kukiri hofu zako, ukidai msamaha, rudi ndani na endelea na safari.
- Omba kwa sauti sasa hivi (au uandike) kwamba haijalishi chochote, utabaki vitani – hata vita vikizidi kuwa vikali. Mshukuru kwa kuwa mshindi na kupendezwa kuwa pamoja na hata katika hali ngumu kuleta utukufu kwa jina lake.