
#26 Kuziba Pengo
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #26, Kuziba Pengo, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Elimu ya magharibi huweka imani yao kwa elimu. Wakristo lazima wapinge mpangilio huu wa elimu na hasa elimu ya dini. Tumeitwa na mwito mkuu kuziachilia nguvu za neno la Mungu kwa maisha ya watu.
Pengo la mafundisho kati ya theologia na huduma inayofaa bado ni kubwa. Wale wanaohitimu hawako tayari kamwe kwa yale yaliyo mbele yao.
Suluhisho la walimwengu kwa swali hili ni kuhitaji elimu zaidi. Shahada za uzamili na uzamifu sasa zapatikana kwa urahisi lakini lile wazo kwamba elimu pekee ndiyo inayohitajika bado halijabadilika.
Bila shaka, mengi yaweshatajwa kuhusu juhudi inayotumika kupata shahada hizi. Nidhamu ya mtu binafsi pekee ni zawadi kubwa, lakini ni vyema kuyaacha hayo na kutazama nyuma ya pazia. Je tunawauliza wanafunzi wetu iwapo wako tayari kwa maisha na huduma? Mara nyingi hawako tayari.
Mtazamo wetu wa elimu unasadiki kwamba mtu akiwa na ufahamu ulio sawa, ataweza kufanya mambo makuu. Hii inatokana na ubinadamu. Ufahamu ni sehemu ya mpangilio, na wala sio sehemu yote. Kunayo mambo muhimu zaidi, yakiwemo uundaji wa kiroho ambao ni lazima utekelezwe katika maisha ya wakristo.
Matumaini ndani ya ufahamu mara nyingi hututenganisha na watu baada ya kutuunganisha. Kukomaa kiroho kunalinganishwa vibaya na mafunzo ya kitheologia, lakini sivyo ilivyo. Wakati tunakutilia mkazo ufahamu, basi kuna wakati mfupi wa kukuza moyo na taaluma za huduma ili kuishi maisha ya utawa yanayotaa na kutumika vyema. Kwa mfano, twajifunza kuhusu shutuma za hali ya juu lakini tuna wakati mchache kujifunza jinsi ya kumruhusu Mungu atusameshe kupitia kwa neno lake ili tuwafunze wengine. haya bila shaka yanajumilisha nusu ya wasomi wote wanaoiaga huduma baada ya miaka mitano.
Kwa Nini Kuanguka?
Kwa nini kuna kuchanganyikiwa na kuporomoko? Ni kwa sababu neno la Mungu limeshindwa? Au yawezekana neno la Mungu halijapenya mioyo yetu? Au hatujapokea mafundisho yanayohitajika ili kuweza kuhudumu katika makanisani?
Mtume Paulo alimalizia sababu ya imani hii ndogo ni kwamba neno la Mungu halijapenya katika masikio ya msikilizaji. Fumbo la mpanzi, hata hivyo, Yesu analeta wazo hili kwa undani zaidi. Anasema kwamba watu wa Mungu hawajifunzi vyema kwa sababu mioyo yao haiku tayari.
Na je tukibadilisha mtazamo wetu ili kuandaa mioyo ya wanafunzi hawa ili wakaweze kulipokea vyema neno la Mungu badala ya kusoma tu kama zoezi au kusoma tu yale watu wengine wasema kuihusu Biblia.
Wakati wa masomo yale, Profesa mmoja wa agano la kale aliliambia darasa langu “Huu huenda ukawa ndio wakati wa kipekee utasoma agano la kale maishani mwako”.
Waza yale aliyokuwa akifunza darasa.
- Agano la kale sio muhimu.
- Agano la kale haitakuwa na umuhimu maishani mwetu.
- Hautahitaji kusoma agano la kale tena baada ya kulisoma mara moja.
Labda alikuwa akitaja kitu kuhusu imani yake binafsi bila kunuia. Bila shaka, mambo yaliyonukuliwa hapo juu sio ya kweli mbali ni mtazamo wa maandiko ambao umekosa imani. Ijapokuwa hakusema hayo moja kwa moja, yaonekana aliyaamini. “Hayahusu maisha yangu na wala sidhani mtaamini kwamba agano Wanafunzi wanaanza kuogopa kusoma Agano la kale; katika hali kama hii, hamna nafsi ya imani yao kukua. Profesa ajua kwamba somo hili ni muhimu kwa sababu wanafunzi wote lazima walisome ili waweze kuhitimu.
