Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#21 Kuyashika Maoni

Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #21, Kuyashika Maoni, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Kama walimu na kufunzi, tunahitaji kuyashika matokeo kamili ya kile Mungu alichonacho kwa kila mwamini, vile vile kwa maisha yetu wenyewe. Kwa nini? Kwa maana hii ndiyo imani ambayo Mungu angependa tufikie, tushikilie na kuwapokeza wengine.

Kuna wengi leo wanazungumza kuhusu malengo, maoni na makusudio, lakini yote yalitabiriwa katika maandiko awali hata kabla ya mwanadamu wa kisasa kuyafikiria, Mungu hutenda kulingana na ratiba kwa sababu anatimiza mpango wake mkuu. Kazi ya maumbile ni mpango wa ajabu, pia vile vile kilele cha kazi hiyo - kanisa la Mungu- mpango wake wa ukombozi. (Ona Wakolosai 1: 15-20)

Mambo ya nyakati yaeleza mabadiliko ya ajabu yaliyotendeka Yudah wakati wa mageuzi ya Hezekiah yalipenyeza kwa ndani zaidi kuliko wageuzi ya wafalme wa hapo awali kwa sababu alikuwa na matumaini ya jinsi mambo yangekuwa.

Matumaini hayo yalitokana na kusikia neno la Mungu. Alitambua yale Mungu alitaka kuhusu kuitambua siku ya Pasaka na hivyo akatenda kama ilivyohitajika na akawaalika Israeli yote na wala sio Yuda ufalme wa kusini. Alifanya hivyo kwa sababu maandiko yalieleza kuhusu umuhimu wa wanaume wote wa Israeli kushiriki. Alistahimili msukosuko wa kisiasa ili kutekeleza neno la Mungu.

Kiini Cha Maisha illustration from page 117

Malengo yetu yanatokana na yale maandiko kuliko yale tamaduni zetu zatueleza kuwa ndiyo muhimu. Biblia inatufundisha yale Mungu anataka kwa ajili ya ndoa zetu, maisha ya kanisa, uhusiano wa kibinafsi na mambo mengi 1. Je, unaamini kuwa malengo ya Mungu kwako yanapaswa kuunda malengo yako? Je ni hivyo?

2. Je, unaamini kwamba Mungu anaweza kukusaidia kuyafikia malengo haya?

Malengo Ya Matunda

Kama vile ilivyo katika kila mmea shambani mwetu (hata kwekwe zisizohitajika) umepangiwa kukua kwa mpango uliyofichika, hivyo ndivyo pia Roho mtakatifu anafunua mpango wake katika maisha yetu. Matumaini yetu makubwa kwa kitabu hiki ni kufunua uhusiano ulioko kati ya mipango ya Mungu iliyofichika na nguvu za Yesu Kristo maishani mwetu.

Bila shaka kila mtu ana huduma tofauti, lakini kungali mambo yaliyosawa.

Hebu waza kuhusu mizizi ya mimea, matawi, majani na matunda. Kila mmea ni tofauti na pia muktadha na hali kuwa usawa katika matumizi. Mmea wa limau unafanana sana na mmea wa mchungwa, na hali ni tofauti kabisa. Tofauti hii ni kubwa zaidi kuliko tu rangi ya matunda.

Kuna mambo yanayofanana jinsi waamini wakristo wanayoishi maisha yao ya utawa, lakini kutakuwa utofauti kati ya mwito na kujitikeza kwa kusudi la Mungu kwa kila mfuasi wa Kristo. Wanavyozidi kujitolea kukua na kujitolea kwa Bwana, Bwana wetu mwema, kwa wakati ufaao huyafunua mambo haya kwao. Mmea hautoi matunda hadi unapokomaa. Iwapo mmea una afya na nguvu, unaweza zaa matunda mema.

Basi kunayo maandalizi ya kimsingi ya watu wote wa Mungu, lakini pia kunayo maandalizi maalum ya watu jinsi kushiriki kwao kwa kazi ya Mungu kunavyozidi kuwa dhahiri. Hapa ndipo tutakapoanza kuona ukuaji wa kipekee na mabadiliko yatakayotokea mtu aanzapo ‘kuzaa matunda’. Hakuna atarajiaye matunda yaliyokomaa kwa mmea mchanga au kuangazia ukuaji wa Tunda litakuja kwa wakati ufaao. Mungu ameunda mipango hivyo.

“Akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke” (Marko 4:27-28).

Huu ndio msukumo wa nguvu za maisha uwaongozao maisha yetu mapya kwa Kristo. Analeta makusudio yake na anataka tuzae tunda kulingana na makusudio ya Mungu yaliyo mema na ya neema.

