
#28 Kuwaandaa Waamini Wapya
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #28, Kuwaandaa Waamini Wapya, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Wapya
Malezi yetu kwa waamini wapya kunaadhiri utaratibu wote wa mafundisho.
Iwapo hatutawaandaa viongozi wetu ili kufundisha, basi ukosefu wa msingi mwema kwa waamini hawa wapya hulemaza huduma yote. Kazi ya Mungu haitatendwa kwa namna na jinsi inavyohitajika.
Mafundisho mema huwezesha kuleta mabadiliko yanayohitajika kuwaandaa viongozi chipukizi ili kuwafunza wengine katika nyanja tofauti za maisha. Kifungu hiki kitatoa mawazo jinsi ya kuwafundisha waamini wapya na umuhimu wa kuchanganya mafundisho haya pamoja na kiini cha maisha.
Kiini cha maisha huzungumzia kuhusu kazi maalum na ya kibinafsi ya Mungu katika maisha ya kila mwamini wa kweli na kanisa kwa jumla. Maisha mapya huanza maafikiano yasiyokoma na ya maisha yote na kazi ya utakaso ya Roho Mtakatifu kwa kila mwamini.

Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Kristo mwokozi wetu” (Tito 3:5-6).
Tambua kwamba kumimiwa kwa Roho Mtakatifu kunaashiria kazi ya Mungu inayodumu na isiyoyumbayumba kama mto unatirika katika maisha yetu.
Mtume Yohana alifafanua vyema kwamba mwamini mpya ana mahitaji maalum kama vile mtoto mdogo, familia hufanya mabadiliko makubwa ya muda na kifedha ili kuridhisha huyo mtoto. Kwa mfano wako tayari kutumia rasli mali zao zilizoadimika kwa kurembesha chumba au kununua vyakula vinavyohitajika kwa ajili ya mwanao. Yohana anatumia mfano huu ili kuongeza ufahamu wetu kwa hitaji lililo kubwa la kumlea mwamini mpya - misingi ya kusitiri maisha.
Mmojawapo ya changamoto ambazo tunazokumbana nazo tunapofundisha wengine jinsi ya kuwalea waamini wapya ni kwamba sisi wenyewe hatujawahi kufunza. Twasema “mimi nilinawiri vyema kwa hivyo mafunzo hayana maana”. Lakini hatuoni jinsi mambo yangelikuwa bora zaidi.
Je, hatuoni jinsi kutoamini kumekita mizizi miongoni mwa vijana? Hawaoni nguvu za injili katika maisha ya mtu binafsi. Changamoto letu kuu ni kuonyesha umuhimu wa injili katika maisha ya kila mwamini.

Makanisa yetu yanatumia muda na fedha nyingi ili kuleta injili kwa maisha ya wengine lakini kidogo mno kwa kuwalea waamini wapya. Ni kama mtu atumiaye fedha nyingi kuinunua mbegu nzuri kabisa ili akuze mmea maalum, lakini baada ya furaha inayotokana na kuona miche ikiota, kisha anasahau kunyunyizia maji.
Iwe ni kanisa, chuo cha Biblia au shule ya mafunzo, ni lazima tukusudie: 1) Kuwashawishi watu wa Mungu kuhusu umuhimu na haja ya kuwafundisha waamini wapya.
3) Kutoa vitabu vilivyopendekezwa ili vikatumike kuwafundisha waamini wapya na 4) Kutoa mwito kwao ili wafundishe waamini wapya wakiwa na mpango wa kuzaliwa ili kutumikia wengi.
Shawishi Wengine
Kuwandaa Wengine
Mara watu wanaposhawishika kwamba kuwafundisha waamini wapya ni muhimu, ni rahisi kuwaandaa. Kama vile mafundisho yo yote, wale wanaofundisha lazima wawe na uzoefu wa utaratibu. Mwalimu lazima kwanza awe na uzoefu wa kufundisha waamini wapya, kisha ataweza kuwaandaa wengine.
Baadhi ya viongozi wamejiandaa kufanya hivyo kuliko wengine. Usisahau kutumia wale ambao wana vipawa, waliomo kanisani au nje ili wafundishe. Ninakumbuka tukiwa watu kumi na watano, tukipitia kijitabu cha mwamini mpya. Niliwapa kijitabu hicho kikiwa tu na vidoze kisha wajaze ndani.
Baadaye hiki kikawa kitabu kikuu chao cha kufundisha wengine. Niliyajenga maono yao pamoja na ujuzi na ufahamu wa kufundisha. Baadaye watawezatumia haya kuwafundisha wengine. (Hapa ndipo nilipoandika 3XE.
Kitabu cha kuwafundisha waamini wapya).
