
#23 Sehemu ya Utimilifu
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #23, Sehemu ya Utimilifu, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Shida moja kuu ya kufundisha ni kutoweza kufahamu vyema jinsi malengo yote ya Mungu yatakavyotimizwa. Ramana ya Yohana kuhusu safari ya kiroho ya mwamini katika 1 Yohana 2:12-14 hata hivyo, inatupa yale yatupasayo kujua ili kutusaidia kuelewa ukuaji katika kila kiwango.
Mfano wa maisha, ukieleza chanzo, nguvu, mfumo wa msukumo wa maisha ni wa msaada mkubwa, lakini haitusadii kuyafikia malengo yanayoweza kupimika, ambayo twaweza kuyaelewa virahisi na kuwashauri wengi kufuatilia. Yohana hakutofautisha tu kiwango kimoja kwa kingine, lakini alitambua nyanja tofauti za ukuaji ambazo zitatokea katika kiwango fulani. Hayo yamekua malengo yetu makuu.
Malengo maalum ya kiroho ni sawa na ishara za kukua za mtoto mdogo.
Hatua za kwanza za kitoto kidogo au kuzungumza sentensi kamili ni ishara za kawaida za kukua kwa kawaida. Ishara hizi ni malengo yasiyokusudiwa kwani hatuwezi kuyabadili moja kwa moja. Jukumu la mzazi ni kutoa malezi ya kawaida na mazingira yanayofaa ili kukua.

Mtoto mmoja au wawili walichelewa kuanza. Kama wazazi tulianza kuwaza kama kuna jambo mbaya. Kwa nasaha nzuri hapakuwa jambo mbaya. Ilitulazimu kujifunza kwamba kila mtoto hukua katika kiwango tofauti.
Ingawa hatuwezi tenda lolote kuharakisha ukuaji huu, ishara hizi ni muhimu sana – yanatueleza kuwa mambo ni shwari.
Katika ulimwengu wa leo na kiwango chote cha utafiti, maafisa wa afya wanaweza mara kwa mara tambua iwapo mtoto haendelei vyema. Labda mtoto amepungukiwa na baadhi ya vyakula ili kukua vyema. Kuna chuguzi kadhaa. Vyakula hivyo vinaweza kuongezewa, au kusaidiwa kuundwa kwa zitafaulu.
Malengo Ya Kiroho
Hii ni hali sawa na mahitaji ya kiroho. Hatutengenezi mifumo lakini twatenda kazi nao. Tunaweka ujasiri wetu katika mfumo wa kiroho ambao Mungu aliweka. Hutenda kazi. Kukua kiroho hutendeka na maandiko yameweka ishara za kupima ukuaji wetu. Kama waalimu na wakufunzi walioteuliwa na Mungu, tunahimiza utaratibu huu wa ukuaji.
Malengo yetu yanakuwa ishara hizi za ukuaji sio kwa sababu tunawafanya watu kukua, lakini kwa sababu inatufanya kutambua yale Mungu anatenda na watu katika viwango tofauti vya ukuaji. Ili kuhimiza na kuchochea ukuaji unaofaa, tunaongezea kile kinachohitajika. Tambua mafundisho ya Paulo kuhusu malengo haya matatu.
“Lakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki” (1 Timotheo 1:5).
Yohana ametambua mambo kadhaa yanayostahili kutendeka katika kila
kiwango. Tunaweza ongezea mawazo haya kwa kutumia mifano ya kawaida. Mimi binafsi nimegundua mfano wa Yohana unaeleza ukweli kwa urahisi tena Kama mkufunzi, nimetafiti kwa mapana na marefu lakini bado sijapambanua kabisa makuu yaliyo katika kila kiwango cha kujifunza. Kama vile uchimbaji wa madini, mtu bado aweza chimba zaidi.
Mafundisho Makuu
Siri ya mafundisho makuu itategemea jinsi tutakavyo unganisha mambo haya mawili.
1. Ufasaha ambao tutaweza husisha sehemu zote za ukuaji kwa malengo yote ya Mungu ya ukuaji wa kiroho.
2. Malezi kabambe ya kiroho na mashauri yanayohitajika wakati wowote kwa mtu binafsi.
Waamini wanapata matatizo makubwa wanapokosa mafundisho yanayofaa.
Matatizo haya huongezeka tunapoona waamini walio walegevu wakianza kuenda mbali na Bwana.
Jambo lililo mbaya sana limekuwa likitendeka kanisani kwa muda sasa. Ninaamini ni kwa sababu hatua hizi mbili zilikosekana kanisani na hivyo waamini hawapati malezi bora.
Somo
- Taswira yote ya yale Mungu anatenda hutusaidia ili kuendelea kuyaweka mambo yote katika mtazamo unaofaa.
- Shida kuu katika mafundisho hutokea wakati tunapo tenganisha sehemu moja kutoka kwa utimilifu wote, malengo ya muda mfupi kutoka kwa yale ya muda mrefu (ambayo ni ya Mungu).
- 1 Timotheo 1:5
Zoezi
- Orodhesha majukumu yako makuu katika maisha, shule, kazi yako, na kadhalika.
- Ni nini malengo ya Mungu ya muda mrefu katika maisha yako hapa duniani? Ni vipi Mungu anataka wewe uendelee kukua kiroho ili kumtumikia?
- Je, umewahi kuhusisha maisha yako ya kiroho na malengo ya Mungu ya muda mrefu ili ukakue kiroho?