
#30 Kuwaandaa Waamini Wachanga
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #30, Kuwaandaa Waamini Wachanga, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Wachanga
Hebu tuzungumzie mafundisho ya waamini wachanga. Kila mtoto mdogo atakuwa mkubwa kimwili lakini wengi huwa na wakati mgumu kukomaa.
Wanaweza kutofahamu mambo mengi, hasa iwapo watakua katika nyumba zisizo na upendo. Iwapo wamechomokea katika mabaya, shida zao zitakuwa nyingi. Lile ambalo ni kweli kuhusu kimwili lafaa kwa waamini wachanga kiroho.
Baada ya kufundisha na kuzungumza na watu wengi tukiwatayarisha kwa huduma, nahisi kwamba sio wachache ambao huenda vyuo vya Biblia ili kushughulikia shida zao wenyewe. Wanadhani kwamba theologia itawafanya shida zao binafsi zitokomee. Wangalipokea mafunzo ya jinsi ya kuyashinda matatizo yao, kanisani na kisha sasa kuingia katika mafunzo rasmi, kwa sababu ya mwito.
Kwa nasaha mbaya, mafundisho wanayohitaji kwa hatua hii ya pili ya mafundisho haipo katika makanisa mengi. Kwa sababu hiyo, katika vyuo Ninawaza iwapo wale huketi katika madarasa hayo husaidika kwa kweli. Sababu ni kwamba pana ukosefu mkubwa wa imani ya mahali wakristo wanapaswa kuwa, au jinsi ya kufika hapa. Washauri wengi hufundisha kwamba mtu anastahili kuvumilia kiasi fulani cha hasira na wasiwasi, lakini hii ni kuchukua msimamo uliotofauti kabisa kutoka tuliopewa katika Biblia. Tunahitaji kumaliza hasira sio tu kuishughulikia.

Mungu yuna malengo na njia yake, lakini kanisa bado halijakubali malengo ya Mungu na halitegemei njia zake ili watu wake wakue. Shida haitokani na ulimwengu ambao waamini wapya wametokea lakini ukosefu wa imani kanisani na katika viongozi wake.
Mungu anapenda watu wake wote wapokee mafundisho makubwa ili wakaweze kukua na kuwa watu wenye nguvu na wema. (Waefeso 4:15-16). Mafundisho haya hayapaswi kuachiwa wataalimu wenye vyeti vya serikkali katika ushauri. Waamini waendelea kuwaza kwamba mtu unahitaji shahada ya uzamifu ili aweze kusaidia mtu mwingine aweze kikabiliana na shida za kimsingi katika maisha. Hili ni kosa.
Ingawa makanisa yapaswa kuwa yakiwafundisha watu wake, wengi hawatendi hivyo na kwa sababu hii maelezo haya yanahitajika, katika shule za Biblia na vyuo. Kile ambacho mchungaji, au mumishonari, au mwalimu wa kikristo, au mtenda kazi wa vijana, au wale ambao hawajaoa au kuolewa, mke, na kadhalika, hawahitaji kufahamu au kuishi maisha ya haki? Sote twahitajika kuishi maisha mema ndio shina ya kuhudumu katika Kristo. Twayahitaji mafunzo haya ili tukaweze kuhakikisha watu wote wa Mungu wako na nguvu na afya kiroho.
Viongozi pia wanahitaji mafundisho jinsi kiini cha maisha kitahusishwa katika huduma zao za mafunzo. Wanahitaji kukubali malengo ya Mungu ili kuishi
- Aandaliwe kabisa ili kuweza kutambua majaribu.
- Afahamu shida kuu katika majaribu
- Atambue jinsi majaribu uhusiana na hali ya dhambi zao na ulimwengu
- Apate na kutumia ukweli ili kupigana na majaribu
- Tambua sehemu ya msamaha katika mioyo yao
- Shuhudia binafsi nguvu za Roho wa Mungu.
Mtume Yohana alitaja ukweli: ‘vijana mmeshinda yule mwovu’. Watu, waume kwa wake wa Mungu ushindi wao umehakikishwa. Tunaporuhusu nguvu zote za neno la Mungu katika maisha yetu, imani yetu hutiwa nguvu na tunawezatambua uongo wa shetani kutekeleza ukweli na kusimama imara.

“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu” (1 Yohana 5:4).
