
#9 Kupata Kufahamu
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #9, Kupata Kufahamu, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Baada ya kutaja jinsi vile Roho hutenda kazi kwa jumla, tunahitaji kutazama kazi yake katika maisha ya mtu binafsi. Baadaye katika sehemu ya mwisho ya kitabu hiki, tutapata mtazamo mwingine kutoka upande wa mkufunzi.
Katika maisha ya kawaida, mara nyingi hatuhisi uwepo wa maisha. Ijapokuwa twaongozwa na kuhusishwa na nguvu hizi kuu za maisha, ni kana kwamba hatuelewi kuhusu uwezo wake wa kutupa uhai kila wakati.
Wakati wa kubaleghe, vijana wa kiume na wa kike wanajishughulisha sana na mabadiliko miili yao inayopitia. Wanaangalia kwa makini miili yao inavyobadilika na faida yao, lakini hawafikirii kuyahusu maisha yaletayo hayo mabadiliko. Kwa sababu hiyo, vijana hujishughulisha wao ni akina nani. Baadaye katika maisha, watu wanaanza kuangazia ni nini walicho nacho. Ni wachache wanaowaza ni kwa nini waweza kukua hadi utu uzima au baadaye kupata kazi. Shughuli za kila siku zimepofusha ufahamu kutanabahi kwa maisha ya kiroho na ya kawaida.
Kutokuwa na shukrani kunasababisha kuishi maisha ya kujitawala wenyewe ambayo mwisho wake ni kiburi.

Hii ndio shina ya maisha ya leo yenye kutamani mali na anasa. Ikiweko dhana kwamba vyote vilivyomo vyaelezwa katika hali ya chembechembe na vitu, hamna tena haja ya kuangalia nguvu zinazosukuma maisha yao. Kwa urahisi wanaziba wazo la Mungu kuhusika katika maisha ya ulimwengu huu, ijapokuwa wanamtegemea yeye kwa kila kitu walichonacho.
Shida Ya Kiroho Iliyofichika
Ukosefu huu wa maarifa umekithiri kanisani pia lakini katika kiwango tofauti. Hatutilii maanani nguvu hizi zinazotutia nguvu katika maisha yetu. Twaanza kuangazia zaidi yale tuyaonayo na kuyashika kuliko yale yawezeshayo maono yetu na kujitolea kwetu.
Nyakati zangu kumekuwa na ushawishi wa Mungu ambao umehusisha kanisa.
Kitabuni ‘Body of Life’ chake Ray Stedman kiliwafahamisha watu wa Mungu kuhusu karama zao za kiroho na pia kuhusu roho wa Mungu awawezeshaye watu wa Mungu kwa ajili ya karama hizi. Uhusiano kati ya mambo haya mawili ulikuwa sio tu kutenda kazi mbali kwa mafunzo ya dini. Watu wa Mungu walibarikiwa lakini maendeleo haya machache yalikuwa mafupi na yalifichwa na maendeleo mengine ya kidini.
Vuguvugu la uchangamfu wa neema kwa njia ile ile limeunganisha karama za kiroho na Roho Mtakatifu lakini lilikuwa pana zaidi; likisambaa duniani kote. Watu wakaanza kuwa na masomo ya Biblia, maombi hata katika makanisa yaliyofifia. Haikujalisha mtazamo wa karama hizi na bila shaka kulikuwa na himizo la ishara katika sehemu nyingine, kujishughulisha huku kupya juu ya kazi za Roho katika maisha yetu kulileta uhai tena katika utaratibu wa makanisa yaliyokufa. kanisa hakutufanyi kuwa mshiriki wa kanisa. Na pia kujua mengi kumhusu Mungu hakutufanyi kumjua Mungu. Ni vyema tukijua mambo haya, lakini kupuuza umuhimu wa nafasi kuu ya Mungu katika maisha yetu au mafundisho yaweza kuwa kikwazo kikubwa. Upofu wa kiroho unaitwa kutoamini na utatuzuia kupata ushindi.
Ufufuo Wa Kale
Ufufuo wa awali ulirejesha ufahamu mkuu wa uwepo wa Mungu. Watu
walijua kwamba sio tu yale waliyoyatenda yaliyoleta utofauti, lakini Roho Mtakatifu akitenda kazi ndani na kupitia kwetu. Ufahamu huu wa Roho wa Mungu akitenda kazi kupitia kwa maisha yetu ni muhimu. Upuuzapo hilo, uhasibifu hutokea; kama vile: kufuata dini, kiburi cha neno la Mungu, uchovu wa Kiroho na kushuka kwa kanuni za maadili. Matokeo yake yote ni kutoelewa vyema jinsi Mungu hutenda kazi ndani yetu.
