
#25 Lenga kwa Makini
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #25, Lenga kwa Makini, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Kama waalimu na washauri, nusu ya tatizo letu ni kujua ni nini ya kusomesha na nusu ya pili ni kuwahimiza wanafunzi wetu kujifunza katika kila hali. Hata hivyo upungufu wa wakati huchangia changamoto za kuwafunza wengine vyema.
Mpango wa Mungu wa kukua kwa kiroho unaendelea kutenda kazi. Tunaweza kumwamini yeye kutekeleza jukumu lake. Lakini tuna nguvu za kutosha kupingana na nguvu za ibilisi zinazozidi kuongeza? Bila shaka twaweza. Tatizo limo kanisani kwa kutotekeleza wajibu wetu ipasavyo.
Twahitaji kufikiria upya jinsi tunavyofunza watu wetu, wawe wana mfumo wa masomo iliopangika kama vile vyuo vya Biblia na kanisa vile vile katika mfumo usiopangika hapo nyumbani au moja kwa moja. Mara tu tutakapopata mtazamo dhabiti ndipo tutakapofaulu. Mipango yetu ya awali ya kufunza wale ambao wanao hulalama kuhusu shida za hao viongozi.
Shida sio kwamba kama tunaweza kushinda, Yohana anasema kwamba sisi tu zaidi ya washindi – hata waamini wachanga. Hii ndiyo imani ambayo itatubidiisha vyema na kumwongoza mwalimu na yule mwanafunzi. Lakini katika visa vingi, wanafunzi hawana imani hii. Katika hali hii imani ya mwalimu sharti iwe ya kutosha kwake na kwa mwanafunzi pia.

Hebu waza kuhusu darasa la wanafunzi wapya. Ni kiwango kipi cha ukuaji kilichoko katika tabia yako, ufahamu na ujuzi wao? Mwalimu anahitaji kudukua malengo ya somo hili na kulivunjavunja ili liweze kusomeshwa vyema – wakati mwingi darasa la mara moja.
Kwa sababu wakati na wanafunzi umeadimika hivyo twastahili kuchagua kwa makini mada zetu na vitabu vya kusomea. Ni nini twaweza kuwaza kuhusu wanafunzi? Wameendelea kiasi kipi? Wastahili kuwa wapi baada ya masomo? Au kwa upeo mkubwa, washiriki hawa wastahili kuwa wapi baada ya miaka mitano hapa kanisani au wanafunzi wapaswa kuwa kiwango kipi wakati wa kuhitimu?
Je, Ni Vyema Kujifunza Kuhusu Biblia?
Twadhani kwamba mafunzo mema ya Biblia yatosha kwa wanafunzi wanaoingia katika huduma ya kila wakati. Bila shaka, hilo ni kweli. Hivyo, waalimu wanajishughulisha na kuunda masomo yao kama vile utangulizi wa agano jipya. Jinsi wakati unavyoruhusu masomo maalum kama vile injili ya Yohana yanaongezewa.
Hili ni nzuri lakini ndilo lililo bora? Tunapoangalia mahitaji ya kawaida ya mwanafunzi kama vile, haja ya kufahamu Biblia, ina maana sana. Nilikutana na mwinjilisti mmoja kutoka India ambaye alikuwa amehuzunika sana kwa Katika vyuo vyetu vya Biblia, tunazo shahada za uchungaji na upelekaji wa injili, vijana au mshauri. Lakini wanasimulia yale watayokuwa wakitenda na wala hao ni nani. Kiini cha maisha chakosoa mtazamo huu kwa sababu unahitaji ukaguzi wa ndani wa yale mwanafunzi na jinsi anavyojifunza. Punde tutambuavyo jinsi Mungu hufunza ndipo tutaweza kushirikisha vyema mipango yetu na yake.
Lengo yetu sio kukashifu mafundisho yanayotuzingira; Wengi, mimi
nikiwemo, tumefaidika na masomo waliotufunza. Hata hivyo twahitaji kunoa maono yetu. Malengo yetu mara kwa mara huwa ni sawa, lakini hayahusiani na malengo makuu ya Mungu na makusudi ya kusomesha.
Huku tukiendelea kutumia mifano ya masomo ya kimsingi ya Biblia, twahitaji malengo makubwa kuliko kuendelea kupata ufahamu wa Biblia pekee. Hapa yamo mambo machache ya kuwazia.
- Hatuwezi tukajivunia ufahamu wetu wa neno la Mungu.
- Twaweza jifunza vibaya neno la Mungu na hivyo likose kutusaidia maisha yetu ya kiroho (kwa mfano mafarisayo).
- Twaweza pia kusoma neno la Mungu hata lianze kubomoa imani yetu (masadukayo ambaye hawakuamini kuhusu ufufuo)
- Twahitaji kujifunza neno la Mungu kwa njia bora hata tukaweza kumsikia Mungu akinena nasi.
- Twahitaji kujifunza neno la Mungu ili tukatambue jinsi linavyoingiana na changamoto zinazotukumba.
- Twaweza jifunza kwamba Mungu huongoza imani yetu tunapozidi kulifahamu neno lake.
- Ni lazima tuwe na moyo uliotayari ili tukajifunze yaliyo katika neno la Mungu.
mwanafunzi. Yesu anataja haya vyema kabisa.
“Nyinyi kusukia mtasikia, wala hamtaelewa; kutazama mtatazama, wala hamtaona. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, na kwa masikio yao hawaskii vema, na macho yao wameyafumba; wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, wakaongoka, nikawaponya” (Mathayo 13: 14-15).
Hatustahili kudhani kwamba ufahamu wa Biblia pekee utatusaidia ilhali mara nyingi huwa ni kinyume. Hata maziwa yaliyo bora kabisa huaribika na kuchacha. Wanafunzi wetu wanahitaji “kufahamu na mioyo yao na kumgeukia Bwana”, hakutakuwa na uponyaji na mafunzo ya kweli.
Je si shida ingali ndiyo kubwa makanisani mwetu? Neno halisomwi ili lilete mabadiliko mbali kwa ajili ya kutumbuiza. Watu wamepoteza matumaini ndani ya neno la Mungu kuweza kubalisha au kuleta mabadiliko halisi katika maisha yetu. Wakati halisi wa kuabudu hauwaongozi watu wa Mungu kuishi maisha matakatifu. Ni kwa sababu hawajaingia ndani ya uwepo wa Mungu au kulisikia neno la Mungu? Mengi yanastahili kutendwa ili kuiandaa mioyo ya watu wa Mungu vyema.
Somo
- Mafundisho ya kiroho lazima yashirikishwe katika mafundisho yetu yote. Umuhimu wa malengo ya kiroho lazima ushinde umuhimu wa masomo.
- Nyakati nyingi waalimu wamekosea kwa kudhani kwamba elimu ndiyo haja kuu ya wanafunzi.
- Mafundisho yetu ni lazima yakaguliwe kuingiana na utaratibu wa mafundisho ya Mungu, la sio hivyo nafasi zetu zetu kutoa mwongozo zitapotaa.
- Mathayo 13: 14-15
Zoezi
- Umewahi kusoma masomo ye yote yanayohusiana na Biblia? (hata ya shule ya Jumapili)? Ni nini kilichofanya madarasa mazuri kuwa madarasa makuu? Ni nini kilifanya madarasa mabaya kwa maovu?
- Je unahisi kuwa masomo au mafundisho yako yalikuaandaa kwa huduma? Eleza vipi.
- Ni vipi yangeboreshwa Zaidi?