
#18 Duara ya Maisha
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #18, Duara ya Maisha, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Mfuatano wa maisha sio tu kweli katika ulimwengu asilia mbali katika ulimwengu wa kiroho. Tulizaliwa ulimwenguni, tukapitia changamoto za kukua na kisha tukachukua jukumu ya kuwaleta wengine duniani na kuwalea. Kisha tunaondoka duniani ili kuwapa wengine nafasi.
Taswira hii nzima inatusaidia kuuelewa vyema jinsi Mungu ametupa wakati mfupi na kazi maalum ya kila mmoja wetu kutekeleza katika maisha haya. Hatuko hapa milele, wakati na nafasi ni vitu vilivyopimwa na huisha. Kiasi kile wazo hili tutalifahamu ndivyo vile tutaanza kuelewa makusudi ya Mungu ya kutuleta katika ulimwengu huu wa neema.
Ijapokuwa wakati wetu hapa duniani ni mfupi, bado kwa njia kubwa maamuzi ya maisha haya ndiyo yanaunda yetu maisha ya milele. Maamuzi yetu ya kila siku ni muhimu zaidi kuliko jinsi tunavyodhania. Jinsi vile kila mmoja wetu anashughulikia maisha haya yana ushawishi mkubwa juu ya maisha yetu ya milele. Mungu anahakikisha hilo.
Kupata Ufahamu Wote
Kufahamu upeo wote wa kukua kiroho hutupa sisi makali ya kuishi maisha yenye kusudi na utimilifu.

Hapa mna njia tatu ambazo haya hutendeka:
- Kuvutana - Kwa wepesi tunazinduliwa jinsi maisha yetu ya sasa yalivyo muhimu.
- Thahiri - Tunapata taswira yote ya maisha kuhusu yale yaliyotokea au yatakayotokea.
Baba yetu alizoea kupima kimo tulichoongezeka kwa kutia alama katika nguzo za mlango kwa kalamu. Nilifurahi kuona ni kiasi kipi nilikuwa nimekua. Hivyo ni sawa na maisha yetu ya kiroho. Kwa kawaida, waamini huchunguza jinsi wanavyokua. Baadhi yake yaweza kuwa na ushindani lakini mna matarajio mema ya kuendelea kukua hadi kufikia ukomavu. Kukua huku kutaendelea katika ulimwengu huu hata tutakapokomaa.
Shida inayotukumba zaidi iletayo ulegevu wa kiroho miongoni mwa waamini ni kwamba hawana malengo na hivyo hukwama katika maendeleo ya kiroho.
Badala ya kuangazia yale Mungu amekusudia kutenda katika maisha yetu wakati huu, wanatiwa fadhaa kwa wepesi na shida zao za kibinafsi, huku wakitekwa nyara na kiburi cha dini au wanalemewa na dunia.
Mioyo Miwili Inalia
Baada ya kusoma vitabu vya Biblia vya Joshua na Waamuzi moyoni nilipata kufahamu kuhusu vilio viwili vya dhati: (1) Kitabu cha Joshua kinaupa moyo wangu kumtumaini kuwa kazi kuu za Mungu ndani ya maisha yangu. Yote yawezekana. Hakuna kitu kiwezacho zuia kazi ya Mungu ndani yangu au kanisani, hapa nchini au duniani.
(2) Kitabu cha Waamuzi hunyenyekeza moyo wangu. Ninahuzunika vile nimetekeleza majukumu ya maisha yangu. Nimepuuza kutekeleza yale ambayo ningelifanya tena vyema sana.
Uweza wa kupata ushindi mkuu umepakana na hali ya kushindwa kwenye aibu kubwa. Kila mmoja akimkumbusha mwenziwe itawezekana. Sisi sio manusura, ingawa tumenaswa na kutokua huku kila wakati tukiwa na nafasi nzuri ya kukua. amatena, lakini kunao njia nyingi ambapo tumepuuza kanuni za maisha – kama vile katika kitabu cha waamuzi. Kile ambacho hapo awali kulitufurahisha hivi leo kimetoweka.
Hapa zipo baadhi ya nafasi za maisha. je, zako ziko wapi?
- Je unaishi na mume au mke mwenye kuchukiza?
- Je, msimamizi wako haoni uweza wako?
- Je, mtu amekupokonya mpenzio?
- Je, unanuna kwa ajili ya uzee kuwadia?
Tukitazama shida miongoni wa walio karibu nasi au katika maisha yetu binafsi, tunastahili kukumbuka kwamba tumeketi karibu na ushindi. Je, umewahi kutambua kwamba katika Biblia, nguvu za adui hazikujalisha. Hii ni kwa sababu nyakati zote, nguvu za Mungu huwa ni kubwa, na hivyo kitabu cha Joshua kikawekwa kando ya kitabu cha waamuzi kama ukumbusho kwetu.
Hatuwezi bila shaka kuyarudia ya kale, lakini tunaweza ingia katika siku za usoni tukiwa na ujasiri mwingi tukijua kwamba Bwana akiwa juu anapendezwa tuimarishe huduma – haijalishi nyakati zetu zilizopita. Mungu yuko tayari na ni mwelekevu kutuongoza leo.
Mtumishi anatuhimiza “Basi angalieni sana jinsi mnavyo enenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana“(Waefeso 5:15-17).
Wakati ni kanuni moja ya maisha ambayo inatuhusu sisi sote, kwa nasaha, kwa neema ya Mungu na unyenyekevu na moyo unaomtafuta na pia unaweza kutufidia wakati uliopotea. Kutengeneza mvinyo huchukua muda kwa ajili ya kuuacha uchache, lakini Yesu aliyabadilisha maji kuwa divai papo hapo.
Fafanua uko wapi katika ramani ya maisha ya kiroho? Tazama mahali unapostahili kuwepo. Mtafute Bwana akufikishe mahali unapostahili kuwa na jizatiti kuzaa matunda kwa ajili yake katika maisha yako.
Somo
- Upungufu wa wakati unatutia hamu ya kutambua mahali ambapo tu katika ramani ya kukua kiroho na kutushawishi kusonga mbele.
- Mungu anataka kwa utaratibu kufanya kazi katika maisha yetu lakini kuendelea kukua na kukomaa ni mambo muhimu.
Tafakari Na Kariri
- Waefeso 5:15-17
Zoezi
- Onyesha uko wapi katika ramani ya kukua kimaisha. Je, unajiona uko wapi?
kwa utaratibu ufaao.
- Tambua jukumu moja, mpango, jambo, maendeleo na kadhalika ambao litakusaidia kuangazia ili kukubali mabadiliko yanayohitajika ili kukua binafsi. Andika ni vipi na ni lini utatekeleza haya. Zungumza na Bwana
kuhusu haya tena (Methali 3:6).