Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#29 Kuwadumisha Waamini Wachanga

Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #29, Kuwadumisha Waamini Wachanga, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Wachanga

Mahitaji ya vijana wanaobaleghe ni tofauti na mahitaji ya watoto, kama vile mahitaji ya mwamini kijana ni tofauti na ya mwamini mchanga. Tofauti imekuwa ni muda wa mwaka moja lakini mengi yamebadilika katika huo mwaka. Kifungu hiki kitaangazia kufunza waamini wakristo wachanga.

Huku hatua kelekea kukomaa huleta kwa haraka waamini wachanga katika hali mpya ambayo inamtayarisha kufikia utu uzima wa kiroho, bado hawajafika hapo. Wanahitaji mafundisho ya kiroho ili kuwaongoza wanapopitia mahangaiko ya namna ye yote ile.

“Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda Yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba.

Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmeshinda yule mwovu” (1 Yohana 2:13-14).

Yohana tena anatupa maono maalum kutoka 1 Yohana 2:12-14. Anatuangazia hali ya mashindano, majaribu na kujifunza kutoka neno la Mungu. Mfano wa mtu aliyevaa silaha za vita katika Waefeso 6 yaja katika mawazo yetu.

“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba baadhi ya waamini hupitia mbali ni jambo ambalo waamini wote hatimaye watakumbana nalo – hilo litahusisha sehemu kubwa na mafundisho yao.

Ufanisi wao katika hatua hii ya pili kunahusiana kwa karibu na jinsi walivyotunzwa katika hatua ya kwanza. Mafundisho ya mwamini mpya husaidia kupata mtazamo mwema kwamba Mungu huwa karibu kila wakati kuwasaidia. Huwasaidia pia kupata uhusiano mwema na washauri. Bila ufahamu huu kusindilia ndani yao, haitakuwa rahisi kwao kumtumaini Mungu wanapopitia mafundisho ya mwamini mchanga. Shaka huleta kuvunjika moyo na kushindwa, ambako hatimaye huenda kukasabaisha kukata tamaa, wakiwaza iwapo wataweza kuwa washindi.

Ufahamu kwamba ‘vijana wote wanaobaleghe’ kiroho hupitia katika hatua hii huifanya rahisi kwa ‘mkufunzi’. Hebu tukapate kuwajua marafiki wapya au wanafunzi ambao huja kanisani mwetu. Twaweza anza kukagua wako wapi katika safari yao ya kiroho. Hii pia itatusaidia kuweka vifaa vya kukagua ili kujua ni nini kanisa laweza tenda ili kuwasaidia katika hali walioko ya kukua kiroho kwa sasa. Yale ambayo awali yalikuwa hayafahamiki vizuri sasa ni wazi kabisa.

Kuhakikisha kwamba hamna hatari ya kulinganisha mtu binafsi na wengine ila kuiweka vyema, ramani ya ukuaji wa kiroho yaweza tumika. Hili itasaidia kila mwamini ajikague mwenyewe na kuwahimiza wenzake – sio kuhukumu. Nia yetu ni kusaidia watu wakue na wala sio kukashifu au kulinganisha.

Mahitaji Ya Mwamini Mchanga

Mwamini mpya anahitaji kujifunza`kweli za kimsingi kuhusu wokovu, hakikisho la milele, na kadhalika’. Kweli hizi zinajenga matumaini ya kimsingi Mwamini mchanga hata hivyo sharti ajifunze kutumia neno la Mungu akiwa peke yake. Anahitaji kulishwa kila mara, ila anapaswa kujilisha mwenyewe neno la Mungu. Mabadiliko haya yatakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mafundisho yetu. Ni lazima tumwezeshe mwamini kupata ujuzi wa kuendeleza nidhamu yake ya kiroho akiwa na roho ya kuona na kutumaini, tayari kulitekeleza neno la Mungu kwake binafsi. Kwa mfano kuwafunza watu jinsi ya kusoma biblia kwa undani kutawasaidia sana katika kupata ujuzi wa masomo zaidi lakini sharti tukumbuke sote hatuna kiwango sawa kielimu kutenda hili.

Kina cha mwamini mchanga kuhusisha neno la Mungu katika maisha yao kutaadhiri pakubwa jinsi watakavyoweza kumpinga yule mwovu. Mafundisho ya walio wengi hapa ni mazuri lakini kushauri moja kwa moja kunafaa ili kusaidia katika shida za kibinafsi. Kuanzisha uhusiano mwema wa kutenda kazi kunatusaidia ili kuweza kushauri jinsi watu wanavyotenda katika hatua tofauti za maendeleo.

Umri wa mtu binafsi unaweza adhiri jinsi mwamini anavyoweza kukua kwa haraka kiroho. Mtoto mdogo atachukua muda mrefu kiasi kuliko mtu mzima ili kupitia kiwango cha mwamini mpya. Hii inatokana na uwezo wao kupokea na kuichanganua habari na jinsi wanavyotangamana na wengine.

Kusudi Kwa Mwamini Mchanga

Urefu wa hatua hii ya pili ya mafundisho, hata hivyo utategemea lakini yapaswa kuchukua miaka mitatu. Baadhi ya wengine, kwa bahati mbaya hawakui kupita hatua hii. Hawajawahi kujifunza masomo yanayohitajika.

Kutoka kwa Yohana tunaweza chambua kwamba mwamini mchanga ana mambo kadha ya kujifunza: 2) Fahamu mafunzo maalum kutokana na neno la Mungu kuhusu nyanja kama vile kumshinda shetani kupitia kazi ya Yesu Kristo msalabani.