Baadhi ya watu, kwa nasaha mbaya hujiepusha kuwaza kuhusu malengo na viwango. Ikieleweka vyema, mafundisho hutuelekeza kwenye malengo haya na sio mbali nazo.

Waza kumhusu mtoto mchanga anayetambaa kwenye sakafu. Wazazi wake wanaweza anza kuwaza kuhusu maisha yake ya usoni mtoto huyo atakapokuwa mtu mzima. Waweza sema mambo kama vile “atakapoolewa … atakapokuwa mkubwa ….”

Hatua hizo za kitoto kichanga, mtoto na vijana wanaobaleghe zote ni za muda mfupi kwa sababu ni za majenzi au maadalizi. Mafundisho mazuri huanza kwa kutambua kila mtu yuko katika kiwango kipi na kisha hatua kwa hatua, kutekeleza m a l e z i n a m a f u n d i s h o yanahitajika. Bila ufahamu na tajriba, tunaiga yale ambayo tumeyapitia. Hivyo ni vizuri kwa kiwango fulani, lakini bado twaendelea kufundisha bila ufahamu.

Mke wangu pamoja nami hufundisha madarasa ya malezi kwa wazazi.

Tunapouliza maswali (na kuna maswali mengi), mke wangu hutambua mtoto yuko na umri upi kabla ya kuyajibu maswali. Katika miaka ya kutambaa, moja au miwili, kuna leta utofauti mkubwa kati ya majibu mtu atayapokea.

Tunapofahamu yale Mungu aliyonayo kwa maisha ya kila mkristo katika kila hatua, basi swali la ‘vipi’ kuhusu mafundisho laanza kuwa dhahiri kwa mwanafunzi na mwalimu pia. Hatutekelezi tu utaratibu wa kanisa kiholela- holela, lakini mafundisho husaidia kuwaandaa waamini kutimiza malengo maalum, kulingana na kiwango cha ukomavu.

Kama waalimu, au zaidi kama washauri, sote pamoja, mke wangu pamoja nami tunaendelea kutmbua mapenzi ya Mungu hata tuendeleavyo kufanya kazi na Bwana, tukitafuta ni njia ipi iliyo bora ya kuyaunganisha mafundisho haya kwa maisha ya wanafunzi. Hamna tofauti na jinsi wazazi wema huwafunza watoto wao.

Makusudio Ya Mungu Na Nguvu Zake

Jambo lililo kuu katika njia hii ni kwamba Yesu Kristo ndiye nguvu za uhai huo zinazozidi kukua ndani yetu. Na kutuongoza kuelekea lengo la sisi kuwa kama yeye. Hii sio kwa bahati, lakini njia iliyo chanuliwa sana. Mungu anaishi ndani ili kutekeleza makusudio yake.

Hatupaswi kuyaunda maisha haya au kuyalazimisha ili kukua. Kama ni ya kweli, yatakuwa na huo msukumo ili, yakue na kuzaa tunda. Kwa kifupi, tunatenda kazi ile Mungu anafanya, kama vile mkulima hupalilia shamba. Kumbuka Yesu alimwambia Petro “lisha kondoo wangu” Petro hakuhitaji kuwapa kondoo uzima ila tu kuwatunza na kuwalisha kama mchungaji mwema. amekuwa akitufundisha sisi.

Somo

  • Maono ya kiroho yanatokana na ukweli wa maandiko ambao unaunda matarajio yetu na mtazamo.
  • Malengo yanapaswa kuwa dhahiri kwa kila hatua ya kukua kiroho.
  • Kwa werevu hatuundi malengo mengine ili kutuongoza kukua mbali kwa uangalifu kuzingatia yale Mungu amesema katika maadiko na kuunganisha hayo na maisha yetu.
  • Mungu ana mpango maalum kwa kila mwamini ili kumzalia upendo na mwanga katika ulimwengu huu. Hili ndilo tunda la mwamini (pia liitwalo kazi nzuri).

Tafakari Na Kukariri

  • Marko 7:27-28

Zoezi

  • Ni nini malengo ya Mungu katika maisha yako kwa wakati huu? Jaribu utambue angalau matatu.
  • Je, unajitayarisha vipi kwa kuunda na kutimiza malengo? Je, unaifurahia au unachukizwa na muundo huu?
  • Ni mpango upi wa muda mrefu Mungu amekusudia kwa mimea mingine ya shambani? Je, hiyo inamaanisha nini kwa maisha ya kiroho?
  • Jikumbushe kuhusu njia ya kutimiza malengo uliyoyataja hapo awali, kisha waaza kuhusu waamini wachache wanakuzingira. Mwombee