
#12 Malengo ya Maisha Yetu
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #12, Malengo ya Maisha Yetu, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Kila nguvu zina mkondo na uweza wake. Kwa mfano, upepo unawezavuma kuelekea kaskazini mashariki kwa kasi ya maili sitini kwa saa. Huo utakuwa upepo mkali.
Nguvu zetu za maisha ni sawa. Miili yetu ya kawaida inakua kulingana na nguvu hizi za maisha na baadaye kutuwezesha kutenda kazi katika ulimwengu wa kisasa. Twaweza zungumza kwa simu za rununu au kushuka kutoka kwenye basi iliyojaa watu. Nguvu za maisha ya kiroho humimia maisha yetu ya kiroho kwelikweli. Ingawa hutenda kazi kwa kiasi kikubwa katika umbo na mawazo yetu ya kimwili, ina kusudi na nguvu zake kipekee.
Ili tukaweze kukua, ni vyema tukatofautishe mwelekeo au malengo ya maisha haya ya kiroho. Kisha badala ya kupingana na malengo ya maisha, twastahili kutenda kazi nazo. Nimetembea tembea katika mitaa ya Chicago siku za upepo mwingi wakati nimetumia nguvu nying hata kutembea. Upepo ulikua ukivuma kunielekea. Kwa upande mmoja, nimewahi kwenda kwa baiskeli kwa mwendo wa kasi bila hata kuendesha kwa sababu upepo mkali umekuwa ukinisaidia kutoka nyuma.
Kuyapanua Maarifa Yetu
Maarifa yamebaki kuwa hali kuu katika maisha ya kiroho. Kama tungeweza kuunganisha ufahamu wa yale Mungu ametenda katika maisha yetu na kujibidiisha kuyatenda hayo, basi mapigano mengi yetu ya kiroho yatatokomea.

Kwa kweli waamini wengi hawafahamu kuhusu ni malengo gani Mungu aliyonayo kwa ajili ya maisha yao. Baadhi ya haya ni ya kawaida. mapepo. Kama upepo, Roho wa Mungu hawezi kuonekana kwa macho yetu. Twaona tu jinsi anavyobadilisha mambo katika ulimwengu wa kweli.
Macho ya mtumishi wa Elisha ilibidi yafumbuliwe ili awezekuona mambo ya kiroho. “Kisha Elisha akaomba, akasema, ee Bwana, nakusihi mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na gari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote” (2 Wafalme 6:17).
Kupitia kwa kusoma neno la Mungu, tunaweza kupata jinsi ilivyo katika ulimwengu wa kiroho. Kwa mfano, twajua kutoka kitabu cha Waebrania kuwa takribani malaika mmoja husimama kando ya kila mtoto wa Mungu.
(Waebrania 1:14).
Upepo Unavuma
Neno la Mungu halizungumzii zaidi kuhusu maelezo haya kwa undani, lakini linaangazia zaidi kuhusu kanuni – yale ambayo maishani mwetu kupitia nguvu za maisha ya kiroho. Paulo ameshatambua lengo hili kwa waamini “Ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo” (Wakolosai 1:28).

Petro asema hivyo tofauti kidogo “bali yeye aliyewaita alivyo mtakatifu. Ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1 Petro 1:15-16).
Tumekuwa tukitumia neno ‘nguvu za maisha ya kiroho’ tukilinganisha na nguvu za maisha ya kumwili kutusaidia kuelewa vyema, lakini kuna mengi zaidi ya haya. Kama vile Kristo kupitia kwa neno lake aliumba na kusitiri maisha ya kawaida, (Wakolosai 1:15-17), basi Kristo kupitia kwa Roho yake alitoa ‘nguvu zake’ ndani yetu.
Mmojawapo wa shida tunazopata kama waamini ni kudhani kwamba maisha ya kiroho na maisha ya kawaida hutokea tu. Hiyo sio kweli. Nguvu za Mungu zatenda kazi ndani yetu kukamilisha mapenzi yake. Hii ni kweli kwa kila mtu na chochote kilichoumbwa. Vitu vyote ni vya kuleta utukufu kwa Mungu. Hii pia ni kweli kwa Roho Mtakatifu ambaye huwapa maisha ya kiroho wale wamwaminio Kristo.
“Nami nitamwoba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele, ndiye Roho wa kweli; ambate ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaakwenu, naye atakuwa ndani yenu” Yohana 14:16-17 Mungu yuko hai ndani yetu ili kutuwezesha kufahamu ya kiroho, kunena nasi, ili sote kwa pamoja tuweze yatekeleza makusudio yake makuu kupitia na ndani ya maisha yetu.
- ‘Nguvu za maisha ya kiroho’ hulingana na nguvu za maisha ya kawaida zinazoyaendesha maisha yetu.
- Nguvu za maisha ya kiroho zinatenda kazi katika maisha ni zile zile ambazo kama Kristo akitenda kazi ndani yetu kupitia kwa Roho Mtakatifu.
- Tunapokusudia kuunganisha mapenzi yetu na malengo ya Mungu katika kutenda kazi, basi maisha ya kiroho na yale ya kawaida, huyafanya mambo kuwa rahisi na lenye malengo.
Tafakari Na Kariri
- 1 Petro 1:15-16
- Yohana 14:16-17
Zoezi
- Umewahi kuwaza kuhusu Mungu akitumia Roho Roho Mtakatifu ili kutimiza malengo yake? Eleza.
- Kutoka Wakilosai 1:28 na 1 Petro 1:15-16 tu, ungesema Mungu anataka kutenda nini kupitia nguvu za maisha ya kiroho zilizoko ndani yako? Unaendelea vipi?