Imani inayotokea yakaribiana na dini ya kibinadamu. Kuangazia kwote kuko kwa juhudi na mawazo ya mwanadamu badala ya Mungu. Haya ndio tuyaonayo katika jamii leo - ulimwengu unaojifikiria pekee.
Kuamini Kwamba Mungu Hayuko Kwa Kweli
Nimetumia kifungu hiki “Kuamini kwamba Mungu hayuko kwa kweli”
Kueleza mawazo ya waamini wengi kwa miaka mingi – waamini wanaoendeleza maisha yao ya kikristo bila kutambua uwepo wa Mungu. Mwaandishi wa zaburi akitahadharisha watu wa Mungu wasiishi kama watu waliongooza na tamaa zao – kama wanyama wa porini. Zaburi 49:20.
Wakristo wanakumbana na hatari kuu ya kuishi bila ya kutambua uwepo wa Mungu ukihuisha maisha yao. Mungu anajua siri na mwamini anaweza kuendelea bila kufaha hili kwa kweli. Hilo pia ni la kweli kwa wale wanaotumikia Mungu. Waweza hubiri, fundisha, eneza injili bali wasifahamu Iwapo ndio basi haidhirishi kwamba kujitambulisha kwa ni pamoja na mwanadamu badala ya Mungu. Mmojawapo ya mategemeo muhimu ambayo lazima tuyarudishe kanisa ni ufahamu wa kila kazi ya Mungu ndani ya mwaamini. Sio tu mtu kutoa sadaka, kuenda kanisani na kusaidia masikini.
Tunaishi katika uwepo wa Mungu, na anatekeleza mapenzi yake mazuri kupitia maisha yetu.
“Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu; wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, hakuna atendaye mema. Toka mnbinguni, Bwana aliwachungulia wanadamu aone kama yuko mtu mwenye akili, amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, la hata mmoja. Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate. Hawamwiti Bwana” (Zaburi 14:1-4).
Kutafuta uwepo wake
Ufufuo huja wakati tunapojitahidi kurejesha mahali hasa pa Mungu katika maisha yetu. Huku tungalitujitegemea wenyewe, tunajiendeleza wenyewe na rasli mali zetu wenyewe ni utukufu mdogo. Haupo utukufu utakao mrudia Mungu.
Wakati basi tunapokosa matumaini, sisi humwita yeye. Tunapokuwa na ufahamu wa uwepo wake na kupata majibu ya maombi yake, basi kuabudu kwa kweli huanza. Hivi ndivyo Mungu hutumia nyakati ngumu katika maisha yetu ili kuturudishia ujana wetu (Zaburi 119: 23-24) Ni kipi kingetendeka, hata hivyo, iwapo tungeutafuta uso wake kila wakati badala ya kusukumwa na kuchochewa na matatizo?
Jamii zetu kwa jumla zimeanza kuwaza kuhusu maisha kana kwamba Mungu hatendi kazi. Mawazo hayo ya kawaida yapenya kanisani ambapo tunaona tofauti finyu katika ya ulimwengu na wanafikiri kuwa wamini.
- Wanadamu, wakiwemo wakristo wengi, wanaishi pasi ufahamu wa nguvu za Mungu za kimwili na kiroho.
- Pasipo kufahamu nguvu za Mungu katika maisha yetu, mioyo yetu inaganda na majivuno huingia.
- Tunapoangazia uwepo wa Mungu katika maisha yetu basi tunakuwa wanyenyekevu, wenye shukrani, wenye kumfanya Mungu kuwa ndiye mkuu na kumtegemea yeye vyema.
Tafakari Na Kariri
- Zaburi 14: 1-2
- Wafilipi 3: 17-19
Zoezi
- Kagua maisha yako uone dalili za kujitawala mwenye kando na Mungu. Je unaishi maisha ya kikristo au unaendelea na huduma yako bila haja ya msaada wa Mungu na uongozi wake kwa yale unayotenda au ilivyo? Eleza.
- Chunguza ufahamu wako kwa wanaokuzigira (waendao kanisa au la)
.