Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#31 Kuwashauri Waamini Wanaokomaa

Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #31, Kuwashauri Waamini Wanaokomaa, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Wanaokomaa

Mmojawapo za changamoto kubwa kuhusu kuwaza juu ya hatua hii ya tatu ya kukua kiroho iliyoelezwa na Yohana kama ‘Baba’, ni kwamba kitamaduni haifai kumweleza mtu au wengine kuwa ni waamini waliokomaa. Mawazo ya namna hii hudhihirisha unyenyekevu wa uongo na huwazuia watu kutopata mtazamo wa maisha kulingana na Biblia unahitajika. Je, wajua Baba ye yote ambaye hukana kuwa baba? “Ah, unafikiri hivyo. Lakini mimi bado sio baba?” Taswira hii ni ya kukanganya. (Hasa unapowaona vijana wake wakimvuta huku wakitaka kitu kutoka kwake). Kwani hali ya kuwa baba ni hatua ya kawaida ya maisha – hamna cha kuona haya.

Shida ya kiburi na mtego wa kudhani kwamba ‘tumeshafika’ ni shida kubwa kabisa, lakini tukitazama vyema hatua ya kuwa baba, tutatambua kwamba kuna njia mwafaka za kibiblia za kukabiliana nalo.

Kulinganisha ni tatizo la mwanadamu wa dhambi. Tabia ya mwanadamu ni kutaka kuwaza kwamba yeye ni bora kuliko wengine. Mtazamo wa Biblia ni kwamba: 1) Endelea kukubali kanuni na malengo ya Mungu.

2) Tuendelee kumtafuta Mungu ili atushauri na kutuongoza kwa utauwa.

3) Tufundishe ili tuweze kuwasaidia waliokaribu nasi vyema.

Je, waona utofauti? Endelea kutafuta kukua. Tunakubali kwamba tuna nafasi ya kukua na kukomaa zaidi. Tukizingatia kuwatumikia wengine, hatutapata wanaotuzingira ambao hawajapata kuwa baba ila wametegwa mahali njiani.

Yesu alisema ilikuwa vyema na busara kwa mtu kujidhani kuwa amekomaa. “Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke” (Marko 4:28).

Hatua hii ya mwisho ndipo twastahili kuzaa matunda. Kinyume ni msiba mkubwa kwamba maisha yetu hayazai tunda lo lote la utawa kwa sababu ya kujionea huruma. Pengine kwa kupoteza wakati ukitazama filamu au kucheza michezo. Hii pengine, hamna dhambi kuu kuliko kwa baba kupuuza mahitaji ya wanawe huku akitumia pesa zake na wakati wake kuponda mali. Hutendeka, lakini ni jambo la kuhuzunisha sana.

Katika hatua ya kwanza tuliona jinsi mtoto mchanga alivyokuwa akiwategemea wazai wake, hata kwa mahitaji ya msingi ya maisha. Kwa njia hiyo, twapata ni vyema kwamba kila mwamini akue ndani ya Kristo hadi kukomaa ambapo watawaongoza wengine kwa Kristo na kuwasaidia katika maisha ya kikristo iwapo hakuna mtu anashughulikia waamini wapya na wachanga, watapatapa katika imani yao. Hii ndio roho ya kuwa baba – kuwajali wale walio karibu nasi, na kwa kiasi kidogo wale tuliowaongoza kwa Kristo.

Katika hatua hii ya tatu ndipo tunapowafunza waamini jinsi ya kuwalea wengine. Ikiwemo hapa ni kukuza msingi wa kuhudumu, ni kufahamu jinsi ya kupalilia maisha yaliyo na uhusiano wa dhati na Mungu. Kama akina baba, waume kwa wake wa imani hukomaa katika mambo haya, hukuza viongozi ambao wako tayari kusimamia mahitaji ya kanisa kwa jumla, na pia kuwahudumia wale waamini wengine walio karibu nao.

Ninao watoto nane wenye umri wa miaka 22 kati ya aliyemchanga hadi aliyemkubwa. Sasa nina vijana wane wanaobaleghe, hali hii itaendelea kwa muda mrefu. Baadhi yao wanakaribia kuhitimu kutoka shule ya upili hali wengine bado hawajatulia katika maisha yao ya utu uzima. Hatumo mbioni, lakini twaomba kila wakati kwamba tutapata elimu inayofaa ambayo itaweza kupata kazi nzuri ili nao pia waweze kuzilea familia zao wenyewe. Kama wazazi twawatakia mema zaidi kuliko mtu mwingine ye yote.

Mungu kama ‘mzazi’ wetu pia anatutaka tukomae. Kukomaa kunaleta hali ya kuridhika kwa yale Mungu amekusudia kwa maisha yetu. Hatua ya tatu ya kuendelea kiroho sio kama kihindi ambapo aliye na roho nyingi hujitenga na familia yake na ulimwengu ‘halisi’ akiendeleza maisha yake yote akitafuta mwangaza wa kiroho. Kinyume na hayo, mwamini mkristo aliyekomaa hutafuta uhusiano zaidi na Mungu ili wakaweze kusaidiana na kuwatumikia wengine.

