
#32 Kuwaandaa Waamini Waliokomaa
Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha
Muhtasari: Kifungu #32, Kuwaandaa Waamini Waliokomaa, kutoka sehemu ya Chanzo cha Maisha na Kiini cha Maisha katika Kiini Cha Maisha.
Waliokomaa
Kuwafunza wale walio katika hatua ya ukuaji wa kiroho wa Mkristo ni tofauti kabisa kutoka kwa hatua za kwanza mbili.
Mtazamo wa hatua za kwanza mbili ni kuwasaidia waamini kuzipitia viwango hivyo. Kulingana na Yohana katika 1 Yohana 2:12-14, hamna hatua ya nne katika kuwepo kwetu hapa duniani. Ukweli huu utabadilisha jinsi tutakavyojadili ukuaji katika kiwango hiki. Kua hivyo katika kiwango cha kwanza na cha pili, mwamini anazingatia malengo ambayo yatamwezesha kuingia katika hatua hiyo nyingine katika hatua ya tatu, mwamini anakubali malengo yanayoleta maendeleo ya kiroho katika kiwango hicho.
Kunazo hatari katika kiwango hicho. Twaweza fikiria kumhusu huyo mzee ambaye amekuwa katika usukani kwa miaka ishirini au zaidi katika kanisa lake na ‘amekwama’ kiroho katika ukuaji wake kiroho. Au waza kuhusu mwamini ambaye anadhani kuwa mwaminifu ni kuketi kwenye kiti kile kanisani kwa (Hesabu 20:11-12)
Shida hizi zawezatatuliwa kwa kufahamu ukuaji vyema katika kiwango hiki cha tatu cha maendeleo ya kiroho. Maendeleo ya kiroho yataendelea kujidhihirisha jinsi tunavyotafuta kudumisha na kukua katika uhusiano wetu na Mungu kupitia Kristo. Hata watu wazima hukua katika kukomaa, hekima, huruma na kutimilika ndani ya Kristo (Waefeso 4:13).

Kudumisha Ukuaji Wetu
Ijapokuwa neno kudumisha halionyeshi juhudi ya maendeleo, linadhihirisha udhabiti mkuu wa baadhi ya nidhamu za kiroho katika maisha ya mtu binafsi. Maombi kwa mfano, uhusiano huo wa mazungumzo ya dhati na Mungu waweza na unastahili kukua. Kama vile masomo ya Biblia ya mtu binafsi, wastahili kukita mizizi.
Hii inatuonyesha ni wapi tunaweza shawishika kuyumbayumba, kuingia katika hali ya vuguvugu au kutotii kunatumika kama maeneo ambayo tunaendeleza kujitolea kwetu kwa malengo ya Mungu katika maisha yetu. Wale walio katika kiwango hiki cha tatu wanaulizwa mara kwa mara na Bwana, “Nini au nani aliye wa umuhimu zaidi kuliko vyote katika maisha yako?” Majibu yetu yanadhihirisha iwapo tunamtafuta bwana na moyo wetu wote au la.
Kunao wafalme wachache ambao walitenda vyema mwanzoni mwa utawala wao kisha baadaye wakawa wenye kiburi na wa kuabudu sanamu. Hatari hizi ambayo inatuhimiza “kushikilia” kiasi cha ukuaji ambacho tumeshapata.
- “Na tushikilie sana ungamola Tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu” (Waebrania 10:23).
- “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubalika na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Timotheo 2:15).
- “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako” (Ufunuo 3:11).
Mwamini aliyekomaa anapaswa kuwa makini kuwa na moyo wenye bidii kwa Bwana. Hili ni gumu. Atakumbana na nyakati za kuvunjika moyo, kustawi, shaka, nguvu, huzuni, kujulika, msiba, maumivu nap engine mateso. Kila hali inatokea kwamba tunahitaji kuchukua ukweli wa jadi na tena kujitolea kuishi njia za Mungu.
Jambo kuu kuhusu maisha ya kiroho ni kwamba hamna mwisho kwa uwezekano wa kukua. Paulo anautaja vyema.

“Sio kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamlifu; la!Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu” (Wafilipi 3:12).
Paulo anatambua kwamba maendeleo yake ya kiroho sio tu yake pekee mbali ni ya Bwana kuyatimiza makusudi yake kupitia maisha yake kwa ajili ya wengine (Wafilipi 1:22-24). Anataka kuyatimiza yale yote, makubwa kwa madogo, ambayo Bwana alimpangia.
Ukamilifu Katika Kiwango Cha Tatu
Tunapowaza kuhusu himizo la Yohana katika 1 Yohana 2:12-14 kwa hatua zote tatu, tunaanza kuangazia kuhusu ukuaji unaotendeka katika kiwango hicho cha ukuaji wa kiroho. Hili pia ni kweli katika kiwango hiki cha tatu cha aishi ndani yetu akitekeleza malengo yake ndani ya maisha yetu.
Kunyauka hutokea iwapo hatutakuwa waangalifu. Huduma inakua mazoea na kukauka iwapo hatutajiburudisha wenyewe ndani ya Bwana. Tazama jinsi Paulo anawakumbusha Wakristo huku Rumi.
“Kwa bidii, pasipo ulegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana” (Warumi 12:11).

