Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#13 Kutafuta Mwelekeo

Mwanzo wa Maisha na Wewe

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #13, Kutafuta Mwelekeo, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.

Mungu ni mwenye juhudi kuishi ndani yetu ili kutusaidia tuwe kama Kristo.

Huu ni ukweli wa ajabu na wa kushangaza, lakini bado twaweza kuchanganyikiwa. (Yule mwovu hufanya kazi maradufu kuhakikisha tumechanganyikiwa). Waamini wanaweza kuwa wamekanganyikiwa kwamba yamaanisha nini kuishi maisha kama ya Kristo au pia waweza kwamba haiwezekani kamwe, jambo ambalo limehifadhiwa la mbinguni.

Wanakumbana na matatizo ya kila namna na hawajui jinsi ya kuyatatua. Labda waamini hawa, kwa mfano, hawajui jinsi ya kuyashughulikia mahusiano ya kibinafsi. Wapatwa na machungu na kuwakasirikia wengine. Kisha mwishowe watakuwa hawana upendo.

Maisha ya kiroho ya mwanadamu huendelea sawa na maisha yake ya kimwili. Bila shaka mna tofauti, lakini kwa ujumla usawa huo unaturuhusu kupata kuona maendeleo ya maisha ya kiroho, katika hatua tofauti ya maisha ya mkristo. Ulinganifu huu ni muhimu kwa sababu nina shida kufahamu kanuni Tunapomwona mtoto mdogo, hatuweki juu yao matarajio yanayoambatana na mtu mzima. Huo utakuwa ni mzaha. Watoto hata hawawezi kujilisha wenyewe! Haya yatafika, lakini itachukuwa muda. Na vivyo hivyo na maisha yetu ya kiroho.

Kiini Cha Maisha illustration from page 71

Yohana alitumia mifano ya maisha ya kawaida kutusaidia kuelewa kuwepo na pia kiini cha maisha ya kiroho. (Kama tulivyojadili kutoka Yohana kifungu cha 1, 3 na 5) Ametupa mfano mwingine wa kutusaidia unaofafanua maendeleo ya maisha yetu ya kiroho.

Katika 1 Yohana 2: 12-14. Yohana anatupa jawabu ya kuelewa hatua tatu za maisha ya kiroho. Hatua hivi tatu za maisha ni rahisi pia kwa undani kunapanua ufahamu wetu wa njia za maisha ya kiroho. Yale yanaonekana kuwa dhana iliyofichika, sasa huwa la kweli na dhahiri.

“Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi watoto, kwa sababu mmemjua Baba. Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemujua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu” (1 Yohana 2:12-14).

Mafungu haya “watoto”, “vijana” na “akina baba” ni mifano ya kawaida na yenye nguvu. Nimesikia watu wakiniuliza kana kwamba haya yanahusu kukua kiroho kwa sababu ya umuhimu wa kuendelea kimwili na miaka. Tunapotazama kwa makini kunayo maelezo yanayohusishwa na kila kitengo, hata hivyo Yohana anaashiria kwa tabia za kirohona sio za kawaida. “Mshindeni yule mwovu” na “neno la Mungu lidumu ndani yenu” yadhihirisha kwamba hayaashiria maisha ya kawaida lakini maisha ya kiroho.

Hatua Tatu Tu

Katika nyanja za maendeleo (kibayologia) kimawazo tumejifunza mengi kuhusu maendeleo ya kawaida. Kila mmoja wa hizi hatua tatu za maendeleo itatajwa kwa kifupi, lakini mwelekeo utakuwa jinsi zinavyoingiana na maisha ya kiroho kwa jumla. (Tunayo maelezo mengine ya kufundisha ambayo yametengwa ili kueleza na kutumia kila mmoja ya hatua hizi tatu).

Kiini Cha Maisha illustration from page 73

Nguvu za maisha ya kiroho zinazopatikana kwa Roho Mtakatifu bila shaka huwaongoza wafuasi wa Yesu Kristo kufikia mabadiliko hadi ukamilifu wa mfano wa Kristo.

Hatua hizi tatu hutusaidia kufananisha yale ambayo yanastahili kutendeka katika kila hatua. Tunaposaidia ukuaji huu, waamini watakuwa wenye nguvu.

Tunapoyatazama makanisa yetu leo, hatuwezi kulaumu neno la Mungu au Mungu mwenyewe kwa ghasia au kutokuwa na mwelekeo kanisani. Kanisa limepuuza jukumu lake la kuwafanya wanafunzi. Tumaini letu hata hivyo, ni wakati tutakapoacha mzaha na kutaka kuwa kama Kristo na kutii yale Kristo ametuamuru, kanisa tena litaanza kupata nguvu. Wafuasi wa Yesu kama vile wanafunzi wa kale, wataitenda kazi yake kwa upendo wake.

Mungu alichagua kutuhusisha na njia ya maendeleo haya katika mawazo yetu kwa kutumia taswira inayo eleweka kwa urahisi, ni kuturuhusu tukue katika familia ili zitushauri. Katika vifungu vinavyofuata, tutaangazia njia ambazo hatua hutusaidia ili kumsaidia mwamini, sisi wenyewe na wengine ili kukua.

Somo

  • Maendeleo ya kiroho ya waamini kwa njia nyingi ni sawa na maendeleo ya kawaida ya wanadamu.
  • Unyonge wa kanisa hauhusiani na ukosefu wa nguvu za injili au neno la Mungu lakini ni kushindwa kwa watu wa Mungu kuwajibika kufundisha walio karibu nao.
  • Kunazo hatua tatu za kuendelea kiroho: waamini wapya (watoto) waamini wa rika (vijana) na waamini waliokomaa (akina baba).

Tafakari Na Kariri

  • 1 Yohana 2:12-14

Zoezi

  • Soma 1 Yohana 2:12-14. Ni vikundi vipi vitatu unavyovipata? Angazia tofauti moja katika kila hatua ya kiroho na ya kawaida.
  • Je, unamfahamu mtu ye yote anayefunzwa? Iwapo la, wewe unadhani ni kwa sababu gani?