Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#3 Mabadiliko Lazima Yaje

Mwanzo wa Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #3, Mabadiliko Lazima Yaje, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Mabadiliko hutufanya kutotulia kwa hivyo hupendezwa kuyapinga. Mhadhiri mmoja alinilalamikia kwamba shule hii inawalazimisha waadhiri wote kutumia tarakanishi. Mabadiliko hayo ni madogo, hata hivyo, ukilinganisha na changamoto halisi zinazolikumba kanisa, kusalia kwake kumo hatarini.

Kukua au kufa. Kuwa washindi au kushindwa. Haya ni maamuzi yetu. Kila mahali kutuzunguka, kanisa, lina wasiwasi. Kwa wakati mmoja ilikuwa kwamba kanisa lenye fadhili lilikuwa linakwisha, lakini sasa pia kanisa la injili. Hili lawezekanaje? Ulimwengu huko nje hudhani kwamba ujumbe hauna maana na dhaifu, lakini twaeza walaumu? Mara kanisa linapoweka kando imani yake ndani ya Yesu, linakosa kufaa. Nguvu zake zinapotea.

Mitandao ya habari imeongeza kasi kwa kututupia habari chungu nzima, ikikanganya macho yetu na mawazo yetu. Je Mungu ameifungua mafuriko haya ya ufahamu ili kuharakisha uenezaji wa ukweli wake? Bila shaka amefanya hivyo, lakini wakati huo huo naye adui anatumia vifaa pia kwa mipango yake miovu.

Hata hivyo, hatupaswi kuhisi tumelemewa. Mungu yuko kutusaidia. Haijalishi adui atatumia silaha gani kupigana nazo. Ingawa mbinu za shetani za kupingana na watu wa Mungu zaweza kubadilika, maarifa yake ni yale yale.

Uwezo wa Mungu kuwasaidia watu wake bado wadumu.

Hata ingawa kanisa la kwanza lilikuwa limetawanyika likikimbia kila upande,

kama vile chungu wakitafuta kichunguu kilichoporomoka. Mungu bado

alikuwa pamoja nao bila kuwaacha kamwe. (Matendo ya Mitume 11:19)

Je, Mungu alikuwa analichunga kanisa? Bila shaka. Alitumia unyanyasaji wa wakati huo ili kueneza neno lake kwa haraka kupitia kwa kanisa. Mateso yalitumka kwa ajili ya kusudi kuu. Ni nini twapata katika Matendo ya Mitume 13? Kanisa kwa sehemu moja, wanafunzi wake waliokuwa wametawanyika, ambalo lilikuwa limeundwa na tayari kwa kudumu duniani.

“Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao” (Matendo ya Mitume 13:1-3).

Baadhi ya watu wa Mungu wanakumbana na mateso kwa hila au ya wazi kama ilivyo katika Matendo ya Mitume 13. Mmoja wa wachungaji wangu katika nchi moja kusini mwa Asia, hupata ishara mara kwa mara, vitisho vilivyofichwa kuyahusu maisha yake, ili aache kusambaza vijikaratasi vya dini.

Wengine, ijapo wanakumbana na vitisho visivyofaa. Kanisa linaendelea na kama awali lakini havina ushawishi ule ule. Hata michezo midigo ya mpira huwatenga watu wa Mungu mbali na kuabudu.

Kutafuta Suluhisho

Kuna mazoea ya kufanya ibada zetu za kuabudu ziwe fupi. Twasema kuwa ni za watafutaji, lakini ukweli ni kwamba watu wa Mungu wapendezwa pia.

Mungu umekwisha kwa sababu hatuoni jinsi linatusaidia katika maisha yetu.

Hamna kitu kwa kweli kimebadilika. Hata hivyo, neno la Mungu laweza zungumza kwa nguvu na kizazi cho chote na tamaduni ye yote au dini ye yote ulimwenguni hata kwa mawazo ya siku zijazo. Mbinu zetu za kale za kulisha na kuchunga makanisa hazifai kwani mashambulizi ya mawazo ya kidunia yamewakumba watu wa Mungu.

Swali ni, “Tutayabadili mambo vipi? Ratiba mpya? Endeleza masomo? Haya yote yamechelewa na ni ya pole mno. Kufika hapo, watu wa Mungu duniani kote wanateseka kwa kukosa nguvu za ukweli kung’aa kutoka kwa maisha yao yaliyo ridhiana. Hebu tazama ndoa ya kawaida. Unaona mapenzi ya Mungu, malezi na mapatano? Ninawafunza wachungaji duniani kote, hata kuwasomesha mambo ya ndoa. Wachungaji na washiriki hadithi ni moja. Wengi wa ndoa zilizoharibika na wanakumbana na shida nyingi.

Kutambua Shida Ya Msingi

Nimeona Roho wa Mungu akiokoa vikundi vya watu katika tamaduni kadhaa lakini kizazi kinachofuata wamo na nia na hukataa kupinga shida za chuki na hasira ambazo hazijamalizwa vyema na upendo wa Mungu ukifanya kazi katika maisha ya wazazi wao. Wanaishia kupuuza yale ambayo wafunzwa. Huku ni kukataa kwa kizazi ambapo kiko hai wakati ukweli wa Kristo umetolewa lakini bado haujakubalika. (Waamuzi 1:2-3).

