
#24 Kufundisha kwa Kusudi
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #24, Kufundisha kwa Kusudi, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Kabla hatujaanza kujadili yale yanayohitajika kutendeka katika hatua na ukuaji kutokana na mtazamo wa kufundisha, hebu tuzingatie ni yapi huunda vipengele tofauti tofauti.
Katika kisa hiki, hebu tuwaze kuhusu lengo la kufunza wanafunzi. Pengine tumeshawafanya watu kuwa wanafunzi. (Uwanafunzi ni mafundisho maalum ya hali ya juu). Tukiwaza kwamba wamekuwa wakubwa, kama vile kila mzazi hufurahia watoto wanapokua, na pia wawezakuwa na tashwishi katika maeneo kadhaa ya maisha yao (pia kama mzazi).
Wakati wa mafunzo ni vyema kuwa makini kwa yale yanayofunzwa kwao. Lengo lililo muhimu kwao ni kwamba, kama sasa, wanastahili kuhisi kwamba wana jukumu la kuwafanya wengine kuwa wanafunzi. Hatuwezi zingatia tu kwamba tumeitii amri hii ila wale ambao tumewafunza wanayo maoni yale yale ya kuwafanya wengine kuwa wanafunzi.
Wale ambao tumewafunza waweza enenda na kuwafanya wengine kuwa wanafunzi. Je, wajua ni vipi? Je, wanajali? Je, wao wenyewe wanajifunza ili wao pia wafunze? Paulo alikuwa akifanya hivyo.

“Na yale mambo uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2 Timotheo 2:2).
Kifungu hiki cha Timotheo wa pili chaeleza vyema utaratibu wa uwanafunzi. Paulo anafunza Timotheo, Timotheo naye anawafunza wengine ili wao nao waweze kuwafunza wengine. Japo ambalo sipendi ni kutekeleza jukumu la wengine. Kunao wakati inabidi kutumika ili kusaidia viongozi ninaowafunza Vijana wengi sasa wanaweka ndoa kando au kuikataa kwa sababu hawajashawishika kuwa ndoa yafaa; na ni heri wawe shelabela. Wazazi wakristo wanawajibika kwa mambo ya watoto wao. Bila kufahamu wanafundisha, wawezakuwa walinuia kuishi pamoja lakini hii ni lengo duni la ndoa. Wawili hao wanapaswa kuwa wamo katika ndoa na familia ili watoto wao watamani pia kuwa na utangamano, uamshano, kufurahishana, upendo dhabiti vyote vikiwa vimechangamana pamoja katika kujitolea kubadilisha maisha.
Wawili walio kwenye ndoa wakaao pamoja kwa ajili ya watoto hawaoni siku za usoni. Iwapo wawili hao wavumiliana hadi watoto watakapoondoka, wanawaonyesha watoto wao kwa nini waidharau ndoa au wasije wakaolewa.
Na je, kuhusu shule zetu za kikristo na taasisi za masomo? Je wanawaza kuhusu yale Mungu angependa kwa jumla? Mara nyingi kupita kiasi, malengo ya muda mfupi, kwa ukubwa yanashawishi mfumo wa elimu ya kisasa, na matarajio ya serikali, pia yaenda kuunda utaratibu na desturi zaidi kuliko yale Mungu asema yuatenda.
Wakriso wanajaribu kukumbana na msukumo huu kwa kuweka kanisa ndogo mahali ujumbe za maisha ya kiroho zahubiriwa. Hili ni la kusifiwa lakini je kiroho badala ya kuridhika kwamba wanatimiza mahitaji ya kushiriki katika kanisa.
Bila shaka Mungu anaweza kutumia nyakati kama hizi kuwafikia wanafunzi walioshawishika ila wale walio na machungu watanyauka zaidi.
Kipeo Katika Maisha Yangu
Acha nimalizie kwa mfano. Baada ya kuhitimu kutoka chuo cha Biblia, kumaliza miaka mingi ya kujifunza lugha na mazoezi katika kanisa nzuri, hatimaye niliona ndoto zangu zikitimia. Nikawa mmishonari wa nchi za ng’ambo na sehemu ya kikundi kikubwa cha watu kutoka humu nchini pamoja na wamishonari kuanzisha kanisa. Watu wakaanza kuja na kumjua Bwana. Sherehe za ubatizo wa kwanza ilikuwa ya ajabu ilifanyika katika eneo la kuegesha magari katika eneo jipya la makazi kusini mwa Taiwan.
