Kiini Cha Maisha Swahili Life Core banner

#19 Kusudi ya Mafundisho

Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha

Paul J. Bucknell · Kimetafsiriwa na Miriam Okeyo

Muhtasari: Kifungu #19, Kusudi ya Mafundisho, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.

Wakati waamini wanaposikia kuzihusu hatua hizi tatu, mara nyingi huwa wanahimizika. Wanapo lifahamu wazo hilo, ni kana kwamba wamepewa miguu mipya. Wengi wao hawajali kuwaza maisha ya Kikristo katika hatua hii, pia inawahusu waalimu wa wakristo na wahubiri. Kwa sababu hii hamna vifaa vingi vya ukaguzi vimewekwa ili kutusaidia kupambanua tuko wapi katika maisha yetu ya kiroho.

Mambo Ambayo Siyajui

Waamini wa kawaida hufikiri maisha ya kiroho hayaeleweki na ni ya kuchanganya. Kubwagizo chao ni “Mimi nimeokoka na ninastahili kuwa ninatazama mbinguni”. Wamechanganyikiwa kuhusu jinsi njia ya utakaso inapaswa kuwa.

Mke wangu nami huwafunza wazazi kuhusu malezi ya watoto. Tunazipata shida hizo hizo kwa ukosefu wa tajiriba nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa familia kubwa au akina mama kutokaa nyumbani. Walio oa hivi majuzi hawajui jinsi ya kuwalea wanao.

Mtu angedhani kwamba msingi ya kulea watoto au kuwanyonyesha itakuwa bila kufikiria, lakini sivyo. Kunayo mambo fulani lazima mtu ajifunze vyema kuhusu kunyonyesha au kulea watoto wema. Hisia wakati mwingine yawezakuwa haisaidii. Hii ndio sababu hospitali na kliniki za wakunga zimeongeza madarasa kama hayo.

Hiyo pia ni ukweli na mafundisho ya Kristo. Je, twaweza hisi uwepo wa Mungu na kumwabudu? Je, waamini watakua tu kwa njia ya asilia? La, mara nyingi haiwi hivyo, zaidi kwa ulimwengu huu wetu wenye dhambi. Hata (Warumi 1:19-20), au makosa ya ubinafsi. Mambo haya yanaweza kuwa sio bayana. Mara nyingi hisia zetu zaweza badili ule ufahamu hafifu tulio nao.

Hii ndio sababu Yesu alitwambia tufanye watu kuwa wanafunzi wake. Ni sharti tuwalete wengine hadi mahali ambapo watajifunza kuhusu yale Yesu alisema na kutenda. “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19).

Ninafurahi kuona watu wengi hivi majuzi wameanza kuandika kuhusu kuwafundisha wanafunzi, lakini yahuzunisha kuona wengi hudhani kwamba hii ni mpangilio badala ya mkondo, tukizingatia zaidi kuujenga uhusiano badala ya mambo yaliyomo. Ninapendezwa na mtazamo wa jinsi mtu binafsi anavyojitolea kufunza wengine. Ninafunza hili kwa sababu mara nyingi ni sanaa hii iliyosahaulika na kuachiwa madarasa ya ushauri. Twastahili kuendelea zaidi ya hapa. Kusudi letu ni kufundisha ili wengine wapate kufahamu ‘kujifundisha’ huku ndio maana halisi ya kufunza. Baadhi yetu hujihisi tumetulia na mafunzo kiasi ambayo yanaweza jaribiwa na kupimwa. Masomo ya shuleni yametufunza kwa ajili hii. Mambo ya kiroho, hata hivyo hayajaribiwi kwa urahisi na hivyo: 1. Hupuuzwa kwa urahisi 2. Sio dhahiri (isipokuwa ifundishwe vyema)

3. Yaonekana hayahusiani Paulo na wengine wanadhibitisha umuhimu wa mabadiliko yanayotokea tukijifunza vyema mambo ya Yesu. “Mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” (Waefeso 4:24).

Kubadilika katika mawazo (4:23) ni muhimu lakini lazima kufuatwe na dhihirisho na dhibitisho ya kutosha ili kuleta mabadiliko yanayohitajika.

Ninavutiwa na mpangilio wa mafundisho kama yalivyoelezwa katika

Yohana 2:12-14. Yohana anaifanya rahisi kuelewa kwa sababu sote tunaufahamu mfano wa familia, pengine kwa kulelewa ndani ya familia au kwa kuona wengine wakilelewa ndani ya moja. Mungu anaifanya rahisi kwetu kujifunza na kukua.

Zaidi ya hayo, Yohana anatoa mfumo kamili kwetu ili kila mtu ajifunze sehemu yake binafsi. Hatua hizi tatu zimetajwa katika sehemu iliyopita lakini huu ni mwanzo tu. Kujifunza kiroho ni kama kuzama ndani sana katika bahari. Twaweza kumbwa na dhoruba ambayo hatukudhania, na tukose kufika kwenye sakafu, lakini Mungu anatuita tuingie katika maji makuu. Anataka tumtumainie kwa yale anayaleta kwa maisha yetu ili tukaweze kufurahia zaidi watu na mipango yake mitukufu.

Kutoka Mtazamo Wa Kufundisha

Katika kifungu hiki, chanzo cha maisha na kiini cha maisha, tutakuonyesha jinsi utaratibu huingiana kutoka kwa mtazamo wa masomo na mafundisho. Tumefanya hivi kwa njia ndogo kwa kiwango cha binafsi, lakini ni vyema kutumia ‘kifaa’ hiki au kudadisi mafundisho kanisani kwa ujumla.

Njia hii hutusaidia kuja na njia mwafaka ya kufundisha ambayo inawezatekelezwa na mafundisho yetu ili kuongeza kukua kiroho badala ya kuongeza masomo tu. Sijui kama tunaweza leta kipimo kiasi ambacho waalimu mara nyingi huangalia, lakini twaweza kukusaidia kufikia ambayo Mungu amekususudia kwako.

Kwa kawaida, mwalimu mkristo, awe kanisani au shuleni, anatamani kila mwanafunzi wake akue hadi kufikia utimilifu wake ndani ya Kristo. Iwapo haya ndio malengo yetu, basi lazima tupalilie mazingara mema yatakayosaidia kujifunza. Kujifundisha ni dhana ambayo hutusaidia kuyafahamu malengo Mungu aliyo nayo kwetu.

  • Kufundisha kunaeleza kusomesha kulikotokea wakati mwamini aliyekomaa anamsaidia aliyemchanga kujifunza kanuni muhimu kumhusu Yesu ili wakapate kuishi maisha yanayofanana na Kristo.
  • Changamoto za mafundisho ya Kikristo, rasmi au la ni kuwa na mwamini ambaye anapata mabadiliko ya kiungu.
  • Ukosefu wa mtazamo wa elimu ya kupima kunaifanya vigumu kukagua kiwango cha mafundisho.
  • Mabadiliko ya maisha ambayo hutokea wakati mtu anamjua Mungu kupitia Kristo ni ya kuvutia. Mwalimu anaweza kuona mabadiliko ndani ya mwanafunzi.

Tafakari Na Kukariri

  • Waefeso 4:24

Zoezi

➢Toa mfano wa wakati ulijifunza kuhusu jambo fulani lakini ukakosa kusadiki na kulitekeleza.

➢Waweza sema sasa una hamu kuu ya kukua kiroho? Iwapo ndio, kwa

nini? Iwapo la, kwa nini?

➢Je, umewahi kumfunza mtu mwingine? Nani? Lini?