
#7 Mwanzo wa Maisha
Mwanzo wa Maisha
Muhtasari: Kifungu #7, Mwanzo wa Maisha, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Maisha ya kiroho basi kama vile maisha ya kawaida ni msukumo wa nguvu zinazodumu katika maisha ya kila mwamini mkristo. Ukiisha kutambua maisha mapya huanza kujidhihirisha kupitia njia tofauti.
Maisha haya ni kama vile maji ya mto mkubwa yanakutanika na kuelekezwa. Nguvu hizi za maisha hauelezi kwa mfano, kuwazia wengine mabaya. Hii ni kwa sababu mwanzo wa nguvu hizi ni Roho Mtakatifu, Mungu mwenyewe kuzaliwa ndani yetu.
Yesu asema kwamba tumezaliwa mara ya pili au kuzaliwa kutoka juu. “Yesu akajibu, Amini amini nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu“(Yohana 3:5-6). Nguvu zetu mpya zatokana na Mungu mwenyewe. Maisha haya mapya basi ni sawa na Roho Mtakatifu aishiye maisha yake ndani yetu. Hii ndio sababu mara nyingi maandiko huashiria mwamini kuwa ana ‘maisha mapya ya kiroho’au roho (kutokana na neno sawa na kigiriki katika Biblia).
Roho Wa Mungu Akifanya Kazi Ndani Yetu
Ufahamu huu ni muhimu kwa sababu kwa njia hiyo tunaona njia tofauti ambazo Roho wa Mungu hutusaidia kila wakati. Anataka kutufanya kama Baba, kwa hivyo anatumia nguvu zake kutufuatilia kwa malengo haya. (Hizi sio nguvu za kutumika mbali ni Mungu mwenyewe). Vile vile Roho hatumii nguvu zake kutusababisha kutenda mabaya, maovu au kitu kingine kinyume na kusudi lake nzuri na takatifu. kisha kwa imani kuyatekeleza.
Nguvu za Roho ni kuu. Hatuwezi kuzifuga (yaani yeye) au kwa mafikirio kumbana nazo, ingawa tunaweza mhuzunisha (Waefeso 4:30). Matumaini yetu mema, kama vile chelezo, ni kuweka nguvu zetu zote katika kusalia imara katika mkondo wa Roho aliye mkuu.
Somo
- Roho Mtakatifu ndiye chanzo cha nguvu za maisha mapya, akituhimiza na kutupa nguvu kuyatenda yote yale Mungu anayopenda.
- Hatuhitaji kuwa wenye nguvu. Sisi ni kama waelekezi wa chelezo na twahitaji kuendelea na kutenda yale Roho wa Mungu ayataka katika maisha yetu.
Kariri Na Tafakari
- Yohana 3:5-6
- 1 Yohana 5:1,4
Zoezi
- Taja mambo matatu ambayo Roho mtakatifu anataka uyafanye
- Sema ombi kwa Mungu. Mshukuru yeye kwa kukupa nia ya kumpendeza yeye, na kuyatenda mambo haya. Muulize Mungu