Kunazo njia nyingi za kuongeza mafunzo haya. Njia moja ya kutekeleza haya ni kuonyesha jinsi inavyotenda kazi kupitia kutekeleza majukumu darasani. Kiranja lazima asimamie darasa la kwanza la kufundisha wanafunzi. Kiongozi huyo anaandamana na mwanafunzi wakati wa mafundisho au kwa uangalifu kupitia zoezi la mafundisho baada ya darasa la kwanza. Kumbuka kwamba hili sio tukio la wakati mmoja. Tunaweza kuwauliza watu waliowaoga kuanza kuandamana nasi na kuwasihi kwamba waanze kushiriki katika wakati wa mafundisho. Kwa mfano, tunapozungumzia kuhusu injili na imani, wanaweza shiriki jinsi Yesu alivyowaokoa. Wanajifunza, wengine haraka, wengine pole pole, ili Mungu aweze kuwatumia kuwafunza wengine.
Akina mama wanaweza walisha watoto wao (isipokuwa katika visa vichache), lakini lenye shida ni kwamba hawajui jinsi ya kukabiliana na hali ngumu. Twahitaji kuwa kando yao tukitoa mawaitha kwa njia ya kuhimiza. Usisubiri wakuulize. Unachukua muda na wanafunzi hawa ili wasije wakakata tamaa.
Wape nafasi ya kwanza ya kukumbuka jinsi ya kuwafundisha waamini wapya.
Leta Wengine Kufundisha
Ratiba na vitabu vya kufundishia wanafunzi vinazidi kuongezeka. Hili ni nzuri. Baadhi ya watu wanadhani hivyo. Nilipokuwa mdogo, kulikuwa na vikundi vichache ambavyo vilikuwa na vijitabu vyao vya mafundisho.
Mafundisho ya kanisa hayakuhusishwa vyema. Umuhimu wa mtu binafsi ulichukua nafasi ya upendo na huduma. Mambo sasa ni mazuri kiasi, lakini bado kunao uhasama kiasi kati ya kanisa na makundi yanayohusiana na makanisa. Wanahitaji kufanya kazi pamoja kwa malengo mamoja.
Makanisa machache hutayarisha vitabu vyao. Ningehimiza mtindo huu. Kila kanisa lingeandika vitabu vyao vya mafindisho ya waamini wapya kulingana na desturi zao, hata kutoa nakala tofauti kulingana na mahitaji ya watu wao.
Kijitabu chenye chapa kubwa kingetengenezwa kwa walio wazee. Nakala maalum zenye lugha maalum zingetengenezwa kwa kuwahudumia wakimbizi au nakala yenye picha kwa wale wasioweza kusoma. (unaweza anza na kitabu chetu na kukiandika tena kiwe chenu).
Cha muhimu zaidi ni yale yaliyomo. Kitabu hiki kimeeleza wazo la kusudi la Mungu katika hatua tatu za mafundisho lakini tukaeleza tu kwa kifupi yale yatakayo jadiliwa. Ili kufahamu vyema tazama maktaba yetu ya mafundisho.
Utunzi Maalum
Utunzi wa mahitaji ya waamini wapya lazima yapewe kipao mbele na kanisa kama vile familia hupanga upya ratiba zao na raslimali zao ili kumtunza mtoto mdogo na mahitaji yake, vivyo hivyo kanisa lazima lihakikishe kwamba kunao utunzi mwema wa watoto wapya wa Mungu.
Mwamini mpya anahitaji mafafanuzi ya kimsingi ya injili. Malezi kutoka kwa neno la Mungu na kusaidia kufahamu jinsi Baba yao mpya anavyowatunza. Kusudi lake kukuza imani yao ili wakaweze kuimarika katika imani wakati huu wa usiodhabiti wa maisha yao.
Imani yao inahitaji kuimarishwa ili wasiweze kupotoshwa kwa urahisi mbali wawe na ufahamu mwema kuhusu dhambi, msamaha, Kristo na imani ili Iwapo mwamini mpya atachomokea kutoka mazingira ya starehe, basi atahitaji mafundisho zaidi kuhusu mambo kadhaa ya maisha ya kikristo, jamii na utakatifu. Iwapo wataokokea kutoka mazingira ya sheria, basi watahitaji ufafanuzi maalum kuhusu wokovu, utakaso na uhuru wa injili.
Iwapo mwingine ana shida ya kujipata katika anasa au shida za kinyumbani au kazini, basi maelezo maalum sharti yatasaidia mwamini mpya ili aweze kufaulu dhidi ya mambo ya kipekee yanayowakumba. Haijalishi waliokombolewa kutoka ‘ulimwengu’ upi, wanahitaji mkazo wa kuambatana nao katika eneo hilo. Hii ndio sababu mafundisho ya mmoja-kwa-mmoja katika hatua hii ya kwanza ya kukua kiroho ni muhimu sana. Tusisahau ya kimsingi, hata hivyo kuangazia mkristo mpya kunatokana na ufahamu wa kimsingi wa wakristo huko wakiwasaidia wakristo ili waishi vyema katika ulimwengu utazingatiwa katika hatua ya pili ya kukua kwa mkristo.
Unganisha Imani
Kuunganisha ufahamu wa maisha yao mpya na yale Mungu anayafanya kwa ujumla ni muhimu. Picha hii kamilifu inaeleza ukweli wa kina ambao ni msingi wa maisha yao ya kikristo yanaendelea.