3) Kila wakati tofautisha na shinda majaribu ambayo huja katika maisha yetu.

Ni vigumu iwapo haiwezekani kusema kwamba mtu anapokuwa kijana wa

kubaleghe na huacha nyuma miaka ya ujana na tabia. Kwa sababu haieleweki vizuri katika maisha ya kawaida, pia twaweza ruhusu iwe hivyo kiroho maana haitaeleweka kwa urahisi. Kunazo nyakati mtu atakuwa mchanga kiroho na kuonekana kana kwamba amekomaa ilhali nyakati zingine itakuwa ni kinyume.

Ni vyema zaidi kuangazia malengo kuu ya mwamini mchanga na kutambua ni nini sharti litendeke ili kuyaafikia malengo haya. Bwana wetu anaweza kutumia kila aina ya hali tunazokumbana nazo ili kutufundisha. Hamna jambo asiloliweza. Kuwa mwanafunzi, kama mkufunzi mkuu, yeye hapotezi wakati.

Kuinua Washauri Wema

Kitabu chetu cha kufundisha hatua ya pili kinaangazia jinsi ya kutumia neno la Mungu ili kukua katika hatua hii ya mwamini mchanga. Kumpata mshauri mwema ambaye anaamini kwamba tumemshinda yule mwovu sio tu kwa maneno mbali katika hali halisi ni muhimu sana.

Kwa sababu waamini wengi hawajafundishwa vyema, hawafahamu vyema

masomo haya. Mkufunzi lazima ajifunze jinsi ya kuwaongoza watu hawa na kuangazia ni wapi wastahili kuwa kama waamini. Iwapo mshauri hajajifunza jinsi ya kuyaepuka majaribu kwa njia moja au nyingine katika maisha yake, Nakumbuka nikijifunza ushauri na kusoma vitabu vingi vya kufundisha wachungaji ili kunisaidia kupata ujasiri nikapate kukua katika maeneo ambayo nilikuwa na changamoto. Haya ni mambo ambayo ningalifunza hapo mwanzo katika maisha yangu.

Kuna kutoamini fulani katika kanisa kwamba waamini wanaweza kuyashinda majaribu fulani ya kibinafsi ambayo yanawakumba. Majaribu haya mara nyingi huwa yanahusiana na maadili ya maisha yetu na jinsi yanavyoweza kuangazia mahitaji ya wengine badala ya mahitaji yao wenyewe. Mawazo ya ‘mhusika’ hudhani kwamba hamna njia ya kushinda. Pasipokuwa na historia ya kushinda, washauri hawana ujumbe wa tumaini kuwapa ila tu kutoamini na kuwapumbaza wale wanaowafunza kueleza kushindwa ni jambo moja lakini mshauri ameeleza kuhusu ushindi.

Hii ndiyo sababu twahitaji kuiweka ramani ya maendeleo ya kiroho wazi kusudi kila mtu, hata washauri waweze kuona wako wapi. Inachochea waalimu, wachungaji na wakufunzi kwa imani kwamba Mungu anaweza kuwasaidia katika tabia zinifu kama vile kutazama picha za ngono (kwa kweli ni uasherati), kiburi cha kiroho, hasira, na kadhalika. Tunakataa mazoea yanayozidi kuongezeka ya kutuma waamini wenye matatizo kwa ‘wataalamu’ ambao wanakomesha shida kwa utumiaji wa ‘dawa’ au ‘kupimwa akili na roho’. Haya yanaweza kuwasaidia kutokana na tabia iliyozidi mipaka lakini hulemaza mfumo wao wa kiroho kujishughulikia. Mbona tusiwaonyeshe jinsi ya kushinda mambo haya na kujifunza jinsi ya kumtegemea Mungu kwa mambo yao? Nia yetu ni kuunda ufafanuzi wa waamini wachanga ili wakaweze kumwona yule mwovu akiwajaribu na jinsi ya kumuepuka.

Wanapoendelea kutenda haya, wataenda hatua ya tatu ya kukua kiroho – moja ambayo itaendelea maishani mwao mwote duniani.

Bila imani ndani ya Mungu katika hatua, hatutaweza kufikia lengo kuu la kukomaa kiroho. Lakini tukiamini, kwa njia moja au nyingine, kwamba kazi ya Mungu itatusaidia tusikate tamaa.

Somo

  • Mwamini mchanga ana njia tofauti ya ukuaji kuliko ya mwamini mpya.
  • Mwamini mchanga sharti ajifunze jinsi ya kujilisha mwenyewe na neno la Mungu ili akaweze kuyashinda baadhi ya majaribu.
  • Kuna shida kanisani kwa sababu waamini waliokomaa hawajashawishika kwamba wanaweza shinda kila aina ya jaribu (hawakuwa kupita kiwango hiki).
  • Ijapokuwa hatua za kuyashinda majaribu ni muhimu, waamini wachanga pamoja na wakufunzi wao mara nyingi hawawezi kujitenga jinsi ya kutenda hili, na hivyo waamini wanazama katika hali ya vuguvugu.

Tafakari Na Kariri

  • Waefeso 6:11-12

Zoezi

  • Kwa nini unaamini kwamba wewe ni au sio mwamini mchanga? Toa sababu.
  • Je, umejiandaa vipi kumfunza mwamini mchanga ili kuyashinda kila aina ya majaribu?
  • Je, kunao maeneo ambao hujayashinda au hautajua kumsaidia mtu mwingine? Ni maeneo yapi? Muulize Bwana akarejeshe imani yako