Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#2 Mtazamo Ufaao

Mwanzo wa Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #2, Mtazamo Ufaao, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Mtazamo huelekeza jinsi tunavyo fikiria, kumbana na shida za maisha na kujaribu kutatua shida. Mtazamo waweza kutusaidia au kutuumiza ikitegemea jinsi unavyolingana na Biblia. Kwa mfano, dunia huonekana tofauti ukiwa angani na jinsi ilivyo ukiwa ardhini. Ni dunia ile ile lakini mtazamo tofauti.

Mtazamo wa Biblia hutoa picha sahihi ya kuutazama ulimwengu. Zaidi ile mawazo yetu yanakumbatia dhana zisizo na ukweli, zinazuia keundelea kwetu kwa kiroho kutokuwa zaidi kama Kristo na kuziendeleza kazi zake nzuri.

Yapaswa kuwa dhahiri kwa kanisa kwamba limeshikilia mtazamo usio wa kweli wakati haliishi maisha machangamfu ya utawa. Kanisa dhaifu na tabia zisizo njema hudhihirisha kufifia kwa imani yetu ndani ya Kristo. Wakati huo huo hudhihirisha kwamba tunamiliki imani kubwa na kutegemea kitu kingine (kama vile mifano).

Ulimwengu unashambulia moyo wa jamii kupitia teknologia ya kisasa. Kizazi hiki, kwa njia nyingi, bila kujua kinashawishiwa na rasilimali zisizo na uungu wa namna yeyote, ziwe ni muziki, kanda za picha, vitabu na kadhalika. Anasa za dunia zinatishia hali yetu kwa sababu, bila kufahamu tunakubali kusudi la dunia. Hatuwezi endelea kuilinda nyumba zetu za kikristo na kanisa letu kutokana na uovu iwapo tutaikaribisha kusudi hilo.

Kiini Cha Maisha illustration from page 19

Kufanya Maamuzi Muhimu

Kanisa ni kama taifa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tunalazimishwa kuwafundisha watoto wetu, japo twachukua, kuchukua nafasi zetu na kupigana. Sisi, kama kanisa tutawafundisha watoto wetu kuwa Kanisa la kikristo kote lakumbwa na tatizo hilo hilo. Mageuzi haya yanakumba kila nchi na tamaduni kwa mawasiliano ya mtandao. Nimerudi kutoka kuwafundisha wachungaji na viongozi wa kikristo katika mji mdigo kusini mwa Malawi. Hebu kisia yale niliyoyagundua? Vijana walikuwa katika mtandao kwenye simu zao za rununu. Wao ni masikini lakini ushawishi wa dunia unavuka mipaka na umaskini unayaunda mawazo yao.

Mashambulizi yamefika. Haja ya kunoa ufahamu wetu wa Biblia na kujitolea ni kwa dharura hasa ulimwengu na kujisifu, kiburi na mawazo ya uongo yanyemeleapo mawazo yetu.

Hata tukiliamsha kanisa kuona hatari, je, hilo ndilo suluhisho? La. Mitazamo iliyosindiliwa haibadiliki kwa haraka. Ni vigumu kukubali ujinga wa makosa yetu, lakini Bwana amekuwa akitupa yote tunayohitaji kupigana na kushinda. Waamini, hata hivyo, kama mtu ashikaye upanga kwa mara ya kwanza, hakufaa kabisa kwa kudhibitisha neno lake.

Mabadiliko Yaja

Mabadiliko lazima yaje. Yaja lakini natumai sio kwa unyanyasaji zaidi wa njia za dunia. Ni lazima tufahamu ukweli wa Mungu na kuenenda kwa ushindi kwa kuwafundisha wengine katika haki.

Tafadhali usikosee – hatuzungumzii kweli mpya, mbali neno la Mungu lililodhibitishwa “Kila neno la Mungu limehakikishwa; yeye ni ngao yao wamwaminio” (Mithali 30:5). Hamna kilichobadilika.

Unyonge wetu unadhihirika. Giza inaanza kunyemelea kanisa. Sasa huu ndio wakati wa kurejelea ukweli wa Biblia. Mtazamo wetu wa elimu ya Kikristo umekuwa, kwa sehemu kubwa unashawishiwa na utaratibu wa dunia. Wanaohitimu kutoka shule za Biblia na shule za Kikristo hawafundishwi

Mtazamo Wa Mungu

Tunahitaji mtazamo wa Mungu katika hali zetu. Tunaona nini? Mungu alilipa kanisa vyote litakavyo ili kuwa na nguvu na wachangamfu tukiwepo magharibi au mashariki. Amefanya hivyo ili kwamba watu wake waweze kuangaza tabia ya Yesu katika tabia, imani na azma yao ili kutimiza kazi ya Baba yetu.

“Na walipomwona, walimwabudu lakini wengine walitia shaka. Na Yesu akaja karibu na kusema na hao Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo 28:16-18).

Mungu ameahidi kutupa vyote tunavyohitaji kama vile alivyowapa waisraeli mamlaka ya kuishinda nchi ya ahadi. Yesu Kristo ana mamlaka. Je, unaamini au unashuku neno la Mungu?

Somo

  • Kanisa duniani kote liko kwenye hatari kwa sababu ya ushawishi wa dunia unaoongezeka katika mawazo yetu na maisha yetu.

Kariri Na Tafakari

  • Mithali 30:5
  • Mathayo 28:16-17

Zoezi

  • Je, unafikiri kanisa, baada ya kuwa na ukweli wa Mungu pamoja na ahadi na uwepo wake, linaweza kushinda yale yanayofishia kanisa? Au, kama wanafunzi wa kale, una shaka? Iwapo ni kweli, unashuku nini?
  • Waza zaidi juu ya hali yako, weka alama kule ambako unahisi ushindi na pia kushindwa.
  • Maisha ya kibinafsi
  • Kazi
  • Familia na nyumbani
  • Huduma
  • Kwingine