
#10 Makaribisho
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #10, Makaribisho, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Wakati Mungu yu hai katika mioyo na mawazo yetu, tunatafuta uwepo wake kila wakati. Yohana asema hivi kwa njia ya ajabu katika kifungu cha kwanza cha injili yake. Anazungumzia maisha haya (1:4) ambayo yalikuja katika ulimwengu na anayatambua maisha haya na mwanga kuwa Yesu Kristo katika Yohana 1:14.
Mistari iliyotangulia inavutia ‘Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu’ (Yohana 1:12-13).
Wale ambao wampokeao ndio ambao Mungu aliwapa maisha mapya – Mungu aliwazaa upya katika roho yake na akaleta maisha mapya kuwepo.
Hawa ndio wale ambao humpokea au humkaribisha. Neno la Kigiriki lililotumiwa hapa ni sawa na mwenyeji ambaye humsalimu na kukaribisha mgeni nyumbani kwake.

Ni tofauti iliyoje kati ya mtu awakaribishaye na kuwatumbuiza wageni na yule hata hatambui uwepo wa wageni. Mungu haishi tu karibu nasi kama kawi au nguvu. Ni mtu na tunamkaribisha, twampendeza na kumfanya ajihisi nyumbani. Maisha ya wakristo shupavu yanapalilia uhusiano unaokua ndani ya Bwana kupitia kwa Roho.
Kufahamu uwepo wa Mungu kisha kufuatwa na moyo ambao hukaribisha na kumtafuta yeye. Maneno ‘kumtafuta yeye’ yanatumiwa mara nyingi katika maandiko lakini hayatambuliki. Nimetafakari kuhusu haya mara nyingi nikitafuta kupata maana na matokeo yako.
‘Kumtafuta Bwana kumeundwa kwa msingi kwamba Mungu yupo. Hapa ndipo imani yajitokeza kwa sababu hatumwoni. “Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao “(Waebrania 11:6). Imani ndio uti wa mgongo ya maisha ya Kikristo na maelezo muhimu ya maisha yake. Palipo imani, pana maisha. Pasipo imani, hamna maisha ya kiroho. Mungu alisema kumhusu mfalme Rehoboamu “Naye akatenda yaliyo maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute Bwana“(2 Mambo ya Nyakati 12:14).
Wakati mtu anapomtafuta Mungu, kutakuwapo sio tu ufahamu wa Mungu lakini hiyo hamu ya kumjua na kumpendeza. Kumtafuta kwetu ni kujieleza kwa hizo hisia ili kumjua yeye na mapenzi yake. Twataka kumjua yeye na kujifunza njia zake. Twatamani kuwa karibu naye na kushiriki kwa yale anayoyatenda.
Mwenyeji mwema huwafanya wageni wake wajihisi wamekaribishwa. Mgeni huwa sehemu maisha ya mwenyeji na nyumba yake kwa muda huo. Kwa mwamini mkristo uhusiano huu wa kibafsi na Mungu hauishi. Baada ya Yesu Kristo kuingia katika maisha ya mwamini huendelea kutafuta inamaanisha nini kuwa na mgeni, na kuendelea kuishi na mgeni maalum katika maisha yake.
- Hapo mwanzo mwamini humkaribishi tu Yesu maishani mwake, (yaani wokuvu) lakini maishani mwake mwote, huendelea kuimarisha ufahamu wa Kristo Yesu ambaye sasa yuashi ndani yake.
- Imani hutokana na hali hiyo mpya ambayo Mungu hutupatia. Imani inayokuwa inawakilisha kutambua na kukaribisha uwepo wa Mungu na kazi yake katika maisha yetu.
Tafakari Na Kariri
- Waebrania 11:6
- Yohana 1:12-13
Zoezi
- Yarudishe mawazo yako wakati ule wa kwanza ambapo Mungu aliuufungua moyo wako kumwelekea. Waza kuhusu Yohana 1: 12-13 na kisha baadaye jinsi ulivyomfungulia roho yako.
- Tafuta katika Biblia kifungu hiki cha maneno “Kumtafuta Bwana”.
- Waza kuhusu wiki iliyopita. Ni kwa njia zipi, umemtafuta Bwana. Imekuwa ya umuhimu upi kwako?
Sio sana ……… kidogo ………….. zaidi? …………….. Eleza.