Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#17 Hatua ya Kukomaa

Mwanzo wa Maisha na Wewe

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #17, Hatua ya Kukomaa, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.

Yohana kwa undani anaeleza hatua hii na ya mwisho kama ile ya wa ‘Baba’.

Ingawa kwaweza kuwa na mashaka wakati wa ‘ujana’ hali ya kuwa baba ni dhaliri vyema. Akina baba wana watoto.

Ulimwengu wetu wa kisasa umeharibu kwa wepesi na raha ya kuzugumzia maisha kama vile Mungu alivyopanga kwa sababu ya mwongozo wa kisiasa. lwapo tunaweza pita zaidi ya hapo na kuwaza kuhusu familia zetu, twaweza pata ufahamu wa malengo ya Mungu kumhusu kila mwamini. Kwa sababu kila mmoja wetu amewahi kuwa na baba. Haimaanishi baba zetu walikuwa baba wema. Kwa kweli katika mikutano ninayofanya, napata kwamba sio watu wengi walikuwa na baba wema. Na ijapokuwa wengine wanakiri walikuwa na baba wazuri, hawa ufahamu mwema na jinsi baba mwema alivyo.

Malengo Ya Mungu Kwetu

Kunayo mambo matatu muhimu kuhusu hatua ya kukomaa ya mwamini.

(1) Mungu anataka kutupeleka sote mbele tufikie hatua hii ya tatu na ya mwisho ya maendeleo ya kiroho.

(2) Mungu anataka kila mmoja wetu awaelekeze wengine kwa maisha mapya ya kiroho.

(3) Bwana anatamani tuwalee na kuwatunza wote wanao pokea maisha ya kiroho karibu nasi.

Mwanzo, Bwana anatamani na amepanga kwamba kila mmoja wetu asonge

mbele hadi akomae kiroho. “Hata na sisi sote tutakapoifikia umoja wa imani na Hatua ya ‘mtoto’ ni daraja la kupendeza, lakini sio lengo letu, vile vile hatua ya “kubaleghe” wangali wanajifunza ya Mungu aliyonayo kwao. Mtume Paulo anaeleza hatua hii ya “Baba”. Kama mtu aliyekomaa (sio utoto, lakini amekomaa kiroho) ikiwa na utimulifu ndani ya Kristo. Ishara za Yesu Kristo zapaswa kuonana dhahiri katika maisha yetu.

Ingawa Paulo anatumia baba hapa, ni dhahiri kwamba yeye kama vile Yohana hataji mzee tu kuendelea kiroho kwa waume bali na wake pia. Waamini wote, kutoka kila nchi na tamaduni wanatumainiwa kukua hadi mfano wa Kristo katika wakati huu.

Ili kukua, lazima tufahamu mawazo ni yapi Mungu aliyonayo kwetu. Hili lihitaji imani na mawazo yetu yaweze kusema kitu cha namna hii “Iwapo Bwana anahitaji tukuwe, basi inamaanisha kwamba ametengeneza mipango jinsi tutakavyokua.” Hizi ni kanuni za kukuza imani. (Kwa kweli – ukweli wote, ukijifunza unakuza imani). Mara tujuapo kwamba waamini wote wanapaswa kukua hadi mfano wa Kristo wangalipo hapa duniani, basi sharti tukubaliane kwamba Mungu aliweka mpango ili tukuwe - haijalishi matatizo tutakayokumbana nayo.

Kuwaza Kuhusu Wengine

Pili, Bwana amepanga kwamba ukomavu utazaa maisha mapya. Hizi ni kanuni za maisha au sio? Ulimwengu umkataa maisha na ukaharibu kabisa taswira ya kuzaana. Lakini waza kumhusu mtu ambaye baada ya kuwa mtu mzima, kisha ampata mtu mwingine mwema wa kuoa na kisha watamani kupata watoto. Hamu hizi zimetimiwa ndani yetu.

Tukizungumza kiroho, hatupasi kusahau wajibu wetu kushiriki na wengine injili na kuwaongoza wengine kuwa na uhusiano na Mungu kupitia Yesu Kristo. Tunapowaleta kwa uhusiano na Mungu kupitia Yesu Kristo jukumu la kutafuta wokovu na kukua kwa mzingira mema.

Malezi Ya Kiroho

Mwisho; tunapaswa kuhakisha malezi ya kiroho kwa wote wanao tuzunguka.

Tunapaswa kuwasaidia wote tuwaletao kwa Bwana. Pia ni wajibu wetu kuwasaidia wale Mungu huleta katika maisha yetu.

Katika ulimwengu huu wa kasi, na watu wakibadilisha kazi wakristo wanazunguka ulimwengu kwa kasi sana. Waamini kutoka sehemu nyingine na nchi au duniani waweza kuwa karibu nasi. Tunastahili kuwasaidia kutafuta nafasi ya kuwatumikia. Hatufanyi hivi kwa ajili ya kubiri, kwani hii njia ya Mungu ya kutunza kondoo wake. Mungu hutumia waamini waliokomaa ili wawalee walio karibu nao.

Katika nchi nyingi magonjwa na mikasa zinasababisha mayatima wasiohesabika. Ni jambo la unyenyekevu kuona jinsi makanisa na wachungaji wengi wanajitokeza na kuwapokea hawa watoto - hata ingawa wao wenyewe hawana cha kutosha kwa familia zao wenyewe.

Kwa njia hiyo hiyo, twastahili kutenda kazi yetu kama kanisa kuhakikisha kila mmoja wetu amepata “mlezi” yaani kuna mtu ambaye analea kiroho. Hii ni roho inayokubaliana na agizo la Mungu kuwafanya watu wanafunzi wake - upendo na malezi ya Mungu kwa maendeleo ya waamini. Uanzinshaji wa vikundi kidogo katika makanisa mengi waweza saidia katika hatua hii, lakini kutakuwa na baadhi ya wengine ambao hawaitaingina na mipango yetu. Tuwe makini kwa mahitaji yao.

Ni aibu ilioaje iwapo baba, kwa sababu anatafuta ustaarabu wake mwenyewe, anapuuza mahitaji ya watoto wake. Hayo ni makosa.

Pasipo shaka kuwatunza wengine ni nafasi kuu ya Mungu ya kupeana upendo na hekima yake kwa wengine. Kwa wanaume hii inatuhusisha kujitolea kwao wanakuzunguka. Mungu aweza kuwa anataka kukutumia kuwasaidia wakue.

Somo

  • “Baba mzazi” ni waamini waliokomaa ambao wamepita mashindano wa waamini wachanga na wanaweza angazia kuwalea wengine.
  • Watu wa Mungu wanaweza na wanapaswa kukua hadi kukomaa ndani ya Kristo.
  • Tuwajibika kueneza kanuni za Mungu za maisha kwa wengine na kuwalea ili waendelee kiroho.

Tafakari Na Kariri

  • Waefeso 4:

Zoezi

  • Umekuwa mfuasi wa Yesu kwa muda gani? Je, wewe ni mzazi wa kiroho?
  • Je, umewashughulikia waamini wachanga ndani ya Kristo? Hiyo imeendelea vipi? Ni vipi ungeweza kuboresha?
  • Je, kunaye mtu sasa maishani mwako unayemlea?