
#11 Imani Inayokua
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #11, Imani Inayokua, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Njia ambayo tunakiri, tafuta na kumfuata Bwana itadhihirisa jinsi tumekuwa kiroho. Matendo haya yanaeleza ukuaji wa kiroho kwenyewe, kama vile kurefuka, kukomaa na kuwa na nguvu ni viashiria vya kukua kimwili.
Waamani wanaotafuta uwepo wa Bwana hutumia na uhimarisha imani yao. Wale ambao hawamtafuti hawaishi kwa imani lakini waishi kwa kuona.
Waakristo wanazo changamoto mbili kubwa, kila mmoja ikihitaji kutumika kwa imani:
- Kujifunza jinsi ya kumrudia Mungu wakati mtu aangukapo.
- Bila kukoma, kumfuatilia Bwana hata mambo yakiwa ni mema.
Katika hali zote, imani inahitajika wakati mwaamini anaponyenyekeza moyo wake, akichanganya na kukiri kwa dhati, anaikuza imani yake ndani ya Bwana anapomtafuta.

Kinyume na Babake Sulemani mfalme Rehoboam hakuanza utawala wake vyema. Alikubali maoni ya marafiki wake baadala ya washashauri wenye hekima. Matokeo yake ni kwamba utawala wake ulitawanyika. Lakini hata baada ya changamoto hiyo, alipomtafuta Bwana, alibarikiwa. Ni baada tu ya miaka hiyo ya hapo mwanzo, alimgeukia Bwana.
“Wakati ufalme wa Rehoboamu ulipostawi na kwa imara, aliiacha torati ya Bwana, na Israeli wote pamoja naye” (2 Mambo ya Nyakati 12: 1).
Kifungu hiki kinaendelea kuhusisha moja kwa moja shida zake Rehoboamu alizokumbana nazo katika mwaka wa tano wa utawala wake na kutokuwa Bwana hata hivyo hakumwadhibu Rehoboamu alipomgeukia na kumwabudu tena. “Na wakati alipojinyenyekeza, ghadhabu ya Bwana ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekanakatika Yuda mambo mema” (2 Mambo ya Nyakati 12:12).
Kanuni zile ambazo Mungu hutumia kujishughulisha na watu wake, ni muhimu kwetu kujifunza lakini pia ni muhimu kujumuisha yale tunayoyapitia na taswira yote ya mpango wa Mungu wa mafundisho. Hii hutuwezesha kuelewa kwa haraka zaidi jinsi Mungu anavyojishughulisha nasi na jinsi tunavyoweza kuleta maendeleo.
Kanuni Za Imani
Vita vyetu vya kiroho hutegemea imani yetu; yale tunayoyaamini kumhusu Mungu wakati yanapohitaka. Wakati imani yetu ni dhabiti basi maisha yetu ya kiroho hukua. Wakati Imani yetu iko dhaifu tunang’ang’ana na kushindwa.
Nguvu za imani yetu ya kiroho hazitegemei habari za wakati uliyopita. Au iwapo tunaondoka vyema au vibaya. Kukumbuka ni wakati Rehoboamu alipokuwa akiendelea vyema ndipo alipoanguka. Alivunjika na alimtafuta Bwana. Kukua kwetu vyema kiroho kunategemea jinsi tunavyo muhusisha Bwana.
Hii inaeleza kwa nini tunaweza kuanguka wakati mambo yetu ni shwari au wakati tuko chini, katika kuvunjika kwetu tunaweza kumwita Mungu kwa msaada maalum na kuupata. Nguvu zetu zinategemea imani yetu iliyopo kwa wakati huu.
Mungu anataka tujiepushe na kushindwa kiroho badala yake tubaki imara. Kila mara maandiko yanatuhimiza tubaki wima. Imani iliyo imara inapaswa kujifunza mambo yote kuhusu majaribu, na jinsi ya kuangazia hali ya kubaki imara katika imani. Kujitia kati katika kila hali na jinsi mtu humtafuta Bwana huimarisha imani. Imani yetu inayokua inafunganishwa na kudhibitisha kwa umuhimu wa Mungu na kazi yake ili ikaongoze maamuzi yetu. Udhaifu wa kiroho una uhusiano na ukosefu wa imani kwamba Bwana ni muhimu kwa sehemu moja au nyingine ya maisha yetu.
Mabadiliko haya na nafasi hizi hutendeka kisiri katika mioyo yetu na mawazo. Katika kifungu kifuatacho, tutapata kelewa vyema jinsi maisha yanayovutia kutoka kwa Mungu hutegemea mambo kadhaaa ili kukua vyema. Mungu anaruhusu mambo kadhaa kuturejesha karibu naye.
Somo
- Kukua kiroho hububujika kutokana na kutumia imani yetu au kumtegemea Mungu.
- Kushindwa kiroho kunatokana na kutoaminii kwamba imani yetu ni muhimu au nzuri.
Tafakari Na Kariri
- Mambo ya Nyakati 2:12
Zoezi
- Eleza imani yako ndani ya Mungu. Unapofanya hivyo kadiri ni kiasi kipi unadhani Mungu yumo katika maisha yako, ukitumia alama ya 0 hadi 10.
- Waza kuhusu wakati ulipokuwa ukirudi nyuma. Eleza wasiwasi wako wakati ule. Je, ulikuwa ukishuku baadhi ya kazi za Mungu na njia zake?