Yatambue mahitaji yao mapya ya neno la Mungu. Ni sawa na mtoto akiyatamani maziwa ya mamake. Wasaidie kutambua kuwa katika maisha haya yao mapya watakuwa wakitaka na kuhitaji neno la Mungu. Kama vile kula chakula, hili litakuwa ni jambo litakalokuwa laendelea ijapokuwa hamu yake ni kuu katika kiwango hiki.
Waamini wapya pia wana hamu ya kuwa na waamini wengine, ili kuomba na kushiriki neno la Mungu na wengine. Hii ni Roho wa Mungu akitenda kazi katika maisha yao akiacha wafahamu kwamba wao ni sehemu ya familia kubwa. Jinsi ambavyo tumedokeza hapa mara kwa mara kuhusu mambo haya, Kumbuka kuunganisha yale yanayotendeka maishani mwao na kwa nini yanatendeka. Roho wa Mungu anatenda kazi ndani yao. Kwamba maisha yanakua na yanajidhihirisha.
Upendo Wa Mungu Usiobadilika
Upendo wa Mungu ni dhabiti na wa kweli. Hata tukianguka, Mungu ameweka njia ya kupata msamaha kupitia kwa Kristo. Yeye ni wakili wetu (1 Yohana 2:1-2).
Iwapo hatujalelewa katika familia nzuri, mara nyingi twajihisi kana kwamba lazima tudhibitishe tupo au tutasalia tukijihisi hatupedwi. Lakini na mafundisho mema, waamini wapya watakua wafahamu upendo wa Mungu usiobadilika kwao, haijalishi malezi yao mabovu.
Hali ya kujithamini (mafundisho ya neema na rehema katika limbuko lake) inakuzwa tunajifunza jinsi ya kujitengea msamaha wa Kristo tusiostahili kwa ajili ya dhambi zao kupitia Kristo. Wataona umuhimu wa kazi kuu ya upendo ya Yesu Kristo pale msalabani kwa ajili yao, sio kupitia kazi au utaratibu/dini zao wenyewe.
Katika kila kiwango, Mungu anakuza dhamani za kimsingi ambazo hatua ile nyingine itategemea. Pasipo ufahamu mwema wa upendo wa Mungu, waamini wapya watakuwa na wakati mgumu kuingia na kusonga mbele katika hatua ya pili ya kukua kiroho.
Leo hii ni shida kubwa ambayo kanisa iliridhi. Ukosefu wa malezi mema kwa waamini wapya huzaa waamini ‘wakubwa’ ambao hawatendi kazi.
Muhtasari
Mengi yanaweza kusemwa, lakini kwa muhtasari kumbuka haja yetu kubadili ukuu wa mambo ili tutilie mkazo wa kusudi ya Mungu katika hatua hii ya Masomo haya ni ya kimsingi na muhimu na kwa dhihaka, yanakosekana kabisa kanisani. Bila malezi haya hawatapata msingi dhabiti wa upendo na kuamini ili kukua vyema katika hatua ya pili ya mafunzo ya Kikristo. Hawakuwa wale waamini ambao ulikusudia wawe, lakini watayumbayumba katika maisha yao ya Kikristo.
Wakati umewadia tuache kuwalaumu wakristo wapya kwa kuwa kigeugeu, na badala yake tuanze kuwapa malezi ambayo Mungu ametuagiza tuwape kuanza mwanzo.
Hatua ya mwamini mpya ni fupi na inastahili kutekelezwa mara moja. Ibilisi yuko tayari kuwamaliza mara moja. Ni sharti tufanye lolote tuwezalo kuwafikia kwanza na kuwaongoza. Kwa muda mfupi wana hamu kuu ya kusoma sana na kukua, na inavutia kutenda kazi nao sasa kuliko kung’ang’ana kurejesha walioshindwa na kurudi nyuma. Hebu na tuwe watendaji wa mapenzi ya Mungu.
Somo
- Kanisa na vikundi vyote vya kikristo vya mafundisho sharti wafundishe waamini wapya kwa uangalifu na binafsi.
- Waamini wapya lazima wafunzwe tukiwa na mtazamo wa siku za usoni, tukizingatia kukomaa kwao lakini pia kuwatumia ili wafundishe wale waamini wengi wapya.
- Vitabu vilivyotengenezwa kwa desturi na waamini wapya sharti zishughulikie mahitaji maalum wanayokumbana nayo katika maisha.
Tafakari Na Kariri
- Tito 3:5-6
- Umefunza waamini wapya. Eleza.
- Ni ratiba au vitabu vipi utavitumia kufunza waamini wapya?
- Waza kuhusu waamini wapya watatu ambao unawajua. Iwapo ungewafunza, ni nini mahitaji yao maalum ambayo ungehitajika kuzingatia?
- Iwapo ungehusika na mafunzo ya viongozi, anza kuweza masomo yaliyoundwa na desturi za watu wako na masomo maalum ili wafunze wengine. Andika umeenda umbali upi na mahali ungeenda kuwa katika mradi huu.