Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#8 Mfahamu Roho

Mwanzo wa Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #8, Mfahamu Roho, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Mkondo wa mto mkubwa ni mmojawapo ya njia za kuonyesha nguvu

zinazitiririka katika maisha ya mwamini. Nyingine ni upepo mkali uvumao. Ijapokuwa dhoruba yawezakuwa na upepo wa ghafla, zote ni sehemu ya tufani kuu ambazo ni utaratibu mkubwa. Upepo unayo majina na huendelea katika mpangilio fulani.

Mikondo hii yenye nguvu hutusaidia kuwaza kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Kwanza kama vile tuliwasilisha katika sura iliyopita, kumbuka kwamba Mungu anatimiza makusudio yake. Kati ya tufani, twaweza changanyikiwa ni mwelekeo upi upepo unavuma. Hata hivyo, hatupaswi kuwa na wasiwasi. Mungu yumo katika usukani hata wakati nguvu za uovu ziinukapo. Jukumu letu ni kudhibitisha makusudio makuu ya Mungu na kutekeleza wajibu wetu mdogo lakini muhimu. Thibitisha kwamba unataka kutumika kwa makusudi ya Mungu haijalishi hali yetu yaonekana ngumu kiasi kipi. Kumbuka kwamba sisi sote tunazo nguvu za kutekeleza makusudi ya Mungu. Twahitaji pamoja kudhibitisha nia yetu kumpendeza Mungu lakini pia kuzitegemea nguvu zake.

Kuinuka kwa upepo kunatupa taswira ya jinsi twahitaji Roho wa Mungu atusaidie. Tai wanayo mabawa yenye nguvu lakini bado wanahitaji mkondo wa hewa ya joto kupenyeza chini ya mabawa yake ili kuwainua.

Ninaye rafiki ambaye huanika tiara angani (tazama picha). Sitaki kufanya hivyo. Tunao uamuzi iwapo tuanike tiara au la, lakini sio kwa kuishi pamoja na Roho wa Mungu. Swali ni,” Je, twafahamu vipi kuhusu kazi za Mungu zenye makusudio maishani mwetu?” Imani ya waamini wengi hapo ndipo husitasita kusema “sijui ni nini Mungu anatenda.”

Kiini Cha Maisha illustration from page 46

Hatua Zisizowezekana Maishani

Kila wakati Roho atatuongoza kuyatenda mapenzi ya Mungu. Wakati mwingine hatua hii itatuongoza katika njia ionekanayo kuwa haiwezekani. Ni kwa nini ionekane kwamba haiwezekani?

  • huonekana kubwa kuliko uwezo wetu
  • Kupungukiwa na wakati
  • Upinzani kutoka kwa familia na marafiki
  • Upungufu wa uwezo na karama
  • Ukosefu wa ujasiri

Orodha hii yaweza endelea sana. Hata hivyo roho wake nyakati zingine atatuelekeza kwa hali ngumu. Je, umewahi kukumbana na mtu mgumu? Bila shaka. Unaweza kuwa na uhakika kwamba pia atakupa subira au cho chote unachohitaji ili kumpenda. Hii ni ishara ya njia ya Mungu – akituuliza kuenenda zaidi ya uweza wetu wa kawaida ili tuhitaji kumtegemea.

Mara nyingi twataka kuelekea kwenye mvuto wa kawaida ikitegemea utu wetu na tabia zetu. Watu wengine wako na ujasiri wa kila kitu – kama Petro. Kila mara hawafanikiwi. Wengine ni waoga kama vile Tomaso. Watakata tamaa kwa sababu ya shaka. wake. (tazama kitabu chetu cha daraja ya pili ya mafundisho ili kuelewa vyema utaratibu wa kukua kiroho na vita – Reaching Beyong Mediocrity). Ni Mungu pekee aliye na nguvu, hekima na maono ya kujua jinsi atakavyotekeleza mapenzi yake, hasa na adui mwerevu kama shetani anayetaka kutumaliza.

Endelea Kuwa Macho Na Mwaminifu

Yesu alisema “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41).

Mwamini wa ukweli anatamani kumpendeza Mungu, lakini mara kwa mara tunaanguka majaribuni wakati hatuoni jinsi Mungu anaweza kutusaidia kukumbana kila hali. Twahitaji sio tu kumtegemea Mungu katika maombi ili kupambana naye ale atakayo lakini pia kujifunza jinsi ya kupata imani, nguvu na hekima kutoka kwake. Wakati tunapoanza kuomba, twaweza kuwa hatuna mambo haya yote yanayohitajika, mbali tukija kwake kwa maombi, atatutimizia.

Mapenzi ya vitu vya Mungu na kutamani kukumbatia vitu vya Mungu vyote vyatokana na Roho Mtakatifu aliyetiwa ndani yetu hapo mwanzo tulipomwamini Kristo kwa ajili ya wokovu na kuzaliwa mara ya pili.

Hatuhitaji kuvumbua au kutengeneza hisia hizi kwa juhudi yetu wenyewe. Mwamini mpya anaweza mwabudu Mungu kwa undani sawa na mkristo aliyekomaa. Hatuhitaji kushindana ili kukuza hamu hii lakini hali ya kutatanisha huja wakati tunapojiuliza ni nini tunachopenda, sisi ni akina nani na ni yapi tunastahili kutenda. Kuupata ukweli wa Mungu kunabainisha sisi ni nani hasa ndani ya Kristo. Wakati huo yule mwovu akitafuta kutuvua utu wetu.

Mungu ndiye nguvu zetu. Upepo huo wenye nguvu unatubeba tunapozidi kudumu katika kanuni zake na kumwita yeye atusaidie.

  • Mungu anataka tumtegemee kwa hekima, wakati, nafasi na mambo mengine ili kuifanya kazi yake
  • Bwana anatamani kwa hamu kutupa kile tunastahili kuwa nacho ili kuyatenda mapenzi yake, lakini twaendelea kutegemea nguvu zetu ambazo zitashindwa bila shaka.
  • Wakati mwingine tunakumbana na watu na hali ngumu lakini Bwana yungali pamoja nasi kutusaidia ili tufaulu, hata iwapo muujiza utahitajika.

Kariri Na Tafakari

  • Mathayo 26:41
  • Zaburi 5:3
  • Isaya 40:31

Zoezi

  • Ni kwa njia zipi una mazoea ya kuzitegemea nguvu zako mwenyewe kuitenda kazi ya Mungu na kisha kufadhaika na kushindwa?
  • Je wewe una utu wa namna gani? Je, huu utaadhiri vipi jinsi utakavyo jikwamua katika hali ngumu?
  • Ukizingatia Mathayo 26:41, je unakesha na kuomba wakati unapo kumbana na hali ngumu au ni nidhamu yako ya kiroho ya kila siku? Fafanua.

Mwanzo wa Maisha na

Wewe Kifungu #9-18