Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#5 Msukumo wa Maisha

Mwanzo wa Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #5, Msukumo wa Maisha, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Wepesi ni wema. Tena na tena imeshadhibitishwa ya kwamba wepesi ni wema. Na hii kweli hata kwa mafundisho ya kukua kiroho pia.

Mungu ametia kweli zilizo muhimu katika maisha kupitia kwa kanuni zinazoonekana katika maumbile. Hii ndio sababu Yesu alitumia mifano rahisi kutoka kwa maumbile kueleza kweli za kiroho amabazo hazingeeleweka vinginevyo. Maumbile kwa mfano yatupa taswira mzuri ya kukua kiroho. Ijapokuwa maisha ya kiroho ni magumu kueleza. Kwa sababu ya hali yake ya kiroho, bado twajua mambo mengi kuhusu mwanzo na kuendelea kwake.

Hebu kwa muda waza jinsi tunavyoishi kwa kweli. Umewahu kumwona mzazi ambaye huamka alfajiri na mapema kila asubuhi, kisha kuelekea kwa mwanawe na kumwambia, `kua’, ‘kua’, ‘kua’ hilo litakuwa jambo la kushangaza, sio kwa sababu hatutaki akue. Mzazi awaye ye yote huhofia iwapo mwanawe hakui vyema. Sababu ambayo hufanya tusitende hayo ni kuwa kukua huja kawaida, bila mipango yetu, kuhimiza kwetu au kuhofu kusio na maana. Ukuaji ni sehemu ya maisha. Maisha yajua jinsi ya kuendelea na kukua kivyake.

Ni vivyo hivyo katika maisha ya kiroho. Maadamu yapo, mtu haweza kuona kujitolea kwake ili kukua, lakini bila shaka yaweza kutatanisha.

Kuwepo Kwa Uhai

Roho wa Mungu ameunganishwa na mifano hii ya uhai kwa sababu Roho ni uhai. “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisa“(2 Wakiorintho 3:6). ndani ya mwamini, mara hiyo huwa amewekwa katika njia ya maendeleo na kujieleza kama vile kukua kwa kawaida lengo lake sio kudhibitisha kuwepo kwake bali ni kuendelea hadi kukomaa.

Wakati waamini wanatambua hili, uoga kuhusu kukua kwao kiroho kunaweza kutengwa kando. Kuwepo kwa Roho mtakatifu ndani ya mwamini kunamhakikishia kwamba nguvu za kukomaa kiroho zimo tele. Badala ya kuwa na wasiwasi kama watakua kutokana na kulemewa au kushindwa kwa kale, waweza furahia ndani ya kusudi la Mungu la kukua na kisha baadaye kutafuta jinsi ya kutimiliza malengo yake.

Imani hubadilisha wasiwasi. Matarajio hupunguza kukosa mwelekeo.

Msisimko huu huanza tunapoangazia kazi ya Mungu ambayo aliianzisha katika maisha yetu tulipo okoka. Hapa ndipo ufufuo huanza: huu ndio mwanzo wa imani yetu. Huu sio tu ukweli kwa mwamini binafsi bali wote wanaofundisha watu wa Mungu. Waalimu nao pia ni lazima wafahamu nguvu za kipekee za Mungu na kutafuta kazi za Mungu katika maisha ya waamini. Kile Mungu alichokianza atakiendeleza. Iwapo ametupa maisha mapya, hana budi kuyakuza na kuyaendeleza katika wakati wetu hapa duniani. “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu” (Wafilipi 1:6).

Ufahamu Wa Maisha Ya Kiroho

Ni lazima tuweke makataa mepesi lakini muhimu kutoka hapa. Watu wengine hushangaa ni kwa nini waamini hawakui kiroho. Shida kuu na kukua kiroho mara nyingi hakutokani na tabia yake kama vile ilivyo katika maisha ya kawaida. Sisi tuko hai au la. Mtu hasemi “Mimi siko hai vya kutosha” ijapokuwa shida za kiafya zaweza adhiri ubora wa maisha.

Wakati mtu kwa kweli amezaliwa mara ya pili, maisha yake ya kiroho yapo na wingi wa matarajio, yakitumaini kukua. ukamilifu, hatua kwa hatua. Hamna vitengo au daraja tofauti za maisha ya kiroho. Hatupaswi basi kuweka makataa kwamba maisha ya kiroho ya mchungaji ndiyo yenye ubora halisi kuliko yetu.

Wakristo waweza kua katika hatua tofauti tofauti lakini hii sio kutokana na nguvu au chanzo cha maisha. Kunazo sababu nyingine kwa ajili ya hayo.

Somo

  • Waamini hawahitaji kujifanya kukua kana kwamba sio jambo la kawaida.
  • Hamna vitengo au daraja tofauti za maisha ya Mungu. Mungu yuaishi kwa usawa kwa kila mwamini.
  • Kubadilika hutokea wakati mioyo yetu yadhihirisha kumtamani Mungu ili mapenzi yake yaishi kukua na kufanya kazi ndani ya maisha yetu ya kawaida na ya kiroho.

Kariri Na Tafakari

  • Wafilipi 1:6
  • 2 Wakorintho 3:6

Zoezi

  • Ni waamini wa kweli ndio waliozaliwa mara ya pili, sawa na “kuzaliwa toka juu”. Je una uhakika kwamba umezaliwa mara ya pili; kwamba kumjua Mungu kunakopatikana katika msamaha wa dhambi kupitia kwa kifo cha Yesu Kristo msalabani?
  • Tia alama na kisha andika tarehe na wakati kwa uweza wa fikira zako, ni wakati upi uliwahi kuwa mwamini – wakati maisha ya kiroho
  • Soma Waefeso 1:13-14. Tambua jinsi Roho Mtakatifu anavyodumu ndani ya mwamini wa kweli. Mshukuru Bwana kwa ajili ya kazi yake ndani yako.