Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#27 Kuwafunza Waamini Wapya

Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #27, Kuwafunza Waamini Wapya, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Wapya

Katika vifungu vilivyopita, tumekuwa tukitambua yale tunayoamini kuwa ndiyo makosa ya mafunzo ya viongozi ambayo yamesababisha kuweko kwa viongozi na makanisa ambayo ni dhaifu, hayana utawa na hayajatayarishwa.

Ingawa hapo hatuwezi toa maelezo yo yote yanayohitajika katika kila hatua ya maendeleo ya kikristo tunatumai kutoa ufahamu wa kutosha wa ni kipi kinachostahili kutendeka. Hii itaelezwa kwetu kutoka kwa kwa mtazamo wa mshauri, mchungaji au mwanafunzi, tukiwasaidia kuwaza jinsi wao kwa uchacha wanafaa kuwaandaa watu wa Mungu.

Nguvu za maelezo ya Yohana ni jinsi kila hatua ya maendeleo ya kikristo inavyotangulizwa. Yohana anawatenganisha waamini katika vikundi vitatu. (Tambua kwamba sio madhehebu). Watoto wadogo, vijana na akina baba, katika kifungu hiki tutaangazia waamini wapya- watoto wadogo.

“Ninawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda Yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo.

Kiini Cha Maisha illustration from page 151

Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmeshinda yule mwovu” (1 Yohana 2:12-14). waalimu na wakufunzi. Kutokana na maneno ya Yohana, ni rahisi kutambua ni nini malengo kuu ya Mungu katika kiwango hiki cha kukua kiroho. Wakati huo huo tunaweza kujua jinsi ya kuwafundisha waamini wapya. Malengo ya Mungu kwa waamini na mafundisho yetu lazima yawe yanahusiana na majaribio madogo.

Kwa njia moja, hoja hii muhimu ya kufundisha na kufanya wanafunzi ( Mathayo 28:20) haijatekelezwa vyema. Wachungaji wachache wanaamini kuandaa wanafunzi ni muhimu, lakini hawatadhubutu kusema hivyo, ni dhahiri kutokana na matendo yao au ukosefu wake. Ingawa twashukuru kwa mwaliko wakumpokea Kristo, kupuuza kwetu kuwalea hawa waamini wapya, kunafedhehesha sana. Tungeshangazwa iwapo tungemwona mama akimzaa mwana na kisha kuondoka na kuenda zake, akiwaza kwamba kazi yake imekwisha. Baadhi ya wainjilisti, kama vile Billy Graham wametenda kazi kiasi cha kufuatilia. Lakini mazoea ya kuhubiri pasi na kufuatilia na mafundisho, kunadhihirisha dosari moja inayochangia waamini wanyonge.

Haijalishi historia yetu wala tamaduni tulizoachiwa, kanisa limeitwa na Mungu kuwamiminia upendo mwamini mpya na kumpa malezi ya kiroho kila mtu binafsi wakati huo huo. Hasa katika hatua za mwanzo, kanisa lahitaji kuwa limepewa mafundisho ili kupeana hayo malezi. Kazi ya mchungaji, mwinjilisti, mwalimu itakuwa ni kutayarisha kanisa ili kutekeleza majukumu yake ya kimsingi ya kuwafanya wanafunzi.

Katika vitabu vingine vyetu vinavyohusu uwanafunzi vinatoa mafundisho zaidi katika nyaya hii, lakini ni muhimu kwamba tikapate kuona jinsi hilo lifanyalo kazi katika mazingira ya mafundisho.

Kwanza kama wakufunzi ni lazima tuwe na maoni ya kwamba ni jukumu la waamini waliokomaa kulea na kusaidia mahitaji ya kimsingi ya waamini wapya. Mwamini wa miaka miwili akiwa ametayarisha vyema, anastahili kuwa na uwezo wa kumwaada mwingine mpya. ukweli wa kimsingi wa neno la Mungu na kushirika jinsi ya kutatua shida zinazowakumba. Shida zaidi zinafaa kupewa mchungaji.

Tatu, twastahili kuonyesha jinsi mafundisho ya waamini wapya yanaingiana na taswira yote ya kukua kiroho na mafundisho yote. Mtazamo huu humsaidia mkufunzi kuyasambaza moyoni ya yale yanayotendeka kwa waamini wapya na itatumika kuwafunza waamini wengine katika siku za usoni.

Nne, tambua yale waamini wapya wastahili kusoma na kuyashika katika kiwango cha kwanza cha kukua ndani ya Kristo. Hii itahusisha kutafuta au kutayarisha masomo ya kufundishia (hilo ilitachukua pengine majuma saba hadi kumi kukamilika). Hayo yatatumika kama mwongozo wa wakati wao na waamini wapya.