Ingawa sio kwa wingi kinyume cha miujiza na uponyaji, kutafuta kuwa na wimbi ligine lao halitatufikisha mahali tunaohitaji kuwa. Nimeshuhudia jinsi viongozi wengi wakuu waliokolewa kiajabu au kusaidiwa na Mungu kupitia njia za kipekee. Lakini hii haimaanishi, mara nyingi itawasaidia kuhusiana vyema na wake zao. Twahitaji kwenda zaidi ya kupata msaada kwa sehemu moja ya maisha yetu bali kuwa watu ambao kila sehemu ya maisha yetu yameguswa na uwepo mtakatifu wa Mungu. na yenye nguvu ya Kristo. Kutoamini ndio shida yetu ya msingi. Maarifa yetu binafsi hupenda kuunda mitazamo yetu. Kutokana na kushindwa kwetu kuishi maisha ya Kikristo yanayotosheleza, tunapoteza ujasiri na matumaini ya neno la Mungu. Kutoamini huongezeka. Kuvumilia kwa kanuni za chini na kupungua kwa matumaini kunaambatana na kutoamini huku.

Mabadiliko Yahitajika

Lazima tubalike au tusombwe zaidi na

ulimwengu. Ratiba mpya huleta mabadiliko machache lakini ni ya juu juu yakipuuza kukabiliana na shida halisi. Shida zile zile huendelea.

Tunawashangilia wale wachungaji, waalimu na wainjilisti ambao hufanyakazi zaidi.

Wanadhani, iwapo wataongea kwa sauti kubwa, au kuleta hisia za upendo, watu wa Mungu watasaidika. Hili halisaidii.

Wengine hupendezwa na hiari kama kubadilisha makanisa, madhehebu au hata watajaribu dini za mashariki kama fumbo la mawazo, yoga, na kadhalika.

Wanatumaini kwamba mambo haya yataleta yale wanayoyatafuta. Hayasaidii kwa sababu mambo hayo huelekeza watu mbali na chanzo za uzima – Yesu ndiye Kristo.

Barabara Ya Kurudi Nyumbani

Ni lazima tumrudie. Kutubu ndiyo njia ya kurudi kwa Mungu. “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kwakuwako kwake Bwana” (Matendo ya Mitume 3:19).

Uamsho ni kwa sababu ya kutubu kwa kweli kunako tendeka katika mioyo mingi kwa wakati mmoja na sehemu moja. Ni mabadiliko haya ya mtu binafsi ambayo yahitajika kuleta mabadiliko kamili ya tamaduni zetu. Usifikirie kuhusu wimbi katika bahari lililodhibitiwa katika ufuo mbali dhoruba iwezayo kuvunja njia asilia zinazokwamisha maisha yetu ya ‘Kikristo’.

Ijapokuwa kiwango cha dhabihu iliyotolewa ilikuwa ya kupendeza, kuwekwa wakfu kwa hekalu kulikuwa sherehe ya kipekee zaidi kwa sbabu ya maombi ya Suleimani kwa niaba ya watu wa Mungu. Twahitaji moyo amabao anatuongoza kwenda kwa madhabahu na kuomba kama Suleimani. “Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao” (2 Mambo ya Nyakati 7:13-14).

Hamna njia nyingine. Ni lazima kila mara turudi kwenye madhabahu mahali msamaha unaweza kupatikana. Haijalishi mambo yalikuwa mabaya kiasi gani, iwe ni ugonjwa, njaa au hata utumwa, iwapo Israeli iliyageukia madhabahu, Mungu alikuwa akisikia na kuponya. Chini ya agano jipya, madhabahu yetu ni Yesu Kristo ambaye anaweza kutusamehe na anatamani kuturejesha.

Matatizo yanayolikumba kanisa katika kizazi hiki sio madogo. Hatujaribu kuyadunisha na mistari ya Biblia. Badala yake, tunatumia ile imani ndogo tulionayo kuanza kuifungua mioyo yetu kutuleta mahali ambapo kushika tena mtazamo wa Mungu kwa yale yanayohitajika kufanywa.

Mungu hana woga wa uongezeko wa ufahamu. Anautumia! Mipango yake haiyumbiyumbi kwa mashambulizi ya shetani. Bwana huketi mbinguni na kuwacheka maadui zake (Zaburi 2). Twahitaji kuiandaa mioyo yetu kwa yale Mungu anataka kwa kunyenyekea, kuja kwa Bwana tukipiga magoti na kukiri Iwapo tutakuja kwake, basi atakuja na kutuonyesha jinsi kanisa linaweza kukabiliana na giza katika ulimwengu kupitia kwa mwanga wake.

Somo

Mungu hutumia mashambulizi ya kanisa kutusukuma pembeni ili kuvunja mitazamo yetu ya kale na kugundua nguvu za ukweli wa mtukufu.

  • Shida halisi ambayo kanisa hukumbana nayo ni kutoamini.
  • Mabadiliko huanza kwa kumrudia Mungu, kunyenyekeza mioyo yetu na kukiri dhambi zetu.
  • Watu wa Mungu lazima watende jambo la sivyo watapoteza hadhi mbele za maadui zetu.

Kariri Na Tafakari

  • 2 Mambo ya Nyakati 7:14
  • 2 Mambo ya Nyakati 6-7
  • Nehemia 1 (Kanda mpya)

Zoezi

  • Je, umehuzunishwa na dhambi inayokuzunguka au unakubali kwamba ndivyo mambo yalikusudiwa kuwa?
  • Kama Nehemia, njoo kwa madhabahu ya Mungu sio tu kwa dhambi zako za kupotea kwa roho na macho, lakini kwa watu wa Mungu jinsi bila sababu wametapatapa katika kushindwa na kukosa matumaini badala ya kuishi ndani ya uwezo wote wa Bwana.