Ilikuwa ni baada ya hili ndipo nilipopatwa na mshtuko ambao ulibadilisha maisha yangu. Sikujua nifanye nini na hawa waamini wapya ila kuwashawishi washiriki katika ibada na kujiunga nasi katika baadhi ya shughuli za ‘kikristo’. Si kwamba sikusomea somo la kueneza injili katika chuo cha Biblia. Hata nilisomea somo la kuanzisha makanisa. Nilipata kufunza hata kulea waamini kwa mafunzo. Lakini kulikuwa na kasoro mahali.
Inawezekanaje jambo lililokuwa la umuhimu kwa viongozi wakristo kiasi hicho likose katika mafundisho yangu. Hiyo ilikuwa ni miaka mingi iliyopita sasa, lakini kila wakati ninawaza kuhusu tukio hilo.
Kwa njia moja sikuwa nimefunzwa jinsi mwamini anavyokuwa na jinsi ya kuwasaidia katika kila kiwango cha kukua. Utaratibu wa kuwaunda wanafunzi haukuwapo katika mafunzo yangu.
Tangu wakati huo, nimechukua muda kukagua mafunzo yangu na ya wengine walio karibu nami. Nilitambua kwamba sijapata kufahamu yote ambayo kuunda ufahamu wa jinsi yalivyohusiana na jinsi maisha yote hukua kiroho.
Baada ya kusafiri na kufunza katika nchi nyingi na makanisa mengi, niligundua kwamba shida hii haijadhibitishwa katika maeneo fulani ya nchi, dhehebu au masomo. Waamini wachache na makanisa machache yana maono ya kuwakuza watu wake katika kuwafundisha wanafunzi. Hata yale makanisa ambayo yana juhudi na kujitolea kukubwa kwa uchache wana mafundisho. Hii inatokana na kutohusisha vifungu vya mafundisho na taswira kamili.
Je, haitakuwa makisio mema kwamba hata baada ya miaka elfu mbili, kanisa bado halijafahamu na kutekeleza msingi ya mafundisho? Je, ni kwa nini mambo yaliyo ya msingi yamepuuzwa?
Kwa maoni yangu, mmojawapo wa pingamizi kuu ya kuunda vuguvugu la watu watauwa waliojitolea kwa Mungu na kuwafundisha wengine vyema ni ukosefu wa taswira kamili ya maisha ya kikristo. Wakristo bado hawajafikiria kabisa kwamba kila mwamini yuko katika kiwango tofauti cha hali ya maisha ya kiroho na wanahitaji maelezo maalum ili kuwafikisha katika hatua au kiwango kingine cha kukua.
Ukosefu wa malengo dhabiti ya Mungu inaruhusu malengo mengine madogo madogo na hafifu kutimiza azma yetu ya mafundisho. Wakati malengo yetu makubwa yanapowekwa kwa kuwaza kuhusu mfano wa maisha ya Yohana, basi mifano hiyo inatupa yale tunayohitaji kurekebisha na kudumisha mafunzo ya muda mfupi.
Somo
- Malengo ya muda mfupi lazima yaundwe na kuunganishwa na malengo makuu ya kiroho ambayo Bwana amekusudia kwa kila mwamini.
- Maono yote ya maisha ya kikristo na matukio hayatoshi kuwapa wengine kwa sababu ni wachache wanaohusisha malengo yote ya Mungu na malengo ya muda mfupi ambayo Yohana ametupa.
Tafakari Na Kariri
- 2 Timotheo 2:2
Zoezi
- Je umewahi kufundishwa ili kuwafunza wengine? Je, kwa kweli unafanya hivyo?
- Iwapo ndio, ni mwamini wa kiwango kipi ulipewa ufanye kazi naye? Eleza ilikuwa vipi?
- Iwapo umeoa (iwapo la, waza kuhusu wazazi wako), je, ndoa yako ni mfano wa ile ungekusudia kwa wanao?