Baadhi ya Profesa hata hawaamini kuwa agano la kale ni la kutegemewa (kinyume na inavyoonekana). Waisomesha kana kwamba wanaikashifu, wakiidunisha imani ya wanafunzi wao. Profesa wengine wanaamini ni la kuaminiwa, kama Yule niliyemtaja, lakini hakuamini linahusiana wo wote na maisha na huduma yao.
Mambo kama haya hutokea kila mara mchungaji anapohubiri injili, badala yeye kuwa amebadilishwa kwanza na neno la ukweli. Mhubiri anakosa imani kwamba kifungu chahusiana na maisha yake.
Imani Tele
Yesu alifunza agano la kale kwa njia tofauti kabisa. Aliishi maisha ya utawa kutokana na agano la kale pekee. Alinukulu kutoka Agano la kale alipojaribiwa na imani yake kwa neno la Mungu ilimlinda. Alifahamu yale Mungu Baba alikuwa nayo kwa maisha yake kupitia agano la kale.
“Na baada ya kufunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” (Mathayo 4: 2-4).
Umuhimu wa kuchunguza tena njia za kujifunza yaliyomo haujakuwa muhimu kipita hivi sasa. Mwalimu lazima aende zaidi kusomesha yaliyomo na kushughulikia imani inayohitajika ili kuimarisha imani ya wanafunzi katika eneo fulani. Imani hii inahusiana moja kwa moja na kupata malengo ya Mungu aliyo nayo kwetu.
Mungu akitimiza malengo yake.
Iwapo tutaenda kupata ufanisi kwa kuzibua kusudi na nguvu za maisha za Mungu, lazima tupinge wazo kwamba ufahamu pekee unaweza suluhisa shida. Twahitaji neno la Mungu likitenda kazi katika maisha yetu.
Wanafunzi wengi wanahitimu kutoka shule na vyuo vya Biblia wakitegemea ufahamu wao badala ya Mungu. Kwa nasaha nzuri, Mungu anaweza na anatenda kazi kupitia mifumo yetu na anafanya kazi kupitia kwao, lakini ingekuaje iwapo tungetarajia wanafunzi wabadilishwe ili kutenda na kuhudumu kama Yesu? Bwana wetu aliye mbinguni anatungojea tupate mafundisho yetu vyema kwa ajili ya kondoo wake na utukufu wa jina lake.
- Na je kama wanafunzi wetu wangeweza kujifunza jinsi ya kuondoka taratibu kutoka shule hadi kwenye huduma? (Je ingewagharimu ni kuhusu ufahamu, ujuzi, kujitolea, tabia n.k).
- Au katika mazingira ya kanisa, ni nini kingetokea iwapo watu wa Mungu wangekua kwa kweli hadi kutikia kukomaa kabisa? (Nia nini kingehitajika kutekelezwa kanisani ili kufikisha watu hapo).
Tunatarajia mambo machache kutoka kwa wanafunzi wetu na neno la Mungu kwa sababu sisi walimu tunayo imani haba. Yesu bila shaka alikuwa na imani kubwa kwenye neno la Mungu hasa agano la kale “Imeandikwa…….” Hoja ni Mungu alisema na neno lake bado lina nguvu hata leo.
Somo
- Kutumaini ufahamu kunachanganya malengo yetu ya mafundisho, mafundisho yenye utaratibu na yasiyo na utaratibu.
- Imani ya mwalimu hushawishi mafunzo na imani ya wanafunzi, kwa wema au ubaya.
Tafakari Na Kariri
- Mathayo 4:4
Zoezi
- Hebu chukua masomo mawili ya Biblia yanayohusiana, ya hivi majunzi au ya kale kisha eleza ni nini shabaha ya masomo hayo (waza kuhusu vyuo vya Biblia, shule za jumapili n.k).
- Walimu walimiki imani ya namna ipi kuhusu kiini cha habari hiyo?
- Je madarasa haya yalikusaidia vipi au kukudhuru?