Pengine watu katika dunia hutumika tu kwa ajili ya kupata kuzawadiwa fedha au hisia. Watu wa Mungu hutumika kwa sababu wamelemewa na shukrani kwa Mungu kwa kazi yake katika maisha yetu. Twatafuta kupendeza yeye na kuwalea wengine. Baadhi ya wakristo wameitwa kuwa wachungaji, lakini waamini wote wamekusudiwa kuwalea wengine. Wachungaji huwaandaa wote ili kutumika. (Waefeso 4:11-12).

Kuwa Na Roho Ya Kutumika

Je mtazamo huu wa kutumika unaingiana aje na maisha yetu? Maono ya kutumika yapaswa kuwa yamehusishwa katika mawazo na moyo wa mwamini. Hii ni changamoto kubwa kwa jamii nyingi katika dunia ambapo walio katika mamlaka wanahisi kwamba sasa ni wakati wa kutumikiwa. Ubinafsi huu ni kweli katika ulimwengu huu wa kisasa. Twatazamia kustaafu ambapo tutajitosa katika anasa, bila ya kuwa na majukumu kwa wengine. mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima” (1 Wakorintho 14:20).

Kama wakufunzi twahitaji kwa makini kuzingatia yale yanayohitajika na wale walio karibu nasi na kutoa aina yo yote ya mafunzo maalum unaohitajika.

Baadhi ya makanisa wanatafuta ratiba za mafundisho. Ratiba huwa mara nyingi ni utaratibu na zisizopindukana mara nyingi bila kuruhusu Mungu atuongoze na kuchangia. Raslimali ni nzuri, lakini wakati sharti utumike na watu binafsi ili kuona jinsi Bwana anavyoongoza mtu. Raslimali nyingi kama vile mikutano ya mafunzo ya video yaweza tumika, lakini lazima tuhusishe nyakati ya kipekee na Mungu.

Asubuhi ya leo, katika wakati wangu mtulivu, kabla sijaandika hili, nilikuwa nikimtafuta Bwana kuhusu maadalizi ya safari yangu ya mafundishi ng’ambo. Bwana alinishawishi kuandika kijibarua kwa baadhi ya ndugu zangu ili waweze kunifafanulia baadhi ya mambo. Nilipoipata tarakilishi yangu, hoja hii ilikuwa imefafanuliwa na barua-pepe kutoka kwa washirikishi wangu akitaja jambo hilo hilo. Mungu alidukua moyo wangu na kisha akadhibitisha hilo. Uamuzi ulikuwa ukihitaji fedha, lakini Mungu alikuwa ndani yake. Nina matumaini kwamba Mungu atatimiza hitaji hilo. Kupitia njia hiyo imani yangu ikakuzwa kwa mambo makubwa zaidi. Mafunzo haya mengi hujifunza faraghani na Mungu.

Wafunze waumini waliokomaa jinsi ya:

  • Kutafuta uhusiano wa dhati na Mungu
  • Chambua kwa kina neno lake
  • Kabiliana na shida kubwa za kibinafsi
  • Vumilia wakati wengine wanakata tamaa
  • Kuwa na imani hata wengine wakiwa na shaka
  • Dhihirisha upendo wa Mungu kwa kuwatumikia wengine
  • Kwa upole kabiliana na wengine inavyohitajika

Mwamini wa kweli haachi kutamani kukua. Tunakua katika uhusiano wetu na Mungu, tukitamani kuwa kama Yesu na kuwatumikia wengine vyema. Kama mkufunzi au mshauri, kila wakati tunamtazamia Mungu ili atuwezeshe jinsi ya kuimarisha maendeleo kati ya nyanja mmojawapo ya maisha yetu.

Somo

  • Waamini wanapaswa kujiwazia kwamba wao “wamekomaa kiroho”, wawezekuwa karibu na Mungu na kuwawezesha ili wakawatumikie wengine walio karibu nao.
  • Mungu anataka tumzalie matunda katika maisha yetu. Hili hutendeka zaidi wakati waamini waliokomaa kiroho huona roho ya Mungu ikifanya kazi katika maisha yetu.
  • Mafunzo yetu ni lazima yatie maono kamili ya waamini lakini kuwaandaa ili wadumu karibu na Mungu na kuwatumikia wengine.

Tafakari Na Kariri

  • 1 Wakorintho 14:20

Zoezi

  • Je, wewe ni mwamini aliyekomaa? Je, unaushahidi upi kudhibitisha jibu lako?
  • Je, una changamoto zipi ili uendelee kukaa karibu na Mungu?
  • Je, umewahi kukabiliana na uchovu wa kazi – ambapo unajihisi umenyauka kiroho na hauwezi endelea kutumika kama vile