Kwa kweli Yohana ana mengi ya kusema kuhusu mfumo huu wote katika kila kiwango. Kunayo mkusanyiko maandiko wa vifaa vya kuwafundisha kwa wao waamini wapya.

Mtazamo Mkubwa

Mungu hufanya kazi na mwanafunzi na mkufunzi kwa wakati mmoja. Hebu waza kumhusu mama na mtoto. Mungu anapendezwa kumwona akimlisha mtoto wake ambao amemleta humu duniani. Mama naye amebarikiwa kuona jinsi Mungu anavyotumia kulisha mtoto (ijapokuwa kuna changamoto pia).

Vivyo hivyo, njaa na watoto wapya wa Mungu hawakumbusha wale

watafaidika kwa kuona jinsi Mungu hufanya kazi na mchango wao, japo mdogo kwa maisha ya mwamini mpya.

Mkufunzi asiridhike kwa kufundisha waamini wapya waliochini ya ulezi wake mbali awafundishe vilivyo ili wao nao waweze kuwafundisha wengine.

Ijapokuwa hili litachukua muda mrefu wa mawasiliano na kukutana. Wanafunzi kwa sehemu kubwa hujifunza kupitia mifano yetu.

Mafundisho ya mwamini mpya yamedhibitiwa na wakati, tupende tusipende.

Kama vile mtoto mdogo hukua kisha anachishwa maziwa katika umri wa miaka miwili, mwamini mpya anahitaji kufunza ukweli wa kimsingi wa imani mara moja. Ninapoendekeza wakufunzi wakutane na waamini wapya. Kweli hizi yapata mara saba hadi kumi mara tu wanapoamini.

Wale ambao wanawafundisha wachungaji na wainjilisti sharti wasambaze maono haya kuhusu yale Mungu anakusudia kutenda katika maisha ya waamini, ijakuwemo kuwafundisha waamini waliokomaa ili kuwafunza waamini wapya. Hili lisipokuwa mojawapo ya malengo yetu makuu katika kufundisha, basi wote tunaowafundisha watakuwa kama mimi - mwamini mpya asiye na habari jinsi ya kuwafundisha wengine au jinsi ya kushughulikia changamoto zangu mwenyewe.

Hata hivyo, shida ni kubwa kuliko hivi. Kwa kuwa tusipokuwa na haya maoni au ufahamu ya jinsi ya kuwafunza wengine ili wawalee waamini wapya, tunaharibu nafasi nzuri ya kuanza kufundisha viongozi na hatuwapi waamini wapya wale wanayohitaji ili kukua na kunawiri.

Je, unaamini matatizo yaliyomo maishani mwa waamini kwa kweli yalianza kutokana na ukosefu wa mafundisho mapema? Ni aibu ilioje kwamba kanisa hupatikana likikashifu waamini kwa kutokua kiroho badala ya kutubu kwa kutopeana mafundisho na malezo ya Biblia kwao ili wakaweze kukua.

Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kugumu. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga” (Waebrania 5: 12- 13).

Changamoto Letu

Katika wakati huu ambapo kuna sauti nyingi za zinatoa ushauri, twahitaji, kama vile mama kwa kitoto kichanga, twahitaji kusambaza malezi yanayohitajika kwa dhati ya mmoja - kua mmoja na kuleta maziwa ya neno la Mungu yanayohitajika katika maisha yao.

Ninapenda kuyasikiza fasiri ya watu wa kanisa letu. “Nilisaidiwa sana na ndugu huyu au yule. Sitasahau yale niliyojifunza” Heri maelezo hayo yakaongezeke duniani kote. Kinachohitajika kwa dharura ni mafundisho ya ‘mtoto’ ambayo hufungua milango ya maisha ya wakristo walio na nguvu jinsi wanafunzi wanavyolewa basi nao vile vile watakuwa wanaouwezo wa kuwafundisha wengine.

Somo

  • Kila mwamini mpya anahitaji mwamini aliyekomaa zaidi ili akamfunze binafsi.
  • Pasipo mafundisho ya binafsi, waamini wapya hutipia changamoto nyingi zaidi na mara nyingi huacha kanisa.
  • Wale wanahusika na uinjilisti na huduma za malezi wasifundishe tu mashauri ambayo hufunza waamini wapya binafsi mbali wasambaze maono kwamba siku moja kwa kuongozwa na Mungu watawafundisha waamini wapya.
  • Waebrania 5: 12-

Zoezi

  • Je umesha mshauri mwamini mpya?
  • Iwapo la kwa nini?
  • Je, uliwafundisha vipi? Tambua mmojawapo wa vitabu au hoja ambayo ilijadiliwa.