
#16 Vijana-Hatua 2
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #16, Vijana-Hatua 2, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Iwapo mwamini mpya anahitaji mapenzi ya dhati na malezi, je mwamini ya ujana anahitaji nini?
Mwanarika hujulikana kwa njia ile huanza kuchukua usukani wa maamuzi yake. Kunayo mabadiliko kutoka wakati alipokuwa hawajibiki na mpumbavu kwa ni yapi yaliyo mema na kwa wema hujitunza na baadaye kuwajali wengine. Wanarika wako katika hali ya kuwa watu wazima na kwa hivyo, kwa wakati mmoja watajua kujifunza na wengine. Kuyaweka malengo ya Mungu katika mawazo ni kwa umuhimu mkuu, ili kupunguza uhasama unaoweza kutokea.
Hatuna ishara za kuonyesha ni wakati upi hatua hii huanza wala wakati wa kumalizika. Lugha nyingi duniani hawana jina maalum kama vile ‘vijana wanao balekhe’. Jina asilia katika lugha ya kigiriki inaeleza kuwa mwamini ni kijana, kuwa sio mtoto mchanga wala aliyekomaa.
Changamoto Za Mwamini Wa Makamo
Mwamini wa makamo lazima ajifunze kutumia neno la Mungu ili aweze kusimama imara kinyume cha ushawishi na majaribu ya yule mwovu. Neno la ya hatua muhimu za kuwa mshindi.
Ukweli wa maisha unaonyesha hivi. Wakati vijana wanakuwa wazee, lazima wajifunze jinsi ya kuhudumu bila wazazi wao. Mfumo huu huchukua muda sana kwa wanadamu ukilinganisha na wanyama, lakini baadaye hutendeka.
Ingawa watoto wachanga wanajifunza kujilisha wenyewe tu, wale walio karibia utu uzima wahitaji kujifunza kutenda kazi kusudi wapate chakula ili wapate kula.
Katika maendeleo ya kiroho, wanarika kiasi wanahitaji neno la Mungu lakini hawawezi wategemea wengine kuwalisha kile wanachokihitaji. Waamini hawa hunaanza kujifunza kwenda kwa neno la Mungu kujilisha wenyewe.
Kuongezea wanajifunza jinsi ya kutumia neno la Mungu kujikinga wenyewe kutokana na adui anayewavizia.
Tazama maneno makali ambayo Yohana ametumia hapa kueleza mwamini wa makamo “Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi watoto, kwa sababu mmemjua Baba. Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemujua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu” (1 Yohana 2:12-14).
Ulimwengu huu sio mzuri na wa msaada kama tungelitamani uwe. Kunayo adui ambaye anatafuta jinsi ya kutumaliza. Tunastahili kupata faraja kwamba Yesu Kristo ameshavishinda vita, lakini mwamini wa makamo lazima ajifunze binafsi jinsi ya kuitegemea neema ya Mungu kumlinda anapokabiliana na hali tofauti katika maisha. kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2 Petro 1:4).
Vijana hupenda kujiwaza kuwa wazee kuliko jinsi walivyo, wakidai uhuru bila majukumu. Si wenye hadhari na wamekosa maarifa ya changamoto zinazowakumba. (Labda hii huwasaidia kuwa na hamu ya changamoto yo yote).
Hatua Zaidi Ya Kukua
Wamo kati ya hatua hizi mbili za “watoto wachanga” na “watu wazima”. Hamu ya kuwa mtu mzima ni nzuri. Wanalishika wazo ambapo Mungu anawaongoza kushika. Hawa ‘vijana’ hata hivyo wana mfumo wa mawazo yaliyotokana na utoto, yale ya kuwategemea wengine ili wawalishe. Wanapo komaa, wanahitaji kuyaachilia ili wakaweze kuendelea hata kufukia hatua ya “baba” ambapo watawalea wengine.
Mwana mwenye hekima huanzisha nidhamu nzuri ya kiroho na hujifunza kutoka kwa wengine jinsi ya kutumia neno la Mungu kuyashinda majaribu. Kwa jicho pevu mwamini huyu wa makamo atatambua kuwa kuna vita ndani na nje. Atastaajabu kwa nini yeye kama mwamini anakumbana na vita vya namna hiyo, hata na vitu anavyovipuuza. Kwa wakati huo huo, atahisi uovu ulioko duniani ukimshawishi kutembea katika njia za anasa na upumbavu.
Mungu amevishinda vita na amemuandaa mwamini wa makamo kupigana na kushinda vita. Hili litachukua muda kujifunza. Kutakuwa kushindwa na kushinda. Iwapo mtu atamfundisha mwamini huyu, wakati wa mafundisho utakuwa mfupi. Mwalimu anaweza eleza jinsi maisha ya kiroho ya kuendelea yalivyo. Anaweza msidia kuelewa masomo, la sivyo waamini wapya itawabidi kupigana vita vya ziada na pengine kushindwa tena na tena, hata kuvunjika moyo. anawezaonekana amekomaa kwa ajili ya umri wake au asili yake. Usimamizi utasaidia katika hatua hii na utasaidia mwaamini “aliyewazi” wakati anapokumbana na majaribu na pingamizi.
Somo
- Waamini wa makamo wanakumbana na changamoto za kujifunza neno la Mungu ili kuishi maisha yenye nguvu za Kikristo.
- Vita vya kiroho vitatendeka katika maisha mapya kwa sababu ya miili yetu na adui atumiaye dunia kutaka kutuumiza.
- Mungu ameahidi kwamba neno lake litatusaidia kuishi maisha ya ushindi kila wakati.
- Usimamizi wa kiroho katika hatua hii unaweza msaidia mwamini wa makamo aliyechanganyikiwa ambaye huenda asifahamu kwa nini mambo fulani hutendeka katika maisha yao ya kiroho.
Tafakari Na Kariri
- 2 Petro 1:4
Zoezi
- Je, una nidhamu nzuri ya kiroho ya kujilisha neno la Mungu? Kwa nini? Au iwapo la, kwa nini?
- Je, unadhani kujilisha neno la Mungu kila siku ni muhimu kwa maisha ya nguvu ya kiroho? Kwa nini unadhani hivyo?
- Tafakari kuhusu wakati mmoja ulioshindwa na pia kushinda. Waza juu ya kila moja yao, kwa nini ulianguka? Ni kwa nini ulishinda?
- Je, umekomaa kiasi cha kujua ni yapi ya kusema?