
#15 Mtoto Mchanga
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #15, Mtoto Mchanga, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Ahadi za kukua kiroho zimefichwa katika maelezo ni yapi yatakayotendeka katika kila hatua ya maisha ya Mkristo. Katika kifungu hiki, tutaangazia ahadi za Mungu anazozitoa kwa mwamini mpya – mtoto mchanga.
Kila mmoja wetu aliyaanza maisha yake kama mtoto mchanga, akakua katika miaka yake ya kubaleghe na kisha, utu uzima, nikitumai kwamba msomaji ni mtu mzima. Umri ambao mtu yuavuka kutoka hatua hadi nyingine sio dhahiri lakini utaratibu umedhihirishwa.
Kunazo ishara mbili muhimu za kutusaidia kuweza kufuatilia ukuaji wetu. Ya kwanza ni tunapozaliwa, na sherehe zinaanza. Mtoto mchanga ameingia duniani. Wazazi wenye furaha hutuma picha na kutangaza kuhusu tunu lao jipya.
Ishara ya pili iliyodhahiri ni wakati mtu anapokua. Kwa maneno ya Yohana wa kwanza, kuwa Baba. Yule ambaye awali alikuwa mtoto mchanga sasa amekua kabisa na anaye mtoto wake mwenyewe. Na duara sasa imekamilika, kizazi kimoja kuzaa kingine.

kuwa mzee na huru, bila mategemeo ya uzazi na majukumu muhimu
yanayotungamana nao. Kwa bahati mbaya, kanisa kwa njia nyingi
limekubaliana na mawazo haya. Hii huacha kanisa na jamii katika mashaka
kwa sababu waamini wengi waliokomaa hawawajibiki kwa kuwafundisha
waamini wachanga.
Mzunguko kamili hutokea mara tu mtu anapokuwa mzima na pia kuzaa
tunda na kuchukua jukumu kwa ajili ya kizazi kijacho.
Somo hili la sasa huangazia hatua hii ya kwanza muhimu ambapo maisha huanza. Yohana mwanafunzi hutumia mfano wetu kuendelea katika familia ya kawaida ili kutusaidia kuelewa kukua kwetu katika familia ya Mungu ya kiroho. Kama vile Yesu hutumia jambo lijulikanalo ili kufunza lile lisilojulikana. Katika vifungu vilivyopita tulizungumzia umuhimu wa maisha mapya ya kiroho. Mwamini ana maisha mapya na hivyo amefananishwa na mtoto mchanga.
Mtoto Hukua
Kama vile mtoto mchanga lazima akue kupitia hatua za maendeleo ya
kawaida- kutambaa, kuketi na kadhalika, vivyo ndivyo Mungu humfanya mwamini mpya kujifunza masomo ya msingi katika hatua yake ya kwanza ya kukua kiroho. Hatua za maisha ni muhimu kwa sababu katika kila hatua, mtu hujifunza na kukua katika njia nyingine tofauti.

Rebeka, binti yangu menye umri wa miaka kumi, juma lililopita alinishawishi nimchukue yeye pamoja na kakake, aliye sasa miaka kumi na mitatu, kuwapeleka uwanjani. Walitaka niwapeleke katika mbuga fulani ili kucheza kwa maana ilikuwa na kumbukumbu za kuvutia kutoka miaka ya hapo awali. Hivyo sote watatu tukaenda. Baada ya kucheza kwa dakika tano au kumi hivi, waliamua kwamba haivutii tena. Niliwasikia wakisema, “Nadhani kwamba tumekuwa wakubwa kuchezea hapa sasa”. Badala yake waliamua kutembea Yule mtoto mchanga sasa ameshamjua Bwana. Huyu awezakuwa mtu mwenye umri wa miaka hamsini lakini haijalishi. Kuzaliwa kiroho kunamwingiza kila mwamini katika familia ya Mungu kama mwanachama mpya.
Waamini walio wazee kiasi ndani ya Kristo wapaswa kupitia hatua hii ya kwanza kwa haraka kiasi lakini ni vyema kukumbuka kwamba bado watahitaji kupitia hatua hii ya msingi. Isipotunzwa vyema, kuna uwezekano finyu kwamba hawatakuwa vyema katika maisha ya kiroho.
Kuwalea Waamini Wapya
Je, mara ya kwanza unapokuwa mwamini ulitunzwa vipi?. Je, kuna mtu aliyekushughilikia kibinafsi? Maswali haya yawezaonekana kana kwamba hayana umuhimu wa wote lakini sivyo. Hebu angalia hali ya kushughulikiwa kwa huyo mtoto mdogo baada ya kuzaliwa. Ni wakati kama huu ambapo watu hasa wazazi humshughulikia yule mtoto mapenzi ya moja kwa moja.
Mtoto sio tu anyonyeshwe lakini pia hupendwa, huoshwa, na kadhalika. Utaratibu huu waweza onekana ni wa kuchosha na marudio, hasa wakati wa usiku, lakini ni muhimu. Lakini hebu tazama yale yanayoendelea karibu na mama, mtoto yuna nafasi ya kusikia maneno ya kupendeza, sauti na hisia hupatikana. Mtoto sio tu anajifunza jinsi ya kujibu na kuwasiliana, lakini kwa kukumbatiwa, kufurahiwa na michezo midogo, mtoto uhisi kupendwa.
