Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#4 Sura Nzuri ya Maisha

Mwanzo wa Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #4, Sura Nzuri ya Maisha, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Maisha ni fumbo la kushangaza amabao inashikilia siri kubwa zaidi duniani.

Sote twajua maisha ya kawaida ni yapi, lakini twaweza tu yaeleza kwa kuzingatia: kutembea, kupumua, kuzaana, kula na kadhalika. Ingawa twasherekea ushindi wa binadamu kwa kuonyesha vyema jinsi chembe za mwanadamu hupangana, bado tumo gizani ifikapo kueleza shina la maisha.

Maisha ya kiroho ni mada ambayo mara kwa mara Wakristo huizungumzia lakini ukweli ni kwamba tunasongwa na kutokuwa na maarifa. Kwa nasaha nzuri, tuna vidokezi vya kibiblia tunavyohitaji kufungua matokeo yanayowezekana katika maisha yetu.

Mifano Ya Maisha

Waandishi wa maandiko matakatifu na hasa Yohana alisema “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu” (Yohana 1:4). Yohana alikuwa akisema bila shaka, kumhusu Yesu. Yesu alikuwa na uhai na uhai ulileta maelewano na kuleta uwazi kwa wanadamu.

Kiini Cha Maisha illustration from page 28

Dhana hii ya msingi wa maisha ni muhimu kupata ufahamu mzuri wa mafundisho. Zaidi tupatavyo wazo juu ya uhai, ndivyo kwa urahisi tutakumbatia maana nyinginezo za kweli. Uhai ndio nguzo ambayo kweli nyingine zote huegemea.

Maisha mapya hueleza mwanzo wa maisha ya kiroho. Tulipopata wokovu, wengi wetu mimi nikiwa mmojawapo, tulitafuta uzima wa milele ili kuepuka hukumu ya Mungu. Hatukuwa na vidokezi kuhusu maana hasa ya wokovu huo. Bila shaka, iwapo tulifikiria, tungejua ya kwamba maisha sharti yawe na Uhai ndio nguzo ambayo kweli zote nyingine zote huegemea. Madarasa ya mafundisho ya neno la Mungu pia yalihusu utakatifu na utakaso (bila shaka mada muhimu). Lakini mara nyingi huelezwa kama wazo badala ya hatua halisi za kuishi maisha ya kiroho. Kweli, ijapokuwa wengi wanaweza kueleza utakaso ni nini, ni wachache wanaweza kueleza utakaso ni nini, ni wachache wanaweza kueleza ni vipi maisha ya kiroho yanapatikana.

Upungufu wetu wa mawazo na kutokuwa kwetu katika uhusiano wetu na

Mungu ni mmojawapo wa shida. Mambo haya yanapuuzwa au yanafundishwa visivyo. Yale ambayo hatuyajui hatuwezi wafundisha wengine.

Picha Isionekanewa

Viongozi wa kanisa waridhika kuifunga tunu hii ukweli kwa njia ambayo ni wanafunzi wa vyuo vya Biblia na wanathiolojia wawezaifahamu. Hii ni kinyume na jinsi Yesu Kristo alivyotumia mambo ya kawaida ya maisha kuwasilisha ukweli muhimu kutuhusu. Kweli hizi muhimu, kisha, zinakuwa hazieleweki ila kwa wale wapendao vitabu vya dini. Hili ni la kuvutia kwa sababu yaonekana kuwa wasomi wa mambo ya dini (wanathiolojia) mara nyingi huwa ndio wakatili na wenye kupinga mafundisho haya. Pengine ukweli umefichwa kutoka kwa macho yao?

Kwa njia ye yote, watu wa Mungu wakiwa wameketi vitini au kwenye mikeka, ikitegemea mahali wanapoabudia, ijapokuwa wamependa kumjua Mungu, kwa sehemu kuu wanabaki wasiojua jinsi wanavyoweza kukua vyema katika uhusiano wao wa kipekee na Mungu. Wengine hata hawatambui kuhusu uhusiano walionao na Mungu. Ukweli wenye dhamani umefungiwa, haufikiki.

