
#22 Upungufu Wetu
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #22, Upungufu Wetu, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Malengo ya muda mrefu wa mwamini ni kukua kufikia kuwa kama Kristo, lakini hili lastahili kufafanuliwa zaidi. Punde tunavyowazia yale Mungu anavyotaka kwa maisha yetu, ndivyo itakavyokuwa rahisi kuyafikia malengo haya.
Kama mkufunzi, shule au mzazi na kadhalika, tutatambua kwa haraka kuwa malengo ya Mungu kwa wale wanaotenda kazi ni makubwa zaidi kuliko tunavyoweza kufanya. Hilo ni jambo twapaswa kutambua na kukubali.
Kwanza kubali kwamba mafundisho yetu na baadhi ya watu yategemea kiasi cha wakati – mwezi, mwaka, miaka mitano, na kadhalika. Vile vile wakati wetu nao pia utategemea. Huenda tukafunza darasa kwa lisaa limoja kwa wiki au kukutana moja kwa moja mara kadhaa kila wiki na mtu binafsi.
Pili, ni muhimu kujifikiria sisi kama wasaidizi wa Mungu. Mungu anatimiza malengo yake katika maisha ya kila mtu. Mungu anafanya kazi nasi ili kutimiza malengo yake kwa wengine. Yesu aliwakemea vikali wote waliojiona kana kwamba wako ‘juu’ ya wengine na pia waliotenda kazi kando na malengo ya Mungu.

“Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu; wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo” (Mathayo 23:8, 10).
Yesu hakumaanisha kwamba hatupaswi kuwa na waalimu au kuwaita watu fulani waalimu, (kama vile Rabbi, ona Yakobo 3:1), lakini alikuwa akizungumzia kuhusu mambo yanayohusu shahada, nyadhifa na utafiti. Ni lazima tutambue kwamba tunafanya kazi pamoja na Mungu kuwasaidia watu katika kuendelea kiroho. Hata hivyo, kwa kiasi kikubwa sio sisi tulio wa muhimu. Mfano wa malezi ya maisha ya kawaida hutusaidia hapa. Hatusababishi mtu kukua lakini tunaifanya iwe rahisi ili kukua.
Kuitambua Njia Yetu Vyema
Tunapoingia katika nyadhifa zetu shuleni au kanisani, tunaweza kuona kwamba tunacho kipawa cha uongozi au kufundisha, kipewanacho na Roho Mtakatifu (Warumi 12:7-8). Roho huyo huyo hutumia kile kutufunulia ili kuendeleza kukua kwa wengine. Kipindi chetu cha mafundisho huenda kikaonekana kifupi lakini kuwa na imani. Mwamini Mungu kwa uundaji unaoendelea hata kwa muda huu. Tarajia jinsi unavyoweza kuendelea jinsi Mungu anavyotaka kuleta katika maisha ya mwanafunzi katika wakati huo.
Kumbuka pia hii ni ‘kazi kuu’ ya Mungu. Tenda kazi kwa ujasiri kana kwamba Bwana anataka kazi iliyo kamilika ya kila mmoja wetu na muda ni ndogo mno (ila ni muhimu).
Kutambua Upungufu Wetu
Baada ya kukagua ni nini malengo ya muda mrefu, na yatakuwa sawa kwa kila
mwamini, twahitaji kutambua ni kiwango kipi cha kukua kila mtu
wakati huu? Hebu tutazame kila hali: Wakati: amua ni wakati kiasi gani tutachukua na kila mwanafunzi. Kwa mfano, twaweza kuwa na masaa kumi na matatu ya darasa. Panga ni kipi kitatendeka kila saa na hakikisha kuna zoezi la kubeba nyumbani.
Hali: Je, hali ya masomo ni darasa la watu wazima katika shule ya Jumapili, darasa la chuo, wakati wa mashauri, au pahali pengine? Hali zetu mara nyingi hutuongoza kwa yale twapaswa kuyazungumzia, na pia kwa matumaini makubwa twaona jinsi haya yanaingiana na lile lengo kuu. Kwa mfano, mchungaji anaweza kutaka atumie kijtabu cha majuma manane kila anapokutana na mwanafunzi fulani au chuo cha Biblia kukuhitaji ukisaidia kutimiza matakwa yake.
Vifaa: Vifaa tulivyonavyo kwa ukubwa vinaunda yale tunayoweza kutenda. Pahali pengine paweza kuwa na vitabu na pengine pakose kabisa. Sehemu moja yawezakuwa na tarakilishi na sehemu nyingine wasiwe hata na nauli ya kutosha kwenda darasani. Kuwa mwangalifu kwa mahitaji haya. Upungufu wa vifaa mara nyingi huleta changamoto wa mafundisho dhabiti, lakini Mungu anatufundisha kupitia hali hizi ngumu ili tuweze kuwahimiza wengine jinsi Mungu anavyoweza kutenda, ijapokuwa na upungufu.
Vipawa: Yale tuyatendayo kwa sehemu kubwa hutegemea jinsi Mungu ametupa vipawa vya kiroho. Hii ni muhimu kwa sababu tunauo imani iliyoongezeka kufanya huduma kulingana na vipawa yetu vya kiroho. Lakini kumbuka kwamba utendaji kazi huenda usilingane na vipawa vyetu katika kila hali. Hii inahitaji uvumulivu na kutafuta hekima ya Mungu.
Makusudi ya Mungu: Hili pengine ndilo jambo lililo muhimu kuliko yote.