Ni yapi hutendeka wakati mtoto ni mwoga na kuanza kulia? Mama
humkimbilia mtoto huku akimkumbatia husema “Pole, nyote sasa ni sawa. Mama yuko nawe.”
Mtoto sio tu anapokea chakula na mapenzi anayohitaji mbali pia na muhimu zaidi anapata mapenzi. Hii ndio hali ya kawaida. Kwa upande mwingine, kama mama hayupo na hashughuliki matokeo yake yake ni mtoto ambaye ujihisi hapendwi. Mungu hupitisha mapenzi, kushughulikiwa, malezi haya kwa msingi wa huyo mwamini mya utakuwa dhaifu.
Mengi Ya Kujifunza
Mwamini ana mengi ya kujifunza. Petro pia anatumia mfano kutusaidia kuelewa waamini wapya. Anatumia watoto wachanga ili kutusaidia kuelewa jinsi mwamini mpya hupenda kupata neno la Mungu. Anaufananisha na maziwa ya mwamini.
“Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwamba mpate kuukulia wokovu” (1 Petro 2:2).
Hamna jambo lolote linalolinganishwa na hamu ya mtoto mchanga kutaka kula. Mtoto atalia na kulia hadi maziwa ya mama yatakapofika kinywani mwake. Lakini mtoto anapoanza kunyonya na kuhisi utamu wa hayo maziwa huanza kuridhika (huja pamoja na ishara nyingine za kuvutia na sauti nyinginezo). Mambo hayo ni kweli kwa mwamini mpya. Mtoto mchanga ana hamu kuu kujua neno la Mungu. Hivyo lazima tuwepo pale ‘kuwalisha’ neno lake ili wakaweze kukua.
Maisha huanza kwa kuzaliwa upya kiroho (kunakoitwa kuzaliwa mara ya pili katika lugha ya kithiologia). Kukua hutendeka wakati mwamini anapopata neno la Mungu kama vile mtoto mchanga apokeapo lishe bora.
Haja hii ya neno la Mungu itakuwa kweli katika maisha yetu yote. Twahitaji kula ili tuishi, lakini kuna jambo hubadilika tunapozidi kukua. Siku za mwanzo za maisha, lishe bora imo ndani ya maziwa na lazima ipeanwe na mama. Mungu alikusudia iwe hivyo ili kuongeza uhusiano. Wakati mama anamnyonyesha mtoto iwe kwa matiti au chupa, wote mama na mtoto huwa wanaangaliana.
Tunapowaza kuhusu maisha mapya ya kiroho, kanuni fulani za kumsingi hujitokeza: uhusiano, kufunganishwa, upendo, neno la Mungu, malezi, na Kwa miaka mingi, kanisa limekuwa na mtazamo mwema wa kuwaleta watu kwa ufalme wa Mungu, lakini wengi wa hawa watoto wapya hupata mshutuko utokanao na kuzaliwa. Hawakupokea malezi waliyoyahitaji kwa sababu wao pia hawakutunzwa na kulelewa na waamini wengine. Mtoto hawezi jilisha binafsi na vile vile hata mwamini mpya. Anastahili kulishwa na baadaye tu akiisha kukua ndipo atajifunza jinsi ya kujilisha mwenyewe.
Ijapokuwa twaweza kuwa twajua kanuni hizi, shida ni kwamba sisi kama kanisa hatujakuwa waaminifu kutekeleza yale tunayoyajua. Na hivyo mwili wa Kristo umepata majuto makubwa. Mara kwa mara huwauliza waamini “Ni wangapi miongoni mwenu mlilelewa na kufundishwa mlipokuwa waamini wapya?” ni wachache hukubali.
Moyo wa Mungu lazima uwe umevunjika kwa sababu ya ukosefu wa malezi kwa watoto wake wenye dhamana. Kwa nini mioyo yetu haivunjiki vile vile? Kwa nini kanisa halitubu kwa ajili ya kutowekeza kwa ajili ya kizazi kijacho?
Somo
- Mfuasi mpya wa Yesu Kristo anafananishwa na mtoto mchanga, kwa sababu mahitaji yake yanaweza tu kutimizwa na mlezi.
- Mungu anahitaji tuwatunze waamini wapya kama vile mama kwa upole na utulivu humtunza mtoto wake mdogo.
- Mungu huwafunza waamini wapya ukweli wa kimsingi kutoka neno la Mungu katika hatua za kwanza ili kufanikisha ukuaji.
- Bwana anataka mtoto huyo mdogo wa Mungu ahisi upendo wake na malezi yake kupitia uangalifu wa kibinafsi na anamfanya mwanafunzi.
- 1 Petro 2:2
Zoezi
- Je wewe ulifundishwa kama mwamini mpya. Eleza ni yapi yalitendeka au hayakutendeka.
- Je, unawashughulikia vipi waamini wanakuzunguka? Je unawafundisha? Kwa nini au kwa nini hufanyi hivyo.
- Iwapo hukufundishwa hapo awali, ni nini unahisi ulipoteza? Iwapo ulifundishwa, ni nini ulinufaika nayo?