Kusudi ambayo sisi huvumilia mambo haya haipaswi kusahaulika tuwepo katika shughuli kali au nyakati za kukata tamaa. Yesu ndiye kielelezo chetu, akituonyesha uhusiano katika hali ya kujitolea na huduma.
“Mimi ndimi mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu name ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi h a m w e z i k u f a n y a n e n o lolote” (Yohana 15:5).
Kila jina linatukumbusha kuhusu
uhusiano wa dhati ambao ni sharti tudumishe iwapo tutaendelea kuishi maisha ambayo Mungu anatenda ndani yetu kwa kusudi fulani.
Kuangazia Vitabu Vya Mafundisho
Mafunzo katika kiwango hiki yanahitaji kukuza maono ya jinsi shetani na werevu wake, anawajaribu waamini hasa wanaokuza uhusiano wao na Bwana. Kutoka hapa twapata kujitolea na uaminifu wa hali ya juu. Mara nyingi waamini wanashindwa kuweka wakati maalum wa maombi. Kutokana na hayo wakua mbali na Mungu na hawezi kukua. Mafunzo mema husaidia.
- Mbinu ya kurejesha vyema wakati mtulivu baada ya kulegea.
- Mbinu ya kupata mwongozo katika vifungu vigumu.
- Njia na kumsikiza Mungu kupitia kwa maandiko.
Nyingi ya hatua hizi haziangazii kanisa la kawaida au mafunzo ya chuo cha Biblia. Tunawalaumu watu kwa kutojua vipi, badala ya kutoa mafunzo makubwa ya Bwana, ambayo yeye mwenyewe angependa kuwapa.

Mtazamo maalum unahitajika katika eneo lote la uzalishaji wa matunda. Ukomavu huzaa matunda. Yesu atuhitaji tuzae matunda na pia tudumu katika hilo (Yohana 15:16)
Nyakati nyingi twapima huduma zetu na kiasi cha matunda tunayozaa. Hili ni nzuri, lakini ni muhimu kuwa na mtazamo mpana katika kiwango hiki cha tatu. Kumbuka kwamba matunda hayapo katika kila kiwango ukuaji wa kikristo kama vile mtu avumiliavyo mateso. Tunda lililotokana na mateso ya Yesu liliweza tu kudhihirika baada ya kufufuka kwake.
Kunavyo vitabu vingi vizuri vya kukuza juhudi za kikristo na kuimarisha huduma zetu. Hii ni baraka kubwa katika kizazi chetu kwamba twaweza ‘kukutana’ na waamini wengine wenye nguvu kupitia kwa mafundisho, vitabu video na kanda. Twaweza hitaji vitabu vya kusoma, mafunzo yanahitajika, lakini tunapoingia katika uhusiano wa dhati na Kristo, tutaona kwamba baadhi ya masomo muhimu hayawezi jaribiwa au kusawazishwa. Hii bila shaka ni sababu moja yanapuuzwa shuleni.
Mtazamo Wa Kufaa
Ushauri katika kiwango hiki ni mwema ukiwepo katika vikundi vidogo vidogo au mmoja-kwa-mmoja. Mazingira ambayo kila mtu anaweza kuzungumza. Jambo kuu kuhusu uanafunzi ni kwamba wakati mwanafunzi Kwa mfano, katika kiwango cha tatu, mpate ndugu mmoja au wawili (dada kwa dada), tafuta hoja moja inayofanana. Mara nyingi, mimi humwuliza mtu ni eneo lipi angependa kukua na vile nami ningependa ukue katika eneo lingine (kwa mfano kumsikiza Mungu, kuchambua Biblia, na kadhalika). Wakati umegawanya kati ya kuomba, kushiriki na kushauriana katika maneno mawili. Mtu anaweza kutana na mtu mwingine mahali po pote na wakati wo wote.
Katika vifungo vifuatavyo, tutaangazia zaidi katika maendeleo haya na yamaanisha nini kuwa katika masomo rasmi katika taasisi za mafunzo, na pia hali zisizokuwa rasmi kama vile makanisani, ambapo hamna shahada (na pia hamna karo).
Somo
- Kiwango hiki cha tatu cha ukuaji hutofautiana na zile za awali kwa sababu lengo lake ni kunawiri ndani ya kitengo hiki badala ya kupitia.
- Hatari zinazotishia ukuaji wetu zaweza zuiwa kwa kuangazia yale Mungu anatenda kupitia katika maisha wakati wo wote ule.
- Mafundisho ya kikristo ni lazima yatende zaidi ili kuwaandaa waamini kukua katika hatua hii ya tatu ya maendeleo.
Tafakari Na Kariri
- Wafilipi 3:12
Zoezi
- Andika hadithi tatu za maisha ya kikristo (yako na wengine) ambayo zimekusaidia katika ukuaji wa kiroho. Eleza jinsi kila moja ilikusaidia.
- Je umewahi kukabiliana na ‘kunyauka’ – imani imekauka na kadhalika. Chagua kisa kimoja na tafakari jinsi kilivyotokea. Hatimaye matokeo yake yalikuwa aje?
- Je, wewe uko katika hatua ya tatu ya ukomavu? Eleza. Ni nini changamoto kubwa unazozipitia ili udumishe imani kubwa?
- Je, umeshauri mtu ye yote katika kiwango cha tatu cha maendeleo ya kiroho? Ilikuaje?
Mwanzo wa Maisha na
Mafundisho
Kifungu #33-40