Tena twastahili kusisitiza kwamba haya yote ni sehemu ya utaratibu ulio mkubwa wa kiina cha maisha. Maisha ya kiroho yalitolewa kwetu ili tuweze kushinda dhidi ya majaribu (ingawa hilo sio lengo letu kuu). Washauri wengi Yesu Kristo. Mungu anataka ushindi kila wakati. Ni sharti tukome kumpa yule mwovu sehemu ye yote katika maisha yetu.
Manufaa Ya Mafundisho
Kutoka mwanzo, bila shaka, twahitaji kurejelea daima nguvu za msalaba ili kupata msamaha na urejesho. Hii ni kwa kifupi kutukumbusha kuhusu neema ya ajabu ya Mungu.
Kama mwamini anavyostahimili vita baada ya vita, hata hivyo anaanza kuona jinsi yule mwovu humlemea na kumshinda. Mafunzo katika kiwango hiki yanastahili kuangazia jinsi ya kupinga hila za yule mwovu kupitia nguvu za neno la Mungu ili kusimama imara.
Kwa kutekeleza mafundisho haya kwa kila mwanafunzi, mshiriki wa kanisa, mhudumu, na kadhalika, tunaikuza imani ya kila mwamini. Hii sio tu kukiri ‘ninaamini’ mbali ni kujifunza jinsi ya kulichukua neno la Mungu na kulitumia ili kumshinda yule mwovu.
Je, haya sio makusudio ya kwa maisha ya kila mwamini? Ni kwa nini waamini wengi hawapiti kiwango hiki. Wachungaji na walimu wengi huniambia kwamba wangali katika hatua hii ya pili. Iwapo wangali hapo, basi hawajakomaa katika imani yao ili kuwafunza wengine jinsi ya kukwepa hasa katika nyanja walio na udhaifu. Kinacho haribu hali hii zaidi ni wale viongozi ambao hawajashawishika kwamba inawezekana kuishi maisha mwema na kuyashinda majaribu.
Kujifunza Jinsi Ya Kufunza
Waweza kuwa unashangaa jinsi ya kufunza mambo haya? Ni wapi twaweza jifunza jinsi ya kutekeleza tabia na tamaduni hizi? Mafundisho yana Kanuni za msingi zaelezwa katika vifungu vinne vya kwanza vya kitabu chetu ‘Reaching Beyond Mediocrity; Being an Overcomer’. Hili limejengwa juu ya wazo kwamba Mungu ameshatufanya kuwa zaidi ya washindi na kwamba Mungu anafanya kazi kwa niaba ya vita hivi vya kiroho ambavyo twajihususha navyo ili kuangaza utukufu wake. Vifungu vya mwisho vinatumia kanuni hizi kuonyesha jinsi ya kututia nguvu kuzishinda shida za kubunafsi kama vile hasira, tamaa na kiburi.
Iwapo mtu hatajifunza jinsi ya kukabiliana na “dhambi ndogo”, dhambi hiyo zitamumiliki kisha zimumalize kabisa. Hebu waza kuhusu hayo. Ulinzi unahitajika kutendeka katika moyo kupitia neno la Mungu. “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” (Mithali 4:23).
Mafundisho haya hayachukuwi muda mrefu. Kama vile mtu astaili kukuwa akipitia miaka ya kubalehe, mwamini mchanga anastahili kukua hadi kufikia ukomavu katika miaka michache.
Mara nyingi nimesema huchukua yapata miaka mitatu kupitia hatua hii kanuni hizo zafahamika vyema iwapo mwanafunzi ana ufahamu wa neno la Mungu. Tatizo sio wakati au gharama. Tatizo kubwa ni kushawishi walimu na wachungaji kwamba hilo ndilo Mungu anataka watende na anaweza kutenda kwa urahisi hatupendekezi aina fulani ya miujiza au uchawi ya uponyaji kufuatwa ila tunatia kanuni za Biblia ambazo zatenda kazi.
Kufafanua Maono Yetu
Waza kwa muda. Ni nini mawazo yako kumhusu mwamini wa wastani? Je, wadhani wakuwa kufikia kukomaa kwa ukamilifu? Je, wanaweza kuyashinda majaribu ya kila namna? (Hili ni tofauti na yale tunayoyaona makanisani mwetu).
Je, si huo ungekuwa ni ujumbe mwema? Kanisa hili ni vuguvugu kwa sabau limekata tamaa kwamba mabadiliko halisi yaweza kutokea.
