
#6 Ishara za Maisha Mapya
Mwanzo wa Maisha
Muhtasari: Kifungu #6, Ishara za Maisha Mapya, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Maisha ya kiroho, basi kama vile maisha ya kawaida, ni msukumo wa nguvu lakini za upole unaodumu katika maisha ya kila Mkristo mwamini. Tunapaswa kuhakikisha kwamba tunayo maisha hayo ya kiroho. Kumbuka kwamba Yesu anatuonya kwamba kunayo tofauti kubwa kati ya magugu na ngano, au wale wasio na maisha halisi kutoka kwa Mungu na wale walio nayo. (Mathayo 13:24-30).
Hapo mwanzo, tofauti hizo ni vigumu kuzitambua. Ninadhani ni kweli kuhusu maisha ya kawaida pia. Umefichika ndani ya mimba, lakini kunazo dalili za kuonyesha kuwepo kwa maisha. picha ya sonograph yawezaonyesha umbo la mtoto ambaye hajazaliwa na mzunguko ndani ya tumbo, ikitoa hakikisho kwa mama mtarajiwa kuhusu afya ya mtoto. Iwapo huu ni ukweli ndani ya tumbo, ni ukweli nje pia.
Mara tu baada ya kuzaliwa kwa watoto wetu, wakunga hufanya jaribio la Apgar kwa mtoto – wakipima afya ya mtoto kwa kukagua rangi ya mtoto, kupumua kwake, kupiga kwa moyo, kujipinda na hali ya misuli. Haya yote yanaashiria kuwepo kwa uhai.
Katika ullimwengu wa kawaida, tunaeleza mzunguko wa mafungu makubwa, kama vile maji au hali ya hewa kama vile mkondo wa upepo – ni kubwa zaidi kiwango ambacho zawezahisiwa kwa urahisi au kuonekana. Twaweza ona mawingu yakipaa au tawi likichukuliwa kwa mkondo wa mto.
Yesu alinganisha mwendo wa Roho wa Mungu na upepo na pia maji. Yohana 3 inaashiria upepo. “Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” (Yohana 3:8). nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele” (Yohana 4:14).
Mifano hii inaeleza ufahamu fulani kuhusu nguvu za asili za maisha, kila ikizungumzia kuhusu urembo na nguvu za maisha pamoja na mkondo wake.
Yesu anaelezea Roho katika Yohana 3 kama upepo uvumao kutoka upande huu au upande ule. Nguvu hizi zimeelekezwa badala ya kutawanyika, na vivyo hivyo katika maisha ya kiroho – tele na huru, lakini yenye kusudi sana.
Uonyesho La Kazi Za Roho
Yohana 3:8 yaeleza vyema kwamba mwamini ‘amezaliwa kwa roho’. Maisha yake ya kiroho yanatambulikana na kuwepo kwa Roho ya Mungu. Maisha ya kiroho, basi yatakuwa na aina na ‘dalili za uhai’ amabazo zimeunganishwa na uwepo wa Roho Mtakatifu. Hapa zimo dalili chache za maisha haya ambayo yanachochewa na Roho.
- Shauku la neno la Mungu.
- Hamu ya kuwa na waamini wengine wakristo
- Nia ya kuzungumza na Mungu (Maombi)
- Kufahamu kuwepo kwa dhambi
- Haja ya kupata msamaha kupitia Yesu Kristo
- Hisia zinazokua kwake Mungu na njia zake
- Kufahamu kuwepo kwa wengine na kushughulikia mahitaji yao
Orodha hii yaweza endelea, lakini tumehesabu hizi kusisitiza kwamba maisha mapya ndani ya Kristo yajidhihirisha kupitia kwa shauku na ufahamu wa kimsingi, kama vile mtoto mchanga hupumua, husonga, hulia na huona njaa. Yesu alisema, “Basi zaeni matunda yapasayo toba” (Mathayo 3:8). ndani yao. Katika hali hii, watu wangekuwa wanafahamu kuzihusu dhambi zao na kunyenyekea badala ya kuwatendea watu vibaya, wangewashughulikia vyema. Kunazo ishara nyingi za maisha mapya. Nyingine ni dhahiri kuliko nyingine, kulingana na mazingira. Shauku hizi zinatokana na maisha mapya yaliyotokana na Roho Mtakatifu aishiye ndani ya roho zetu. Zitaunda mawazo yetu na tabia zetu wakati unapoendelea na hivyo kufanya matendo yetu ya kiroho kuwa dhahiri kwa wengine.
Somo
- Upepo na mito yatufundisha kuhusu uwepo, kusudi na nguvu za Roho Mtakatifu
- Maisha mapya hutokana na uwepo wa Roho ndani ya mioyo yetu
- Maisha ya kiroho, kama vile maisha ya kawaida, hudhihirisha ukweli wake kupitia ishara kadhaa zinazotarajiwa.
- Ishara hizi za maisha ya kiroho zitakuwa dhahiri kwa kila mwamini wa kweli ingawa zaweza dunishwa au kuharibiwa kwa kuendelea kutenda dhambi.
Kariri Na Tafakari
- Mathayo 3:8
- 1 Yohana 3:10; 23-24
- Waza kuhusu wakati ulipompokea Yesu. Rejelea ishara za maisha zilizotajwa hapo awali. Je, unaweza kuzitambua katika maisha yako? Zitaje zilizo muhimu.
- Na je leo? Ishara hizi zastahili kuwepo hata leo. Ndio majaribu, kujitenga na Bwana kutazidunisha, lakini ni kipi kilicho cha muhimu kwako? Iwapo mmojawapo wa dalili hizi za maisha ni za kweli kwako, ziandike karibu na picha hii iliyopo hapo chini.
- Baada ya kuziandika taja kila mmojawapo katika maisha kama vile. “Nalipenda neno lake Bwana”. Hizi ni shauku kuu ambazo sasa ni za kweli kukuhusu iwapo umezieleza vyema au la. (Kuziombea ni jambo muhimu sana).
- Iwapo shauku hizo sio za ukweli kukuhusu, basi kunao uwezekano kuwa bado hauna Roho wa uhai ndani yako. Unapaswa kumpokea Bwana. Mwite Mungu wetu akuokoe kupitia kwa Yesu Kristo.
- Jinsi wakati unavyokuruhusu, soma Yohana 3:1-8 na Yohana 4:10-14 kama vitambulisho. Tafuta kifungu cha maneneo ambacho kinalinganisha Roho na upepo na maji ikitukumbusha kwamba Roho Mtakatifu ndiye chanzo cha maisha ya milele.