Mungu hadhibitiwi na upungufu wetu – hata vipawa na raslimali zetu. Hii ndiyo sababu maombi na mahojiano madhubuti ya yale Mungu anakusudia kutenda kwa masaa au dakika hizi ni muhimu.
Baadhi ya watu hujihisi kuwa wametulia na wako tayari hali wengine wamechanganyikiwa na hawawezi. Kiasi kile tunafahamu yale Mungu anataka kutenda, ndipo tuonapo ni kiasi kidogo aje twawezachangia. Haijalishi jukumu hilo ni ndogo kiasi kipi. Mungu yungali anadhamini huduma yako.
Sio ya kudharauliwa.
Waza kumhusu mtu aliyesimama na mfereji akiinyunyizia mimea yake. Haleti maisha au ukuaji lakini kwa huduma yake, Mungu anaweza kutimiza kazi yake kubwa. Huduma kidogo? Ndio. Mchango mkubwa? Ndio pia.
“Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye” (1 Wakorintho 3:6-7).
Kwa hivyo, ijapokuwa twahitaji kufahamu kuhusu upungufu wetu, hatuuruhusu upunguze kiwango cha Mungu au kusababisha kudharau kujitolea kwetu. La hata hatujiwezi zaidi kuliko tunavyostahili. Kutokuwa na imani (shuku) sawa sawa na kiburi huharibu kazi ya Mungu akusudiao kuitenda katika maisha ya wengine.
Kuimarisha Imani Yetu Ili Kufundisha
Tunapoangalia malengo ya Mungu (haya huenda yakawa ni tofauti na malengo ya mchungaji wako au idara yako) twashangaa jinsi twaweza kuyatimiza malengo haya katika hali iliyodhibitiwa, wakati au vinginevyo. Twahitaji muujiza.
Kila wakati ninapokuwa na mikutano ya mafunzo ya viongozi wakristo wa lugha tofauti kwa siku tatu ninakumbana na tatizo hili. Wakati umeadimika, lugha ni kikwazo, yaweza kuwa kuna joto jingi. Nakumbuka wakati mmoja huko India, kulikuwa na kelele kutokana na gwaredi ya sanamu nje ya eneo la mafundisho. Milio ya fataki ilikuwa inashindana na ujumbe tuliokuwa tukifundisha.
Mungu nafasi alitukuze jina lake kupitia nyakati za mafundisho. Anaweza kutimiza mengi kwa dakika moja kuliko yale tunaweza kutimiza kwa wiki moja. Imani yetu inakuzwa kwa kufahamu makusudi yote ya Mungu ya kuwainua watu wake.
“Nami nakuambia wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Mathayo 16:18).
Petro alikuwa amepewa mamlaka mengi lakini bado Yesu asisitiza kwamba atalijenga kanisa lake na hamna chochote kitakachobatilisha mipango hiyo.
Kuishi Maisha Yanayomtegemea Mungu
Iwapo maisha yetu yameundwa kulingana na mipango mikubwa ya Mungu, tutatambua kwamba twaendeleza maisha tu na wala sio kuyaumba. Kristo ndiye mwalimu sio sisi. Kama waalimu wasaidizi na wakufunzi, twapaswa, kuzingatia upande wetu. Tufanyapo hivyo, Mungu anatafuta kutujaza na Roho wake ili tutimize yale yote ambayo Mungu anataka katika hali na wasaa uliopungufu.
Iwapo tutafunza msururo wa mahubiri, darasa ya shule ya Jumapili, kikundi kidogo na kadhalka, twaishi katika mwenye wa makusudi makuu ya Mungu na hivyo basi kwa unyenyekevu kutafuta atuwezeshe ili kuzitenda vyema kazi zake nzuri.
Kumbuka kukemewa kwa Kristo. Iwapo tunadhani kwamba tumeyafahamu
mambo haya, basi sisi ni sehemu ya shida na wala sio suluhisho. Mungu husababisha ukuaji wa haki na hivyo kuwaondoa wanafunzi wetu kutoka kiwango kimoja hadi kingine.
Kristo ndiye Mwalimu Mkuu. Ni Roho yako ambayo itendayo kazi maishani mwa mkufunzi na mwalimu kama vile maishani mwa mwanafunzi au msomaji. Anatafuta mpatanishi atakayepeana ukweli wake. Tuzingatie jinsi
Somo
- Malengo ya muda mrefu hutusaidia kufurahia sehemu yetu ndogo ijapokuwa muhimu katika kufundisha.
- Kwa sababu tuna uhaba wa wakati na mengineo, tunastahili kwa unyenyekevu kutafuta hekima kutoka kwa Mungu ni jinsi njia ipi iliyo bora ya kutumia raslimali ili kuchochea ukuaji wa mwamini.
- Kwa imani, ni lazima tufundishe na tushauri ili kwamba Mungu akachukue kile kidogo tulichonacho na kukiongeza ili kikatimize malengo yake makuu.
- Mwalimu huuweza moyo wake ili utende kazi karibu na Bwana kama msaidizi mwaminifu.
Tafakari Na Kariri
- 1 Wakorintho 3:6-7
- Mathayo 23:8-10
Zoezi
- Taja ni somo lipi muhimu umejifunza kutoka kifungu hiki? Omba kwa ajili yake.
- Je, unakusudia kuweka malengo ya juu na kisha kufedheheka au kuwa na malengo duni na kutoyatimiza? Tafadhali eleza.
- Je, somo hili laweza aje wasaidia wenye kutimiza makuu au wenye kutimiza machache ili wayasimamishe mafunzo yao.
- Tafakari 1 Wakorintho 3:5-10 na fupisha ni njia ipi ya kuwasomesha na kuwafundisha wengine