
#14 Udadasi
Mwanzo wa Maisha na Wewe
Muhtasari: Kifungu #14, Udadasi, kutoka sehemu ya Mwanzo wa Maisha na Wewe katika Kiini Cha Maisha.
Mara waamini wasikiapo kuzihusu hatua hizi tatu, na kutambua kwamba hakuna hatua ya nne, waanza kuwaza wamo katika hatua ipi. Ni sawa na kuonyesha watu picha ya mandhari au matembezi. Macho yetu yana tabia ya kuchungua yenyewe. Je mimi nipo wapi kwenye picha? Ninafanana aje?
Wakristo huku wamejawa na upekuzi wa maisha yao wenyewe, wanataka kujua umbali waliofika. Waamini wengi hawajawahi kusikia kuzihusu hatua hizi za kuendelea kiroho, hivyo kuchochea hata hamu zaidi kwa wale yenye imani ilivyovuguvugu. Bwana pia ametumia mifano ya familia ambayo kila mwamini anaweza kuifahamu, kuikumbatia na kuwapa wengine kwa urahisi.
Tunapozungumza kuhusu hatua hizi, kunayo hatari kwamba mtu mmoja
atajiona kuwa mkubwa au mwenye dhamana kuliko mwingine, hata kuwaza kwamba anastahili kuwanyoosha wengine (waweza waita msimamizi wa kiroho). Hii sio maana ambayo Yohana aliyonayo katika mawazo yake.
Badala ya kujilinganisha na wengine, tunapaswa kujitambulisha ni umbali upi nguvu za Roho Mtakatifu zimetuwezesha kuangaza mfano wa Kristo. Yote ni kiasi kipi tumekua na ni njia zingine zipi twapaswa kukomaa zaidi. Tuwaze maisha yetu kama ya kijana mdogo ambaye anatamani atakapokomaa anataka awe kama baba yake.

Maono Mapya Ya Kukua Yahitajika
Waamini wengine, badala ya kuona ukuaji wenye afya, wameangukia ulegevu wa kiroho. Hawakui. Hawajui hata kwamba wanapaswa kuendelea kukua. Au iwapo hawafahamu hili, wanahisi wameshindwa. Wana shida katika maeneo kadhaa ya maisha yao na kiasi kikubwa wamekata tamaa ya kwamba waweza kuwa tofauti na jinsi wavyojiona sasa. Wanadhani kuwa hapa ndipo watakaposalia.
Zaidi kama kuuelekeza mzabibu unakua hata utakapotambaa, ndivyo hivyo twapaswa kuyaongoza mawazo yetu. Tunapounganisha ufahamu wetu wa maisha ya Mungu yenye nguvu pamoja na kusudi maalum kwetu katika kila hatua ya maisha ya kikristo, basi twaweza inuka zaidi katika kuendelea kwetu kiroho.
Kama vile kukua kwahitaji bidii kwa maisha yetu ya kawaida ilituwezesha kufikia utu uzima, vivyo hivyo pia katika maisha yetu ya kiroho, kuufahamu ukweli huu huongeza imani yetu na kusababisha tukue kiroho.
Msururo wa mawazo ambayo hujenga matarajio yetu ya kiroho kwaweza kuwa hivi:
- Roho Mtakatifu bado yungali ananivuta nipate kuendelea kiroho kwa ukamilifu. Bado hajakata tamaa nami.
- Aaaah, ni wapi nilichukua mkondo mbaya?
- Mungu yuna mpango nami.
- Mungu amenitayarisha kukua hadi kukomaa.
- Ni hatua ipi yangu ya kuendelea kukua?
- Ni vipi naweza kuendelea kukua?
Haya ni mawazo machache ambayo yamesababishwa na mafundisho mema ya neno la Mungu kwa maisha ya kiroho. Ukweli huu unamrudisha mwamini hadi mkondo mwema ambao imani yao ndani ya kazi ya Mungu itawashwa tena.