Kwa nasaha nzuri, kumekuweko na vuguvugu chache ambazo zimezingatia kukua kiroho, kama vile Keswick Movement, lakini nazo ni chache. Tunaweza pia fikiria kuhusu mikutano ya ufufuo ambayo ilibadili watu wa Mungu maelezo. -- hawakuhitaji kujifunza jinsi ya kuja mbele ya uwepo wa Mungu. Alikuwa hapo katika utukufu wake uliong’aa. Walihisi kwa urahisi.

Kumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu karama na uponyaji. Zina umuhimu katika nyumba ya Mungu na kwa wengine huu ni ukweli uliopatikana lakini hamna kuangazia kanisa, ingawa kukua kwa kiroho hutokana na kukua kwa imani na miujiza. Hili hutendekea wachache wa watu wa Mungu ili kuimarisha imani ya msingi itakayosababisha kukua kiroho.

Lakini sio utaratibu wa kawaida ambao Mungu hutumia kwa wengi wa watu wake. Hii ni kwa ajili ya kudhibitisha kazi za Kristo kwetu – na sio kuwa utimilivu wa vyote.

Mungu ana malengo makuu kupitia kwa miujiza. Miujiza ni mwanzo tu, kwa mfano, ingawa mtu aweza ponywa jeraha la mgongo na kumpata Kristo bado anastahili kuitawala hasira yake kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Uponyaji uliifungua roho yake lakini hiyo sio sawa na uweza wa kuutawala ulimi wake wakati wa hasira. (Waefeso 4:16-29). Iwapo hatajifunza jinsi Roho Mtakatifu atamsaidia kwa hili, basi atamdunisha mke wake nap engine kuibeba riho ya ukandamizaji kanisani.

Nidhamu Ya Maandiko

Maendeleo ya Kikristo yamefanya vyema yanapotilia mkazo nidhamu ya Kikristo inayoambatana na kukua Kikristo, lakini wakati mwingi mkazo umo kwa utaratibu ijapokuwa ni muhimu, waeza sababisha kutokeza kusudi kuu. Je umewahi jipongeza ya kwamba uliomba au kusoma Biblia siku hiyo lakini ukapata kwamba haikuleta ufufuo katika maisha yako? Katika hali hii, marudio yalichukua nafasi ya ufufuo.

Kuhimiza waamini kukua ni kama mfano kuwaambia kwamba watafika waendeko wakiendelea na safari. Mwanzo walifurahi walipoingia kwenye gari na kuianza safari. Lakini baadaye, baada ya kuendesha zaidi na zaidi na bila Mafundisho na elimu ya Kikristo yamefanywa vibaya sana kwa kutambua kule waamini wanaelekea na jinsi wataovyfika huko (na simaanishi mbinguni). Bwana alifanya ukweli huu kuwa rahisi na wa kueleweka. Kwa nini kanisa limekuwa dhaifu ilhali linasomesha ukweli huu? Kanisa linagaagaa katika kutofahamu kusikofaa na kutokuwa na kusudi, isipokuwa neno la Mungu bado linaweza kusoma na kufunzwa kwa urahisi. Wakati umewadia sio tu kujifunza mbali kusambaza umuhimu wa kuwa na maisha tele ya Kikristo. Yesu alisema katika Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele“. Petro alisema, “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa” (1 Petro 2:24).

Somo

  • Mungu anataka tufahamu kweli hizi na kuzishikisha kwa maumbile yake.
  • Yesu na waandishi wa maandiko walitumia mifano hata kutumia neno ‘uzima’ kutusaidia kushika na kufahamu kweli zilizo muhimu kwa maisha yetu ya Kikristo.
  • Kanisa lote kwa jumla bado halijashika wazo hili la maisha na kusudi lake.
  • Taasisi za elimu ya Kikristo zimeficha ukweli uliomuhimu kutoka kwa wanafunzi wake, zikilemaza sio tu maisha yao mbali hatimaye kwa kanisa lile.
  • Yohana 1:4
  • Yohana 10:10

Zoezi

  • Fanya bidii kueleza maisha ya kiroho na jinsi mtu hukua kiroho
  • Ni nini lengo la maisha ya Kikristo? Onyesha dhahiri iwezekanavyo.
  • Je, unawaona watu wakipata wingi wa maisha ya Kikristo katika maisha yao? Eleza jibu lako?
  • Ni shida zipi ambazo zimeendelezwa kwa sababu ya mafundisho yasiyowazi yanayahusu kuendeleza maisha ya kiroho na utimilivu? Eleza kwa nini.