Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#20 Kiini Cha Maisha

Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #20, Kiini Cha Maisha, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Wanadamu wengi wanaishi bila kuzingatia kwa kina vilivyomo chini ya ardhi.

Hata hivyo, huenda baadhi ya wanadamu hulipa suala hilo uzito wanaposhangazwa na yanayoibuka kutoka ardhini kunapozuka vimbunga au tetemeko la ardhi.

Maisha yetu ya Kikristo yanaweza kulinganishwa na hali hiyo; Wakristo wengi wanaishi bila kujua yaliyomo kwenye maisha yao ya Kikristo. Japo mengi yametafitiwa na kuandikwa kuhusu masuala ya utakaso, wengi wanaishi kwa mapuuza kuhusu masuala muhimu zaidi katika maisha ya kiroho.

Awali katika kitabu hiki, uwezo wa maisha ya mtu anayeongozwa na roho mtakatifu uliangaziwa kwa kina. Maisha sio suala la kijumla bali linazingatia zaidi maisha ya mtu binafsi, nia na kusudi lake maishani. Iwapo binadamu ataishi katika maisha yanayoongozwa na roho mtakatifu, basi uwezo wa maisha yake utahisiwa na kueleweka zaidi.

Kiini Cha Maisha illustration from page 111

Wakristo wanapoishi bila kuzingatia kusudi la roho mtakatifu, maisha yao hutawaliwa na kuchanganyikiwa katika masuala mbalimbali, hali ambayo huwafanya kuishi maisha yasiyoambatana na maelekezo ya roho mtakatifu. Kuna makundi mengi yanayohusishwa na Ukristo na yanayotambua utendakazi wa roho mtakatifu ambayo hayana ujuzi wowote wa kikweli kuhusu roho mtakatifu au kusudi la Mola licha ya kujihusisha na kujazwa kwa roho mtakatifu.

Sio sadfa kwamba Mtume Petro aliweka kifungu cha 1 Wakorintho

kinachozungumzia Upendo kati ya sura za 12 na 14 za kitabu hicho zinazongumzia karama za roho mtakatifu. Karama/vipaji hizi ni muhimu la sivyo hazingetajwa kwenye biblia. Hata hivyo, Petro alitilia maanani mstari

Kuzingatia Masuala ya Moyo

Mambo ambayo Mola hutekeleza maishani mwetu kupitia roho wake na kututakasa tufanane na Kristo hushiria kusudi kuu la Roho Mtakatifu. Vipaji bila kuwepo kwa mwongozo war oho mtakatifu havifai.

Matendo ya roho mtakatifu maishani mwetu ndiyo nimeyaita “Kiini Kikuu cha Maisha,” kwa kuwa ndiyo hudhihirisha kilichoko mioyoni mwa Wakristo. Roho Mtakatifu huleta uhai na kumfanya Mkristo kung’aa. Roho Mtakatifu huwapa Wakristo vipaji na hakomei hapo, kwani humpa Mkristo kichocheo kutamani kuishi maisha yanayozingatia Imani kwa Mola.

“Akija Yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wak mwenyewe bali atanena yote atakayosikia.

Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo” (Yohana 16:13).

Ni jambo la kuvunja moyo kwamba tunaweza kujua kuhusu Roho Mtakatifu bila kumfanya yeye kuongoza maisha yetu.

Huu ni mojawapo ya mapungufu ya mfumo wetu wa elimu ambapo tunapata ujuzi kuhusu mambo mengi bila kuyatilia maanani maishani mwetu. Upepo unaweza kuvuma na tukakosa kujua unakoelekea. Kinyume cha hayo pia kinaweza kutendeka, watu wanaweza kujazwa na Roho na wakafanya miujiza bila wao kuelewa kusudi lake maishani mwao. Huo ni ujinga na mapuuza. Kuishi bila kusadiki kusudi la Kiungu la Roho Mtakatifu ni Kutotii. Baadhi hujua ni yapi Roho Mtakatifu anawataka kufanya lakini wanapuuza na kukosa kuyafanya namna wanavyotakiwa na Roho. Mfalme Sauli ni mfano wa waliofanya mioyo yao migumu kwa kutotii maelelkezo ya Roho wa Mola na kufanya kinyume cha maagizo licha kuwa na fursa chungu nzima za kujifunza kutokana na maelekezo ya Roho. kutumikia wengine bila kulalamika Je, huwa tunatakeleza kwa kasi yale ambayo Mola anatuelekeza kutekeleza?

Majibu Mawili Kwa Mungu

Tunapobaini yale ambayo Mola anatekeleza maishani mwetu kupitia Roho wake Mtakatifu inakuwa inakuwa fahari na rahisi kwetu kuziweka nafsi zetu kuambatana na kusudi lake.

VIELELEZO 2: Uhusiano Wa Roho Mtakatifu Na Mkristo

Katika sehemu ya kwanza ya mchoro, hapo juu, ni bayana namna ugumu wa moyo na mapuuza unaweza kuwa kizingiti cha uhusiano mwema kati ya Roho Mtakatifu na Mkristo. Katika sehemu ya pili ya Mchoro upande wa kulia, Mkristo anajazwa na Roho Mtakatifu baada ya kizingiti kuondolewa na Roho Mtakatifu kuruhusiwa kutiririka hadi kwenye nafsi ya mkristo. Hiyo ndiyo maana kamili ya “kujazwa na Roho Mtakatifu,’ na kuishi maisha yanayoshawishiwa na Roho.

Somo

  • Wakristo wengi wanaishi kwa kupuuza utendakazi wa Roho Mtakatifu maishani mwao na hiyo wanatilia shaka kazi yake kwa kuwa hawaifahamu.
  • Mkristo anapokosa kufanya anavyoagizwa na Roho Mtakatifu, anakuwa na hali ya ugumu wa moyo katika masuala ya kiroho
  • Tunapobainisha namna Mola anavyotimiza kusudi la utakaso maishani mwetu kupitia Roho Mtakatifu, tunaimarika katika maisha yetu kiroho na kuelewa zaidi namna ya kuishi maisha ya kiroho.
  • Hili ndilo tunda la mwamini (pia liitwalo kazi nzuri).

Tafakari Na Kukariri

  • Yohana 16:13
  • Soma Yohana 16:5-15. Nakili/andika yanayojitokeza kuhusu

Roho Mtakatifu.

  • Wazia wakati wowote karibuni ambapo nafsi yako ilikuwa na

mvutano na ushawishi wa Roho Mtakatifu akikutaka kufanya au kukosa kufanya jambo. Ilihusu nini na uliishughulikiaje?