Tumaini Lilnalokua
“Unamaanisha unataka niwe kama Yesu? Utanisaidia kuelewa ni kipi ambacho kwa kweli kinamaanisha kwangu, na utanionyesha njia kuelekea
huko? Je ni hatua ipi kwangu?”
Mawazo haya yanazaa imani, matarajio yakiwa mwamini anaweza na anastahili kukua zaidi kiroho.
Sasa wanawaza kuhusu kuendelea kiroho na kuanza kuangalia malengo Mungu ameweka kwa niaba yao badala ya matatizo ambayo yamekuwa yakiwakumba. Matumaini ya mabadiliko huanza kurejea. Pamoja na ongezeko la imani, wanayo matumaini kwamba Mungu atawasaidia kuendelea kukua.
Kila mwamini, hatua kwa hatua, inamaanisha huendelea kukua hadi kukomaa kabisa kupitia kila hatua ya maisha ya kiroho. Baadhi ya wengine huenda wakapinga mafundisho haya, lakini ndiyo yanayofundishwa hapa katika Yohana 2:12-14. Shida kubwa katika kushukiwa huku ni mawazo yetu yenye makosa kuhusu kukomaa. Hakuna awezaye kuwa mkamilifu bila dhambi. Sisi sote tumeshatiwa mawaa, lakini twaweza ona maisha yetu yamebadilishwa na maamuzi ya kila wakati yanayoleta utukufu kwa Mungu. Hebu tambua maneno ya Yohana yanavyoleta wazo hilo.
“Watoto wadogo nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na
kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo
tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake” (1 Yohana 2:1-3).
Wakati waamini wanaanza kuwa wadadisi, hawako tayari kujifunza na kukua (waalimu wajua jinsi uelekevu ni muhimu kwa wanafunzi wao). Ni tofauti na mawazo ya mwaamini ambaye anadhani ameshafika (sijui hiyo yamaanisha nini) kwa kuja kanisani miaka kumi na mitano.
Maisha sio jambo tunapaswa kuyafanya yakue. Hukua peke yake. Kama vile chipuko la mmea, twahitaji kuutunza mmea huo mdogo na kuupa vitubishi vifaavyo kama vile maji, samadi na jua. Hatufanyi maisha au hatusababishi kukua lakini twapalilia na ndivyo ilivyo na maisha ya kikristo.
Wakati mwamini afahamupo uwezo wake wa kukua atakuwa na hamu ya
kupokea ukweli zaidi wa Mungu kuunda mawazo yake. Tukiuacha ukosefu wa maarifa kando, hujiinua katika utukufu wa malengo ya Mungu ndani ya Kristo Yesu.
“Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, pindi wanaponiambia mchana kutwa, yuko wapi Mungu wako. Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu. Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa siku kuu” (Zaburi 42:3-4).
Kukua kunawezekana. Tunapoamini, kama Daudi, tunafuatilia kwa imani kwa kiwango kile tumo katika maisha yetu ya kiroho. Hata tutendapo dhambi kwa neema ya Mungu twaweza epuka (Zaburi 32).
Somo
- Ukuaji ulio mlegevu unaonekana kwa ukosefu wa hamu ya kukua, au kwa kuamini kwamba ukuaji hauna maana au umuhimu.
- Iwapo waamini wataona kukua kiroho kwawezekana hamu yao ya kukua huimarika.
- Zaburi 42:3-4
- 1 Yohana 2:1-3
Zoezi
- Je, watu ni wenye bidii kujifunza neno la Mungu karibu nawe? Kagua shauri ya wale waohudhuria mikutano ili kujifunza, kuomba na kuabudu.
- Je, unashauku kiasi kipi kujifunza na kukua? Ni katika maeneo yapi ungekuwa na nguvu zaidi? Je, unafikiri una nafasi ya kukua katika maeneo hayo? Eleza.