Ni watu wa namna gani wanaohitimu kutoka vyuo vyetu na shule za Biblia? Ni viongozi wa namna gani tunaowatoa kutoka makanisani mwetu? Je, tunaridhika na ukomavu wao wa kiroho? Katika hali nyingi majibu ya maswali hayo ni ‘la’. Jibu ni rahisi. Hatujawafunza kwa namna ambayo neno la Mungu linatuongoza. Kutokana na kutoamini na kushindwa walikojifunza, watawafunza wengine kutokuwa na ushindi katika maisha yao ya kibinafsi. Ni muhimu viongozi wetu kujifunza kuishi kwa ukweli wa neno la Mungu na kuwafunza wengine kufanya hivyo.
Makanisa yetu yako matatani sio kwa sababu hayawezi badilika mbali kwa sababu yanaamini hayawezi kubadilika. Ingawa mazoea huongeza vizuizi zaidi kuweza kushinda, vile vile vyaweza rukwa kama tunavyotekeleza kanuni hizi katika mioyo ya imani.
Kutekeleza Maono Ya Mungu
Tutatekelezaje mambo haya shuleni na makanisani mwetu? Baadhi ya maelezo yanaweza someshwa katika madarasa, lakini vikundi vidogo na ushauri ni muhimu kutambua shida za mtu binafsi na kuweza kuonyesha jinsi mpango wa ushindi hutenda kazi.
Mara nyingi watu hawapendi kukiri unyonge wao na dhambi zao hadharani.
Huenda wasiwe na shida kuzungumza kuhusu aina fulani za dhambi, lakini zingine zimefichika, hata mawazo yaliyo kinyume na ya dhambi, marejeo mengi ya dhambi kama vile roho ya kutosamehe, yamekita mizizi katika maisha yetu mapema tangu utotoni hivyo mazoea yetu yanazima dalili za uchungu, kujitoa, kuhisia na kutoamini. kushindwa na kupungukiwa badala ya ushuhuda na ushindi upande ule mwingine nimeshapata kuona maajabu yatokanayo na nguvu za ukweli ukitenda kazi maishani mwangu na ya mwingine. Ushindi wa kibinafsi huchangia pakubwa kuanzisha mafundisho murwa. Hauwezi toa kitu usichokuwa nacho. Shule za huduma pamoja na makanisa sharti waanzishe wakufunzi wenye ushindi ili kutekeleza mpango wa 2 Timotheo 2:2.
Mungu anatushangilia tufikie ushindi. Ametenda hivyo ili tukaweze kuwa washindi, sasa twahitaji kumtii yeye, tukue katika hatua hii na kufikia kukomaa kwani huko ndiko aliko na mipango mikubwa kwa ajili yetu. Ubora na wingi wa huduma zenye mazao kunategemea kwa ukubwa jinsi tutakavyotenda katika hatua hii ya pili.
Iwapo kanisa litakuwa na kweli hizi zimetangamanishwa na mafunzo ya waamini wote, watu wa Mungu wangekuwa wenye nguvu katika imani yao. Ufufuo ungekuwa umefika. Familia zinerejeshwa. Tungekuwa na viongozi wengi wakubwa. Pasipo kufinyangwa vyema kwa roho na mawazo, ingawa wanaongeza shida zetu, huku njia za giza zake yule mwovu zikinyemelea maisha yetu. Mafunzo ya kweli lazima yahusishe kuimarisha maisha mema yenye nguvu pasipo hivyo hamna upendo wa kweli.
Somo
- Waamini wengi huedeleza maisha kana kwamba wameshindwa kwa sababu hawajaguswa na nguvu na utukufu wa neno la Mungu linalofanya kazi katika maisha yetu.
- Mungu ameipa kanisa mbinu za kuishi maisha matakatifu kwa kuishinda dhambi kila wakati na kusisitiza ukweli wa msalaba kwa kushindwa kwake.
- Mafunzo lazima yatoke kwenye viongozi ambao wameona nguvu za Mungu zikitenda kazi maishani mwao.
Tafakari Na Kukariri
- 1 Yohana 5:4
Zoezi
- Tambua unyonge mmoja katika maisha yako na hatua zinazohitajika kuushinda. Je, unajishughulisha kulishinda shida hiyo? Je unaweza kuwasilisha mpango huo kwa wengine.
- Taja dhambi kadhaa kubwa ambazo waziona kwa wengine. Eleza hatua zinazohitajika kuwasaidia kila mmoja wao kupata matumaini na imani ili watoke kwenye hizo dhambi.
- Je, kanisa lako au shule yako huvumilia kutokomaa na tabia/ mambo ya dhambi kati ya viongozi wanaowaandaa. Shida hii inawezatatuliwa vipi?